Tulonge

Ndugu wadau nikisema TULONGE.COM ya Dismas inatokana na FOTOBARAZA.COM ya Babukajda, nina hakika sintakuwa nimekosea. Hili hata Dismas mwenyewe analitambua--au niseme kuwa mimi kujuana na Dismas, Alfan, Angela, Chaoga, ALex Magere, Mama Malaika, Lucy wa Mama, na wengineo wengi ambao wanakaribia elfu moja ni kutokana na FOTOBARAZA ya BabuKadja. Na hata leo hii uwepo wa TULONGE unatokana na Fotobaraza ya Babukadja.

La kushitusha ni kwamba; leo yaani tarehe 4-3-2012 nilipojaribu kutembelea kijiji kile cha jirani (FOTOBARAZA) nilikutana na ujumbe unaoashiria kupotea kwa kijiji cha fotobaraza katika ulimwengu wa social network.

Ujumbe ulikuwa unasema "This Network is overdue in payment and at risk of being disabled".

Nilijaribu kumtafuta Babukadja ili nipate kujua zaidi juu ya hili, lakini all my efforts ended up in vain.

Wasiwasi wangu ni kuwa; marafiki ambao tulikuwa nao kule na hawajui ni wapi watatufuata wenzao tulipo, wanaweza kupotezana na sisi. Hivyo ombi langu ni kuwa tuwape taarifa ya kuwepo kwa kijiji hiki cha TULONGE.COM, hii itasaidia kuendeleza urafiki wetu uliodumu kwa takribani miaka mitano sasa. Mpe taarifa rafiki kwa njia yeyote ile, ilimradi tu atambue uwepo wa TULONGE.COM

MAONI YANGU

Maoni yangu kwa mkuu wa kijiji hiki na wadau wenye mapenzi mema na kijiji hiki ni kuwa, tufanye hima kwa maana ya kuitisha HARAMBEE kwa ajili ya kijiji ili tu tuweze kuepukana na kile ambacho naamini kinaweza kutokea kwa FOTOBARAZA siku chache zijazo.

Nina hakika kuwa; wapo wadau kwa kuwataja kwa uchache kama vile DIXON KAISHOZI, CHAOGGA, PASCAl aka MABAGALA, ANGELA, ALFANI, CRYSTER na wengine wengi ambao wapo teyari kuchangia chochote pale watakapoombwa kufanya hivyo. Haiitaji kuwa na pesa kama REGINALD MENGI ili kucangia. NI moyo tu. Binafsi nipo teyari kuchangia chochote kwa ajili ya kijiji, na mwisho nipendekeze kuwepo mradi utakaowezesha kijiji kujipatia pesa kwa ajili ya kujiendesha na si tu kutegemea pesa toka mfukoni mwa DISMAS. Si mbaya hata products za PamoJah zikitumika kutunisha mfuko kwa ajili ya pesa za kuendeshea kijiji. Maana yangu ni kuwa; pesa zitakazopatikana kutokana na mauzo ya products za PamoJah kwa maana ya STICKERS, T-SHIRTS, na products zingine asilimia fulani itatumika kutunisha mfuko maalum kwa ajili ya kuendeshea kijiji. Hii itawahusisha hata wadau waliopo nje ya nchi--Mama Malaika, Dunda, Magere, Chibiriti, Mary Wa Mkumbo na wengine wengi.

Nimalizie kwa kusema "PamoJah We Can" Keep on Moving.

Amani kwenu wote.

Views: 1434

Reply to This

Replies to This Discussion

Hata mimi nashindwa kuelewa kwanini Kijiji kimekufa....hakisikiki kabisa, Babu sijui yupo wapi tena hatumsikii kabisa.

dah kwa kweli nimeshindwa kuielewa kabisa kwangu namaanisha ndo imekufa ila natumai ikifufuka nitajulishwa ili niweze kurejea tena. KILA LA KHERI FOTOBARAZA

Naungana na Cha kwa maoni yake.. Najua kuna gharama za kuendesha hiki kijiji ambazo inambidi Dismas aingie mfukoni kwake ambazo inabidi tusaidiane ili tuweze kufaidi yale mema tunayo yapata kwenye kijiji chetu. Kama hutajali bwana Dismas unaweza kuweka wazi gharama zilizopo ili tuchangiane yasije yakatukuta kama ya pale kijiji jirani.. naogopa na sipendi kabisa kupoteza NDUGU zangu nilionao hapa!!

Teh teh teh hamna noma mzee Dixon, mimi yakinifika shingoni nitasema mapemaaa.Ila kwa sasa ngoja niendelee kukomaa peke yangu mdogo mdogo.

Lkn huwezi jua kama ni payment issues ndiyo zimefanya kijiji jirani kifikie hatua hii. Yawezekana ni sababu nyingine. Pia bado kuna muda wa kukifanya kikiji kiendelee kuwa hewani,siyo kwamba kimeshakufa kabisa.Dixon Kaishozi said:

Naungana na Cha kwa maoni yake.. Najua kuna gharama za kuendesha hiki kijiji ambazo inambidi Dismas aingie mfukoni kwake ambazo inabidi tusaidiane ili tuweze kufaidi yale mema tunayo yapata kwenye kijiji chetu. Kama hutajali bwana Dismas unaweza kuweka wazi gharama zilizopo ili tuchangiane yasije yakatukuta kama ya pale kijiji jirani.. naogopa na sipendi kabisa kupoteza NDUGU zangu nilionao hapa!!

Hihihihiii... Nimekuelewa vizuri Kaka Dismas.. Sawa.. mimi nipo tayari kwa mchango utakao itajika.. Mambo yakiwa shingoni tustuane tu!! Siku njema!

jamani tuwe pamojah ktk shida na raha, tupendane kama mungu anavyotupenda yeye, na tushilikiane kama mungu anavyotushirikisha tulonge, tulonge isitupoteze marafiki leo na hata kesho, umoja ni nguvu na utengano?

Duh! hii news imekaa suprise!Sasa inakuwaje Botobaraza inataka kukata roho wakati bado sijamaliza kutoa virago vyangu?!

Nilikuwa nahama mdogo mdogo lakini sasa itabidi nifanye faster ,yaani mhamo inabidi uwe ule wa Tandika to Mbagala,ule wa kubeba kila kitu cha kwako,humuachii mwenye nyumba hata kijiko!!.

Enewei napita tu nitarudi tena kucomment,hapo sijakomenti nilikuwa nagusa gusa tu,ngoja nimeze mate kwanza then nitarudi kutoa maoni.

Kiukweli news hii kwangu imekuwa ya kush2wa sana maana kiukweli kila aliopo hapa kama si wote ila asilimia kubwa tumetoka fotobaraza je tunaweza kumtafuta muasisi wetu na kujuwa kilichojili huenda tukipata kujuwa kinacho tunaweza kufanya jitihada za ziada za kuweza kukinusuru kijiji chetu pendwa. Babu popote ulipo jitokeze wajukuu zako tunahitaji kujuwa kitu toka kwako Tafadhali.

Mr Tulonge pls pls tafuta kamfuko katakakoweza kuendesha kijiji maana napata woga kupoteza ndugu zangu

Mama,Angela,Alfan,Chaoga,Dixon,Chalii,siwezi kuwamaliza wote jamani tupo wengi kama mjuwavyo umoja ni nguvu utengano ni Dhaifu hivyo kwenye umoja wetu naamini tunaweza chochote tutakachotaka kufanya kinawezekana ilimladi tuwe na lengo moja.  TULONGE me nitakuja mpaka geto kama utakuwa na nia ya kutusambaratisha sema tu kwa Babu sipajui ningefanya maandamano ya pekeangu mpaka kwa Babu nikamuuliza maswali 2 tu. 

Kama Omary mimi sina chakuongezea.. siku ukiwa unaandamana kwenda kigamboni .. nifahamishe nibebe bango langu.. Nakuunga mkono kwa asilimia zote.

Teh teh teh,Pamoja sana wadau wote.

ha haaahaa,chalii a.k.a ILYA,kweli wewe umenichekesha sana ,kwa hiyo baada ya kusikia fotobaraza inataka kukata roho wewe umerudi kuchukuwa kilicho chako.ha haaaa haaa,yaani umenikumbusha ngoja na mimi ni wahi faster nikabebe vifurushi vyangu ha aaahaaa.

Chalii_a.k.a_ILYA said:

Duh! hii news imekaa suprise!Sasa inakuwaje Botobaraza inataka kukata roho wakati bado sijamaliza kutoa virago vyangu?!

Nilikuwa nahama mdogo mdogo lakini sasa itabidi nifanye faster ,yaani mhamo inabidi uwe ule wa Tandika to Mbagala,ule wa kubeba kila kitu cha kwako,humuachii mwenye nyumba hata kijiko!!.

Enewei napita tu nitarudi tena kucomment,hapo sijakomenti nilikuwa nagusa gusa tu,ngoja nimeze mate kwanza then nitarudi kutoa maoni.

HAhahahaahahahah! Mkuu Chalii umenichekesha sana. Wahi kabla kijiji hakijavunjwa ukapoteza vitu vyako..

Chalii_a.k.a_ILYA said:

Duh! hii news imekaa suprise!Sasa inakuwaje Botobaraza inataka kukata roho wakati bado sijamaliza kutoa virago vyangu?!

Nilikuwa nahama mdogo mdogo lakini sasa itabidi nifanye faster ,yaani mhamo inabidi uwe ule wa Tandika to Mbagala,ule wa kubeba kila kitu cha kwako,humuachii mwenye nyumba hata kijiko!!.

Enewei napita tu nitarudi tena kucomment,hapo sijakomenti nilikuwa nagusa gusa tu,ngoja nimeze mate kwanza then nitarudi kutoa maoni.

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*