Tulonge

 Nianze kwa Ushabiki Tuyapangia maneno

Niwatieni  ashiki         Pasizuke mapigano

Tetea hiki na hiki        Yadumu maelewano

NI LIPI CHAGUO LAKO KATI MABINTI WANNE.

 

Mnene kaviringika    Umbile la wafalume

Akenda atetemeka    Kivutio aso kinyume

Mrembo amithilika   Fadhaa kwa wanaume

NI LIPI CHAGUO LAKO KATI MABINTI WANNE

 

Mwembamba ameumbika Mkavu wa maumbile

Maringo asemezeka         Mrefu mwenye kilele

Bashasha asie shaka        asifika tangu kale

NI LIPI CHAGUO LAKO KATI MABINTI WANNE

 

Mweusi kicheka cheka   Avaacho hupendeza

Popote waweza toka      Ikawa ni miujiza

Wengine kubabaika       Masuali kuuliza

NI LIPI CHAGUO LAKO KATI MABINTI WANNE

 

Mweupe ni yake rangi   Leo unagombaniwa

Samawati hazurungi      Rangi zisizobuniwa

Safu ya nyuma hupangi Atitia msifiwa

NI LIPI CHAGUO LAKO KATI MABINTI WANNE

 

Haya wanatulonge - kwa faida yako ukichagua tugaie sababu ubora la chaguo kwa viwango vya tbs.

Nimekuja kimtindo wa shairi si lengo lazima uje kimtindo huo - yatakushinda ikiwa si fani kwako lakini kama uweza " basi tafadhali......."

Babengwa wa Upendo...HAHAHAA!!

Views: 440

Reply to This

Replies to This Discussion

Mimi napenda mnene, makalio ndiyo hobby yangu hahahahaaa
Mimi nampenda huyo mweusi teh teh teh
ha ha ha kaka Severin

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*