Tulonge

Na sisi wanaume tuna haja ya kuwa siku ya wanaume kama ilivyo siku ya wanawake?

Kwa nini kuna women's day lkn hakuna men's day? Kuna haja ya kuwa na siku ya wanaume??

Views: 857

Reply to This

Replies to This Discussion

Mmmh.. sina uhakika na hilo...
hakuna haja wanaume wanawajibika zaidi kwa wanawake katika siku zote za mwaka si busara kuwa na siku maalum

08 March 1911 (miaka 100 iliyopita) kipindi siku ya wanawake ilipoanzishwa karibu nchi zote duniani wanawake walikuwa hawaruhusiwi kupiga kura, hawakuruhusiwa kwenye masuala ya maamuzi, hawakuruhusiwa kushiriki kwenye nyanja za kisiasa, hawakuruhushawa kufanya kazi maofisini, hawakuruhusiwa kusomea professionals nyingi isipokuwa ualimu na u-nurse tu nako na hata hivyo ni nchi za magharibi. Kipindi hicho ilikuwa ni mfumo dume kwenye nyanja zote. Hivyo siku hii ya wanawake ilipoanzishwa ilikuwa ni kuunganisha wanawake wote bila kujali utaifa ili na wao watambuliwe na kuthaminiwa kuwa ni part ya society na vile vile ni kiungo kikubwa katika familia. Kumbuka hadi leo tunapoengea kumekuwa na matendo mengi ya ukiukwaji wa haki za binadamu juu ya wanawake. Mwanamke anapigwa na mumewe wakati mwingine kukatwa masikio, mikono, midomo au kupoteza maisha kwa kosa dogo tu.

Moto wa siku ya wanawake mwaka huu wasema 'Every MOTHER counts'. Lengo lake ni kutambua tatizo linalowapata wanawake wajawazito na kupelekea vifo vingi (kila sekunde mwanamke afa kwa uzazi) kwa wanawake wanapokuwa wanajifungua hasa nchi za sub Sahara Africa ambako serikali zetu zimesahau kabisa kudumisha huduma hii ingawa kumekuwa na misaada mingi toka nchi za west ili kusaidia kudumisha huduma ya kina mama na wajawazito.

Kwa maelezo hayo mdau Severin unafikiri kuna umuhimu kweli wa kuwa na siku ya wanaume kama ilivyo ya wanawake????

Kwa mimi naona hakuna haja kabisa kuwa na siku ya wanaume.Kwani amuoni hao wenye hiyo siku wanaishia kupiga kelele likn hakuna lolote la muhimu zaidi ya kuendeleza utegemezi.Sisi tulishatunukiwa toka kwa Mungu na tunatekeleza kwa vitendo na tuendelee na vitendo zaidi ya maneno.
Kwa maoni yangu mimi naona hakuna haja hiyo...ukizingatia kwamba mwanamke aliumbwa baada ya mwenyezi Mungu kukonyoa ubavu wetu na kumkabidhi. Hata hivyo nasikia kwamba kuna siku ya wanaume iitwayo daddy's day ambayo sio official kama ya kina mama!

Ni kweli kaka Eddie siku ya kina baba ipo na hapa UK yatambulika. Siku ya kina baba na siku ya kina mama zasheherekewa kwa watoto kuwakumbuka wazazi wao kuwanunulia zawadi na kuwa spoil kama asante kuwaleta duniani. Tatizo siku hii ya kina baba na kina mama miaka hii ya karibuni hapa UK imekuwa too commercialized kiasi kwamba inaanza kupoteza muelekeo wake.

Na siku ya wanawake duniani iko tofauti na siku ya kina mama kwani siku ya wanawake yajumuisha wanawake wote uwe umeolewa au hujaolewa, uwe ume una watoto au huna watoto wote twasheherekea.

eddie said:

Kwa maoni yangu mimi naona hakuna haja hiyo...ukizingatia kwamba mwanamke aliumbwa baada ya mwenyezi Mungu kukonyoa ubavu wetu na kumkabidhi. Hata hivyo nasikia kwamba kuna siku ya wanaume iitwayo daddy's day ambayo sio official kama ya kina mama!

Sikutegemea mwanasheria aweza andika sentence kama hii kwenye social network. Hujalelewa Africa nini? Ina maana huoni mchango unaotolewa na kina mama/wanawake katika jamii na familia za Tanzania na Africa kwa ujumla hadi waishia kuaandika hivi?

Nakunukuu  ulivyoandika "Kwani amuoni hao wenye hiyo siku wanaishia kupiga kelele likn hakuna lolote la muhimu zaidi ya kuendeleza utegemezi".

Ila siwezi kukushutumu sana kwani wanasema kuwa kila mtu ana uhuru wa kusema kila anachokiona ni sawa machoni na moyoni mwake.

riziki matitu said:

Kwa mimi naona hakuna haja kabisa kuwa na siku ya wanaume.Kwani amuoni hao wenye hiyo siku wanaishia kupiga kelele likn hakuna lolote la muhimu zaidi ya kuendeleza utegemezi.Sisi tulishatunukiwa toka kwa Mungu na tunatekeleza kwa vitendo na tuendelee na vitendo zaidi ya maneno.
Duh! hii ndiyo raha ya kuwa na kina mama wenye busara ndani ya Tulonge.Hongera mama Malaika kwa komenti nzuri,umenijuza mengi sana.
Mnaweza mkawa nayo endapo mtaona kuna ulzima wa kuwa nayo kama ilivyo kwa wanawake. Kama na nyie mna jifungua katika mazingira magumu nk mnaweza kuanzisha ili mdai haki zenu.
sasa we Joan kwani bila wanaume nyie mngejifungua???

WANAWAKE WANA JUKUMU KUBWA SANA KATIKA JAMII,KUMUHUDUMUA MWANAUME ASIYE NA SHUKURANI,KUBEBA UJAUZITO KWA MIEZI TISA IKIANDAMANA NA HOMA ZA MARA KWA MARA ,KUTAPIKA KWA WINGI NA HATIMAYE KUJIFUNGUA KWA UCHUNGU HUKU WAKITUKANWA NA WANAWAKE WENZAO (MANESI), BADO JUKUMU LA KUMLEA MTOTO NA KUMFUNDISHA MAADILI MEAMA NI LAKE!!

TUNAPASWA KUWAHESHIMU NA KUJITAHIDI KUWAONYESHA UPENDO NA KUWATIMIZIA YALE YA MUHIMU WANAYOHITAJI!!

MAMA NI MAMA HATA AWE CHANGUDOA ATABAKI KUWA MAMA!

Nimefurahi kuona kuwa kuna watu mnajali sana mchango unaotolewa kila siku na kina mama/wanawake kwenye jamii zetu.

Alfan Mlali said:

WANAWAKE WANA JUKUMU KUBWA SANA KATIKA JAMII,KUMUHUDUMUA MWANAUME ASIYE NA SHUKURANI,KUBEBA UJAUZITO KWA MIEZI TISA IKIANDAMANA NA HOMA ZA MARA KWA MARA ,KUTAPIKA KWA WINGI NA HATIMAYE KUJIFUNGUA KWA UCHUNGU HUKU WAKITUKANWA NA WANAWAKE WENZAO (MANESI), BADO JUKUMU LA KUMLEA MTOTO NA KUMFUNDISHA MAADILI MEAMA NI LAKE!!

TUNAPASWA KUWAHESHIMU NA KUJITAHIDI KUWAONYESHA UPENDO NA KUWATIMIZIA YALE YA MUHIMU WANAYOHITAJI!!

MAMA NI MAMA HATA AWE CHANGUDOA ATABAKI KUWA MAMA!

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*