Jamani naomba tuwekane wazi juu ya hii ishu,tusije tukafa kama kuku. -Kwanza ni kinga au tiba? -Ilijaribuwa na kufanikiwa kukinga/kutibu ukimwi kwa 100% ?
@ Severin... AIDS has no cure. Na hata hizo porojo za kinga/tiba zimekuwa zikitanda magazeti (e.g. British Medical Journal) kila mwaka na kuwapa watu matumaini duniani kote bila mafanikio ya kweli.
@ Hashim Rajab..... Mungu anamsaidia yule anayejisaidia mwenyewe. Inatubidi Africa tuchacharike kwenye Research & Development ajili ya kugundua tiba/kinga ya AIDS na sio tujibweteke kusubiria hadi Mungu atapoamua dawa ipatikane la sivyo Africa tutapukutika wote kwa kusubiria Mungu. Africa kuna wataalamu wengi tu wa kutosha.
Large pharmaceutical firms zote za west zinazotengeza dawa zinajali profit na sio bin-Adam au Mungu. Iwapo soko kubwa la dawa & kinga ya AIDS lingekuwepo Japan, nchi za Ulaya magharibi, north America (US & Canada) basi kasi ya utengenezaji dawa ingekuwa kubwa. Na siajabu hadi kufikia mid 1990s dawa ingekuwa tayari ilishapatikana. Tatizo soko kubwa la ugonjwa huu liko nchi masikini duniani; south Asia, sub-Sahara Africa, Caribbean & south America ambako tunategemea dawa za misaada na vifa kila siku.
UKIMWI sio ugonjwa tambua hilo, hivyo Kinga yake ni kula vizuri na kulala vizuri.
tuzungumzie VVU/UKIMWI
wataalamu wanapambana na watu wanaoishi na virusi vya ukimwi wasiambukizwe virusi vipya na kufikia katika ukimwi, na wasio na vvu wasiambukizwe.