Tulonge

mwaka elfu mbili na nane nilichoma sindano za majira, nikawa nimenenepa sana mpaka nikaharibika shepu yangu kwani nilikuwa sio mwembamba sana na wala sio mnene ilipofika 2o10 nikaacha sindano lakini bado nimenenepa sana. naombeni ushauri rafiki zangu nifanyeje ili nirudi katika shepu yangu.

Views: 2311

Attachments:

Reply to This

Replies to This Discussion

hahaha umeonaeee mm nimeanza mazoezi last saturday na pia najitahd kunywa maji moto kila mara na kupubguza vyakula vya wanga na mafuta sjui nitafanikiwa au natwanga maji kwenye kinu ila duuu unene nomaaa hauchagui pa kunenepa nanenepa kila kiungo hata ambavyo havistalili kwkwkwkwkwk

Hebu angalia hivyo kitambi uwiiiiii 

serious nisaidieni njia ya kuondoa hicho kitambi tu hata kama mwili utagoma kupungua basi.

kunywa maji yasiwe ya moto saana kila siku asubuhi ikifika saa 6 kula vipande 4 vya mkate ukiambatanisha na mchicha wa kuchemsha kwani yale maji ya moto yanatoa vitamen nyingi sana mwilini huo mkate uwe ndio lunch yako kabisa usile tena mpaka jioni na usiku ule ila sio saana bila kusahau maji yako yasiwe ya baridi yawe ya moto kiasi kila wakati yawe ndio chakula chako cha mchana mazoezi sio mpaka ukimbize upepo hata ndani unaweza chukuwa kamba ukaanza mdogomdogo  lala kifo cha mende nyoosha miguu yote huku ukiwa umeibana mikono shika kichwa chako kama kuna m2 karibu anaweza kukalia miguu ili kukupa uzito isinyanyuke kisha anza kujibeba kuamka bila kushikilia sehem ukifanya hivyo mala 10 kwa kila siku 2mbo lote linaisha.

namuomba MR TULONGE  atutafutie DR wa kijiji kwani mambo mengine ni muhimu sana yanahitaji dr atusaidie.

@Hilda kunywa maji ya uvugu vugu ndo mazuri, maji ya moto yana madhara ktk ngozi, yanafanya ngozi inasinyaa

Pole sana Farida. Upande wangu inakuwa vigumu kukupa ushauri kwani sijui lifestyle yako (chakula gani, kazi/shughuli ufanyazo, vinywaji unavyokula, etc.)

Kwa wote (Farida na Hilda) nachowaomba ni kuangalia chakula manachokula. Chakula ni uhai lakini ni vizuri kuangalia nini unaingiza kwenye mwili wako ni kitu muhimu sana kwa maana hiyo kama ulikuwa unapendelea kunywa soda sasa yapasa kuziacha na kuhamia kwenye maji ya chupa, kama mwaona ni vigumu basi muanze kupunguza kidogo kidogo na baadae mtazoea. Na badala ya chips (for lunch) ahamia kwenye matunda au wali/ugali na mboga mboga. Ngoja nitafute site nzuri ajili ya Farida na Hilda, itawasaidieni kwa njia moja au nyingine upande wa chakula. Pia kama unakunywa bia acha kwa muda kwani bia yasaidia kukuumua (yaongeza kitambi). Chaoga asije nisikia hapa akanitia makwenzi bureee. LOL....

Na kubwa zaidi ni mazoezi. Kwani wengi wetu kazi tunazofanya ni za kukaa kwenye kiti siku nzima hivyo calories tunazozisindilia mwili (through food) hazipingui. Hivyo mazoezi pekee ndio yanasaidia kuzipunguza uzito na kupunguza mafuta mwilini. Hivyo jitahidini kutembea, kufanya kazi majumbani (kupiga deki nyumba nzima huku umeinama na kubana misuli ya tumbo lako ni zoezi tosha kukutoa jasho). Na hata kama mazoezi ni vyema kufanyia nje kwani kuna oxgen ya kutosha na sio ndani, wenzetu wazungu wanafanyia mazoezi ndani (gym) sababu hali ya hewa muda mwingi haiwaruhusu kwao. Kipindi cha summer wazungu wanakimbia nje mabarabarani na kufanya mazoezi ya viungo kwenye parks, kipindi cha winter wanahamia ndani (gym).

Kazana na mazoezi, mabadiriko hata kama usipoyaona sasa subiria baada ya muda utayaona.

Chngulia kwenye hii link yaweza kukusaidia

http://www.bbc.co.uk/health/treatments/healthy_living/your_weight/a...

http://www.bbc.co.uk/health/treatments/healthy_living/your_weight/Hilda Masaure said:

hahaha umeonaeee mm nimeanza mazoezi last saturday na pia najitahd kunywa maji moto kila mara na kupubguza vyakula vya wanga na mafuta sjui nitafanikiwa au natwanga maji kwenye kinu ila duuu unene nomaaa hauchagui pa kunenepa nanenepa kila kiungo hata ambavyo havistalili kwkwkwkwkwk

Hebu angalia hivyo kitambi uwiiiiii 

serious nisaidieni njia ya kuondoa hicho kitambi tu hata kama mwili utagoma kupungua basi.

Mnaojisema wanene hapa kwa hawa manjemba wawili hamuoni ndani. Wazungu kinachowaumua ni mavyakula yao ma-junk food (sausages, chips, piza, crisps, etc.) na ya kwenye packets, wakija kwetu bongo wanapenda kula vyetu vya asili sababu ni vyakula vizuri vyenye afya na pia fresh.

Hahaahaahahaaaa yani hiyo mijamaa inawaza kula tu katika maisha yao. Wapo kama Chaoga.

Mama Malaika said:

Mnaojisema wanene hapa kwa hawa manjemba wawili hamuoni ndani. Wazungu kinachowaumua ni mavyakula yao ma-junk food (sausages, chips, piza, crisps, etc.) na ya kwenye packets, wakija kwetu bongo wanapenda kula vyetu vya asili sababu ni vyakula vizuri vyenye afya na pia fresh.

Noted, nitawatafutia dokta soon. Ila naona hata Mama Malaika anaweza kuwa dokta wa tulongee kwa sasa teh teh teh

Omary said:

kunywa maji yasiwe ya moto saana kila siku asubuhi ikifika saa 6 kula vipande 4 vya mkate ukiambatanisha na mchicha wa kuchemsha kwani yale maji ya moto yanatoa vitamen nyingi sana mwilini huo mkate uwe ndio lunch yako kabisa usile tena mpaka jioni na usiku ule ila sio saana bila kusahau maji yako yasiwe ya baridi yawe ya moto kiasi kila wakati yawe ndio chakula chako cha mchana mazoezi sio mpaka ukimbize upepo hata ndani unaweza chukuwa kamba ukaanza mdogomdogo  lala kifo cha mende nyoosha miguu yote huku ukiwa umeibana mikono shika kichwa chako kama kuna m2 karibu anaweza kukalia miguu ili kukupa uzito isinyanyuke kisha anza kujibeba kuamka bila kushikilia sehem ukifanya hivyo mala 10 kwa kila siku 2mbo lote linaisha.

namuomba MR TULONGE  atutafutie DR wa kijiji kwani mambo mengine ni muhimu sana yanahitaji dr atusaidie.

Disma weye. Ha haa haaaaaaa

Mie sio doctor wa medicine au nutritionist bali niko kwenye professionals nyingine. Ukisema mambo ya uchumi, biashara au mapping hapo nitawasaidieni kwani ndio niliyosomea. Kuhusu masuala haya ya kupunguza uzito ni bora ututafutie nutritionist awe anatushauri humu Tulonge, na wengine walio na ideas vile vile ni bora wachangie hata kama sio wataalamu wa masuala haya.

duh,dada umenikumbusha ule wimbo wa mr Profesa Jay aliposema nikusaidieje,lakini siwezi kukosa jinsi ya kukusaidia.na weza kusema zingatia mazoezi kama alivyoashiria kaka Tulonge.Mazoezi ndio mmkombozi wa hilo.ukiendeleza mazoezi kila siku dakika kadhaa basi kwa fulani mwili utapungua na kurudia kiwango chake.na hii ndio njia inayoashiriwa na wataalamu wengi kimataifa,wengi hushauliwa kuingia kwenye GYM ili kufanya mazoezi ya viungo ikiwa ni kwalengo la kupunguza mwili.na kuna wanene ambao kweli wamefanikiwa kupitia njia ya kujizoesha mazoezi na kula vyakula visivyokuwa vya kunenepesha kupunguz mwili wao na kurudia hali ya zamani.

enewei,pole sana n ani imani utarudisha mwili wako.

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*