Tulonge

Sina mengi ya kuandika; ila kila nikijenga picha ya enzi za Yesu kupitia maandiko matakatifu--huwa napata shauku sana kuwa ningezaliwa kipindi hicho. Nahisi maisha yalikuwa mazuri zaidi, yalikuwa halisi zaidi kulinganisha na maisha ya dunia ya sass.

Vp, mdau/wadau mna mchango/maoni gani juu ya hili?

Views: 1239

Reply to This

Replies to This Discussion

Ungekuwa ulishakufa zamaniiiiiiiiii

Kama ulisha badilishwa jina na kuitwa MAREHEMU
Cha the Omniscient nilisha kwambia hili jina lako linatutisha kiasi kwamba nakuogopa. Lol.....

Kuhusu hoja yako kuwa "Maisha yalikuwa mazuri zaidi, yalikuwa halisi zaidi kulinganisha na maisha ya dunia ya sasa" unasema ukiwa pande ipi? Ukiwa kama mwanafunzi na mfuasi wa Yesu enzi hizo au mtu wa kawaida na mlala hoi enzi hizo??
Samahani kwa kukuuliza, nashindwa kujibu moja kwa moja bila kuelewa uzuri.
Hm... Kwa upande wangu nikichambua maisha enzi hizo, upande wa "simplicity of life" naweza kubaliana nawe kwani enzi hizo mtu wa kawaida alihitaji vitu muhimu tu: chakula, sehemu ya kulala na pia kumiliki mifugo hasa kondoo ajili ya chakula na manyoya ambayo walijitengenezea nguo nguo zao. Mtu wa kawaida wa sasa ukiacha hivyo vitu muhimu anataka mobile phones, TV aangalie Premier League, n.k. Ha haa haa haaa.....

Lakini nikija kwenye "humanity" nina mashaka kwani maisha enzi hizo hazikuwa tofauti sana na dunia ya leo. Kulikuwa na matajiri ambao hawa kujali binadamu wenzao na watu waliishi kimatabaka sana. Kulikuwa matatizo ya udini (Wayahudi dhidi ya Yesu mara wapagani ambao walikuwa warumi vs wayahudi). Na hiyo ilisabusha kifo cha Yesu kisa mafundisho yake yako against na wengine. Wafuasi wake wengi waliteswa na kuawa na warumi pia wayajudi. Kulikuwa na ukabila/ethnic groups kitu ambacho kilizua matatizo kila wakati, ila Yesu hakuwabagua. Pia ukisoma maandiko matakatifu unasikia habari za watumwa, wakoma, vipofu na omba omba, makahaba/malaya ambao walikemewa na Yesu. Kulikuwa na uasherati, ulevi, n.k. Maandiko yameandika wanawake waliokuwa wakiomboleza vifo/mauaji ya waume zao na wengine mauaji ya watoto wao. Na hiyo ilitokea kwa wanawake kuanzia kabla Yesu hajazaliwa (Rachel aomboleza mauaji ya watoto wake, Book of Jeremiah) na hadi kipindi cha Yesu alipokufa (twasoma jinsi Mary alia kwa uchungu akishuhudia kifo cha mwanae Yesu pale msalabani). Kulikuwa na vita mara kwa mara kati ya Wayahudi na wakoloni wao wa-Rumi (Roman Empire).
Kulikuwa na ruthless leaders ambao waliua hadi watoto wao wa kuzaa. Na wengine waliua vitoto vidogo visivyo hatia. Mmoja wao ni mfalme Herod (Herod the Great) aliyetawala Judea (Israel Kingdom), alipata kuwa na wake 10 na watoto kibao. Herod ameandikwa kwenye maandiko matakatifu St Matthew's Gospel 2, imeandikwa kuwa aliamurisha watoto wote wadogo wa kiume walio chini ya umri wa miaka 2 wauawe. Na Mtoto Yesu alikuwa ni miongoni ya watoto wa umri huo huko Judea kipindi hicho, karibu watoto wote waliuawa, maandiko yanasema kuwa Mtoto Yesu alipona baada ya wazazi wake kuondoka kimya kimya na mtoto wao kukimbilia Misri (Afriica). Hivyo Cha the Omniscient iwapo ungezaliwa kipindi hicho, na jinsi ulivyo mjanja mjanja na mwana mapinduzi siajabu na wewe ungeuawa na Herod the Great au watawala wengine wa enzi hizo. Ha haa haa haa haaa......

Oops... Halafu nimesahau, maandiko yametaja watoza ushuru. Watoza ushuru enzi hizo walikuwa matajiri sana kwa huo ushuru/kodi waliyotoza/wakamua masikini. Hawakutoza matajiri wenzao. Na hii haina tofauti na watoza ushuru wa sasa (e.g. TRA, viongozi).

nazani mie ndie ningekuwa miongoni mwa wafuasi wake wa kwanza yesu, ile divai aisee mie ndie ningekuwa mshika birika la kumiminia wengine...siku hizi pombe unanunua bwana...bora ningezaliwa kipindi hicho nakuunga mkono CHA.....Teh teh teh teh

Teh teh teh Chaoga ulevi utakumaliza. Mama Malaika naona umeshusha gazeti(mzalendo), ngoja nikavae miwani nije kusoma then na mimi nichangie

Yani ungezaliwa kipindi cha sodoma na gomola ungelijua hilo jiji.. teheheheeee

Ha haaa haaaa... Pole Dismas. Na hapo sijagusia nafasi ya mwanamke ndani ya ndoa. Na vidume enzi hizo ni ndoa za mitala, na mitala wengine walioa hadi wake 20 na kuishi nao pamoja ndani ya nyumba. Maisha hayo nisingeweza hata kidogo. Ha haaaTulonge said:

Teh teh teh Chaoga ulevi utakumaliza. Mama Malaika naona umeshusha gazeti(mzalendo), ngoja nikavae miwani nije kusoma then na mimi nichangie

Chaoga wewe chiboko. Siajabu ungemsaliti Yesu kwa kupewa glass moja tu ya divai na wayahudi. Teh teh teh

chaoga said:

nazani mie ndie ningekuwa miongoni mwa wafuasi wake wa kwanza yesu, ile divai aisee mie ndie ningekuwa mshika birika la kumiminia wengine...siku hizi pombe unanunua bwana...bora ningezaliwa kipindi hicho nakuunga mkono CHA.....Teh teh teh teh

Mama Malaika-dada yangu, you are a superb lecturer. Ndio maana basi Dismas ameishia tu kusema namnukuu "Mama Malaika naona umeshusha gazeti(mzalendo), ngoja nikavae miwani nije kusoma then na mimi nichangie". Hii inaonesha ni namna gani ambavyo maoni yako yalivyoshiba.

Naomba uendelee kuchangia pale ulipoishia--then nitarudi na jibu lako.

Dixon--sina la kusema.

Chaogga, umenichekesha mpaaaka baaasi; yaani siku tukikutana katika ile TULONGE PARTY---bili zote za Konyagi utakazotumia, zitakuwa zangu--I promise.

Ungekuwa katika kumbukumbu za maandiko matakatifu.

Ha ha ha wapendwa kwa nini wengine mnasema ingekuwa ni marehemu iwapo ningezaliwa enzi za Yesu?

Naombeni majibuzzz!

 

Reply to Discussion

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*