Kumekuwa na matukio mengi ya mimba zisizo tarajiwa. Unadhani nani wa kulaumiwa kati ya msichana na mvulana? Toa sababu kutetea pointi yako.
Tags:
Kwangu mimi naona kama wote wawili wanastahili kulaumiwa, kwa nini nasema hivyo. Tendo la ndoa huhusisha pande mbili kwa makubaliano yao mvulana na msichana hufanya tendo hilo. Cha kushangaza lawama zote humuangukia mwanadada kwa kuwa yeye ndiye mwenye uwezo wa kubeba mimba. Lakini je kama mkaka asinge mpa hiyo mimba ingetoka wapi??
Zama ilikuwa wavulana ndo wanawashawishi wasichana lakini kwa sasa hata wasichana huwashawishi wavulana hadi hata kuwahonga pesa na magari ili mradi tu watimiziwe haja zao. Katika hilo mimba ikipatikana unafikiri nani atalaumiwa?
Mhimu mimi naona ni kuwa na mipango madhubuti katika kupendana kwao. Maana daima jambo lisilo na mipangilio mwisho wake si mzuri, tena afadhali abebe mimba ila asipate UKIMWI!!
© 2021 Created by Tulonge.
Powered by