Tulonge

Ndugu wadau nikisema TULONGE.COM ya Dismas inatokana na FOTOBARAZA.COM ya Babukajda, nina hakika sintakuwa nimekosea. Hili hata Dismas mwenyewe analitambua--au niseme kuwa mimi kujuana na Dismas, Alfan, Angela, Chaoga, ALex Magere, Mama Malaika, Lucy wa Mama, na wengineo wengi ambao wanakaribia elfu moja ni kutokana na FOTOBARAZA ya BabuKadja. Na hata leo hii uwepo wa TULONGE unatokana na Fotobaraza ya Babukadja.

La kushitusha ni kwamba; leo yaani tarehe 4-3-2012 nilipojaribu kutembelea kijiji kile cha jirani (FOTOBARAZA) nilikutana na ujumbe unaoashiria kupotea kwa kijiji cha fotobaraza katika ulimwengu wa social network.

Ujumbe ulikuwa unasema "This Network is overdue in payment and at risk of being disabled".

Nilijaribu kumtafuta Babukadja ili nipate kujua zaidi juu ya hili, lakini all my efforts ended up in vain.

Wasiwasi wangu ni kuwa; marafiki ambao tulikuwa nao kule na hawajui ni wapi watatufuata wenzao tulipo, wanaweza kupotezana na sisi. Hivyo ombi langu ni kuwa tuwape taarifa ya kuwepo kwa kijiji hiki cha TULONGE.COM, hii itasaidia kuendeleza urafiki wetu uliodumu kwa takribani miaka mitano sasa. Mpe taarifa rafiki kwa njia yeyote ile, ilimradi tu atambue uwepo wa TULONGE.COM

MAONI YANGU

Maoni yangu kwa mkuu wa kijiji hiki na wadau wenye mapenzi mema na kijiji hiki ni kuwa, tufanye hima kwa maana ya kuitisha HARAMBEE kwa ajili ya kijiji ili tu tuweze kuepukana na kile ambacho naamini kinaweza kutokea kwa FOTOBARAZA siku chache zijazo.

Nina hakika kuwa; wapo wadau kwa kuwataja kwa uchache kama vile DIXON KAISHOZI, CHAOGGA, PASCAl aka MABAGALA, ANGELA, ALFANI, CRYSTER na wengine wengi ambao wapo teyari kuchangia chochote pale watakapoombwa kufanya hivyo. Haiitaji kuwa na pesa kama REGINALD MENGI ili kucangia. NI moyo tu. Binafsi nipo teyari kuchangia chochote kwa ajili ya kijiji, na mwisho nipendekeze kuwepo mradi utakaowezesha kijiji kujipatia pesa kwa ajili ya kujiendesha na si tu kutegemea pesa toka mfukoni mwa DISMAS. Si mbaya hata products za PamoJah zikitumika kutunisha mfuko kwa ajili ya pesa za kuendeshea kijiji. Maana yangu ni kuwa; pesa zitakazopatikana kutokana na mauzo ya products za PamoJah kwa maana ya STICKERS, T-SHIRTS, na products zingine asilimia fulani itatumika kutunisha mfuko maalum kwa ajili ya kuendeshea kijiji. Hii itawahusisha hata wadau waliopo nje ya nchi--Mama Malaika, Dunda, Magere, Chibiriti, Mary Wa Mkumbo na wengine wengi.

Nimalizie kwa kusema "PamoJah We Can" Keep on Moving.

Amani kwenu wote.

Views: 1434

Reply to This

Replies to This Discussion

Nimeipenda hii mkuu Pascal

Saint Pascal of Zanzibar said:

Kila kilichozaliwa kitaonja mauti.

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha Pascal unasema kilakilichozaliwa kitaonja mauti, kwa hiyo hata chupa ya beer unayokunywa itaonja mauti. Tehe tehe tehe!

Saint Pascal of Zanzibar said:

Kila kilichozaliwa kitaonja mauti.

Ha ha ha ha ha ha. Omary wewe ni noma.

Safi sana ,Alfani nimeipenda sana hii.PamoJah we can.

Alfan Mlali said:

Unajua ukimuombea mwenzio mabaya siku zote yanaweza yakakurudia wewe.Chunga sana!!

Baada ya Fotobaraza kuzimia kipindi cha nyuma, Dismas akaona tusipotezane akaanzisha kijiji hiki cha Tulonge ili kutuweka pamoja. Kwa bahati nzuri Fotobaraza ikamwagiwa maji ya barafu ikazinduka na kuwa hai tena na wadau tukafurahi maana tukawa tuna vijiji viwili vinavyoshirikiana. Kibaya kilichojitokeza ni kwamba wenzetu ambao hawakupenda tulonge iwepo wakawa wanapiga vijembe na kuponda kuanzishwa kwa kijiji cha tulonge kiasi kufikia kusema kuwa kitakufa muda si mrefu kwa sababu wadau wote ni waliokuwa fotobaraza. Lakini walishindwa kujua kuwa waliokuwa wanakiweka kijiji kile "alive" ni wadau hao hao waliounga mkono uwepo wa tulonge na waliogoma ni wadau ambao sio active sana matokeo yake kijiji kile kikakosa mvuto na nadhani ikapelekea na Mwenyekiti kukosa ari ya kukiendesha. Nina imani Tulonge kitazidi kudumu na kuimarika siku hadi siku ukitilia maanani kuwa wadau wake wengi ni wastaarabu na wanaopenda kushirikiana. Mungu Ibariki Tulonge daima..Pamojah We Can Change the World.

Naungana na ushauri au maoni ya Cha,nadhani tumpe muda Dismas wa kufikiria  kuhusu sisi kuchangia  kijiji chetu cha tulonge,pale atakapo ona anahitaji msaada wetu basi asisite kutujulisha tupo tayari kwa hilo.Ni kweli  baada ya Fotobaraza kuyumba na kuzimika kipindi kile ,Dismas alipata kazi kubwa sana kututafuta na kuturudisha tena katika hali hii ya kuwa pamoja tena.Umoja ni Nguvu.

Cha the Great said:

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha! Alfan na Chalii inaonesha mlikunywa soda zinazolewesha before kuchangia. NImecheka sana. Kwa hiyo Chalii unataka kuhamisha kila kilicho chako pale fotobaraza?

Anyway, wadau kikubwa ni kujadili namna gani tusaidiane kuendesha kijiji hiki cha TULONGE hasa ukizingatia kuwa raha tunazipata woote na si DISMAS peke yake kama walivyosema Alfan na Chalii. Na kama alivyosema Alfan na Dixon,kuwa Mkuu wa Tulonge asione soo kusema iwapo kuna tatizo la kiuendeshaji. Na sisi kuchangia pesa kwa ajili ya kijiji haina maana kuwa tunataka kuki-rule kijiji kwa sababu tu pesa yetu inafanya kijiji ki-run, la hasha....hitaji letu la kutaka kukichangia kijiji ni kujenga ushirikiano katika mambo mbalimbali, na kufanya tuwe pamoja zaidi. Na isifikie wakati tukashindwa kujuliana hali eti kwa sababu hakuna pesa za kuendeshea kijiji. Kwa kuzingatia michango ya Chalii, Dixon, na Alfani niseme tu kuwa tupange mikakati itakayofanya kijiji hiki kiendelee kupaa na kuwa unique. Ni hayo tu kwa sasa.


ha haaa ha aaa,kweli hiii issue kila mtu amekuja namtazamo wake.ha haaa.
Cha the Great said:

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha Pascal unasema kilakilichozaliwa kitaonja mauti, kwa hiyo hata chupa ya beer unayokunywa itaonja mauti. Tehe tehe tehe!

Saint Pascal of Zanzibar said:

Kila kilichozaliwa kitaonja mauti.


Ha ha ha ha ha ha ha ha! Inaonesha wengi walikuwa na madukuduku. Ila Tutafika tu!
Mary wa mkumbo said:


ha haaa ha aaa,kweli hiii issue kila mtu amekuja namtazamo wake.ha haaa.
Cha the Great said:

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha Pascal unasema kilakilichozaliwa kitaonja mauti, kwa hiyo hata chupa ya beer unayokunywa itaonja mauti. Tehe tehe tehe!

Saint Pascal of Zanzibar said:

Kila kilichozaliwa kitaonja mauti.

Nimependa sana maoni ya CHA the Great, na mimi nimuunge mkono kwa hili kuwa tuweke ama tujenge utaratibu wa kuwa na mfuko utakaowezesha kijiji kujiendesha. Hii itasaidia sana kuondokana na matatizo kama hayo ambayo yamesemwa hapo juu na wachangiaji.

Asante CHA the great kwa mjadla mzuri kabisa. Na mimi nitakuwa miongoni mwa watu watakaonunua product zako za PamoJah kwa ajili ya kuchangia kijiji, nitakuchek any time. Ila hujasema ni asilimia ngapi utachangia kijiji. Natania ndugu, usijepata kigugumizi.

PamoJah We Can!

Ila nimebakisha t shirt ya fotobaraza ukumbusho


Pascal bado tu hujamaliza kuongea. Tehe tehe tehe!
Saint Pascal of Zanzibar said:

Ila nimebakisha t shirt ya fotobaraza ukumbusho

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*