Tulonge

msahada mi nandugu yangu anasumbuliwa na figo na inahitajika abadilishiwe figo lake moja co nahitaji kujua itachukuwa kiasi ngani cha fedha kununua hilo figo na ninaweza kulipata wapi naumbeni msaada kwa hilo

Views: 2086

Reply to This

Replies to This Discussion

Kwaiyo wewe umekuja Tulonge kutafuta marafiki wa kukuuzia figo umeambiwa zinauzwa Tulonge?  Kama vipi mpatie yakwako humu hakuna anayeuza au anayejua zianauzwa wapi nasikia unawakomalia watu sana kuhusu hili.  We umesikia figo ni damu mtu anatoa tu au? Unaishi wapi wewe inaonekana kwanza hata kiswahili hujui vema acha kuharibia watu siku hakuna mwenye figo we kama vipi toa yako moja mpe nduguyo.

Pole kwa matatizo Chris, binafsi sina idea yoyote juu ya hilo

Hospitali hiyo  waliyokuambia kuwa inahitajika figo basi watakupa msaada wa wapi pa kupata.

SUALA LA KUMGAWIA MTU FIGO NI LA KIBINADAMU NA NI JAMBO LA UPENDO ZAIDI KULIKO GHARAMA ZA PESA UNAZOTAKA KUTOA KWA HIYO NINGEKUSHAURI NYIE NDUGU ZAKE NDO MUMPE BILA GHARAMA YEYOTE NAIMANI MTAKUA MNAMPENDA NDUGU YENU KULIKO MTU MWINGINE YEYOTE. USITANGAZE HIYO BIASHARA YA VIUNGO VYA BINADAMU NI HARAMU NAJUA KUNA WATANZANIA WAMECHOKA WATATAMANI KUFANYA HIYO BIASHARA HARAFU ITATUPA SHIDA BAADAYE IKIKOMAA.

Mtu akiwa mgonjwa au akiwa anauguliwa hua anakuwa desperate sana, lugha mliyotumia baadhi ya wachangiaji sio nzuri coz huwez kujua dk aliwaambiaje, inawezekana figo zao hazifai kuwa transplanted kwa mgonjwa n.k. Instead ya kumkatisha tamaa mngetumia tu lugha nzuri coz matatizo ni yetu wote binadamu, leo kwake kesho kwetu sie......pole sana kwa kuuguliwa naamini mungu atawasaidia mtaweza kulivuka hili jaribu coz upendo mlio nao kwa ndugu yenu mungu anaujua na hawezi kuwaacha bure,

Ni vena wanadamu tukajua juu ya swala shida na mahangaiko kama aliyonayo uyu jamaa, lakini anachotakiwa kujua kuwa kutoa ni moyo na si utajiri na hivyo mtu kutoa figo si kitu ambacho unaweza kuongea kibishara kama hivyo bali inapasa aongee kwa namna ya kutaka apewe msaada tuu hata kama atapewa fedha lakini haiwezi haiwezi kufanana na thamani ya figo maana huo ni uhai.

Kweli kbs @ Trien. Pole sana Chris.

Hilo swala hapa sio mahala pake, Tulonge hatuna biashara ya figo. Nakushauri nenda hospitali mbalmbal esp.mhimbili watakuelekeza utaratbu wa kupata figo...  Lakini pia kwa nin usimpatie ya kwako huto nguguyo,?  kiufupi swala lako ni gumu sana. ila  kama una maana nyngne tofauti fungua pin code zako tukusome vema

Ni uhakika utakuwa umepata wazo-chukua hatu

Hee! kumbe tulonge ni sehemu ya kupashana habali za furaha tu sio matatizo?

Hapana Geoffrey, hata matatizo tunasaidiana ndomaana kuna kuna mfuko wa kuchangia watoto yatima. Check hapo

http://tulonge.com/group/mfukowawatotoyatima

Na hapo chini pia kuna jambo linalohusu kusaidiana
http://tulonge.com/forum/topics/n

Doh! kiukweli inawezekana mwenzetu anauguliwa au amekuja kutupima imani ila dunia kwa sasa imehalibika mno humjuinani mzuri nani mbaya hivyo inatupa woga kuamini moja kwa moja pili wewe ni mgeni hapa kijijini so tunajiuliza kama isingekuwa ugonjwa usingeingia hapa kijijini? je nani kakuelekeza kijiji hiki? na umekijuwa kwa muda gani? kigine hata sura yako umeificha tutakuaminije? kiukweli unatia mashaka,

hakuna mwanaadam anaeomba maradhi yote kaleta MUNGU hivyo tunakupa pole sana kwa kuuguliwa mimi nakuombe MUNGU amuafu mgonjwa wako INSHALLAH atapona bila kuwekewa figo ya mtu mwengine kwa MUNGU hakuna kisichowezekana yote yanawezekana na usione kama wana tulonge hawana msaada la tuna msaada tuna huruma tuna upendo wa hali ya juu ila the way ulivyokuja ulikuja kimasihara kwani kuja na kuomba figo lazima umshtuwe kila mtu na ulichokiomba sio kitu kidogo ni uhai wa mtu maana hata atakaetowela hiyo figo 1 hatakuwa mzima kama mwanzo utakuwa umemtia ubovu

ndio watu wakashtuka kwa upendo tulionao hakuna mtu anaona mwana tulonge anatolewa figo yake kwa kitu pesa eti kauza?  hapa kwetu mwana tulonge 1 anathamani kubwa sana kwetu na si tu mwana tulonge kila mwanaadamu anathamani kubwa sana kwetu kwani MUNGU pekee ndio mwenye kila sababu ya kuleta hapa duniani na kila sababu ya kumuondoa hapa duniani.

 

POLE SANA TUNAMUOMBEA MGONJWA MUNGU AMUAFU INSHALLAH.

TATIZO HUYO NDG HAJAOMBA MSAADA  ANATAKA KUJUA ZINAKOPATIKANA, BEI YAKE NA ATANUNUA.SASA HUYU ANATANGAZA BIASHARA YA FIGO TUWE MAKINI LABDA BIASHARA ZA NGOZI ZA BINADAMU,VIUNGO VYA SIRI NA VIUNGO VYA ALBINO ILIANZA HIVI.

Reply to Discussion

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*