Tulonge

mwaka elfu mbili na nane nilichoma sindano za majira, nikawa nimenenepa sana mpaka nikaharibika shepu yangu kwani nilikuwa sio mwembamba sana na wala sio mnene ilipofika 2o10 nikaacha sindano lakini bado nimenenepa sana. naombeni ushauri rafiki zangu nifanyeje ili nirudi katika shepu yangu.

Views: 2311

Attachments:

Reply to This

Replies to This Discussion

Duh! hapa mimi siyo mtaalam sana wa hayo mambo. Ila ninachofahamu unene unaosababishwa na hizo dawa huchukuwa muda mrefu kidogo kuisha. Kuna mwenzako mmoja ilimchukua zaidi ya mwaka mmoja hadi kurudia hali yake ya kawaida. Pia alikuwa anafanya mazoezi ili arudie shepu yake.

Kwa kifupi hayo madawa siyo mazuri kivile.

Kwanza pole na matatizo yanayokupata,jambo hilo si geni kuwahi kutokea kwa nyinyi watumiaji wa sindano za majira.

ushauri wangu hapo ni kukuomba urudi hospital na ukaonane na madaktar bingwa wanahusika na matatizo ya uzazi kwa ujumla,huku ukijaribu kufanya mazoezi ya kutembea au kukimbia.Lingine inawezekana vyakula navyo vinaweza kusababisha tatizo hili nalo.

Tafadhali wasiliana na washauri wa maabara wanaweza kutatua tatizo lako

Du kwenye hilo mi sina mchango dada zaidi ya kukuambia pole na ujitahiodi kufanya mazoezi na pia kuwaendea wataalamu kwa ushauri zaidi

Duh, pole sana. Fanya fanya mazoezi na upunguze vyakula vya wanga na protein

 

Pole sana farida, hilo ni tatizo la kawaida, nashukuru ni tayari umeacha ila ungeweza kungundua mapema ingekuwa vzr zaidi nakumbuka nilishawahi kukutana na hilo tatizo ila niliacha mara baada ya kuona niko ndivyo sivyo. Usiwe na shaka mwili wako utarudi tu vzr endapo utafanya mazoezi na kuangalia vzr mlo wako taratibu utarudia kuwa na shep yako ya awali, ila ukumbuke kuwa mabadiliko ya mwili kwa mwanamke baada ya kujifungua yapo ingawa si kwa wote. kwa sasa kuna njia nzuri zaidi ambazo unaweza kutumia na madhara yasiwe makubwa naamini umeshatembelea vituo vya uzazi salama na kupata elimu tosha kama bado tembelea sasa.
nashukuru sana kwa mawazo yenu unajua ukipata ushauri hata kama hujapona lakini napata matumaini kabisa kwamba nitarudi kama nilivyokuwa zamani.jamani nawapenda wote wa tulongeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!
Pole sana dada, hebu weka picha yako tukuone ulivyo nenepa.Ukute ukibaki hivyo ndiyo unapendeza zaidi.
hivi ndivyo nilivyo sasa hivi lakini nilikuwa mwembamba, sijui rafiki wewe unasemaje?

hahaha farida umenichekesha sana leo ss kama wewe hapo ni bonge cjui mie nitasemaje lol

 

Wadau tusaidieni nani mnene kati yetu ili namie nijue kama natakiwa kuanza mazoezi haraka iwezekanavyo

Kwanza nawapongeza kwa kuwa wa wazi juu ya matatizo yenu ya kuongezeka mwili[yaani unene],lkn hapa nataka nikwambie kitu Hilda,unene au wembamba hamzuii mtu kutokufanya mazoezi .please unatakiwa uanze sasa kufanya  mazoezi kwa ajili ya afya yako.Hilda tatizo lenu mmekuwa wa tu wa aibu sana ,mnaogopa kuchekwa pindi mtakapoonekana miataani.

Nakuomba sana dadangu zingatia haya ninayookwambia,utaona faida yake                              

mwenzangu wewe ni noma aaaaaaahhhh, tena anza mazoezi umetia fola nikisema kwangu kunaungua kwa mwenzangu kunateketea hebu nione ninisimama

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*