Tulonge

Nini kifanyike kwa kiasi cha fedha kilichopatikana kwa ajili ya watoto yatima kipindi hiki?

Hadi sasa mfuko wa watoto yatima una Tsh. 200,000/=, naona uchangiaji unasuasua sana.Nini kifanyike kwa kiasi kilichopatikana kwa ajili ya watoto yatima? Zitumike kwa watoto yatima wa kituo gani? Toa wazo lako.

Bofya hapa kuona kiasi kilichochangwa.

Bofya hapa kujiunga na kundi la Mfuko wa watoto yatima

Views: 1136

Reply to This

Replies to This Discussion

mdau mbona utaratibu huu wengine hatuufahamu? anyway may be because we are new in the tulonge network. mm nadhania kukaa nazo ni tatazo tafuta kituo chochote cha yatima halafu organize wanatulonge wote wakutune siku hiyo kukabidhi huo msaada kwa pamoja automatically utakuwa umewahamisisha kutoa michango.

Asante kwa ushauri mkuu Majata, ukitaka kujua zaidi ingia kwenye hilo kundi la mfuko wa watoto yatima kwwa kubofya link yake hapo juu.Pa1

Naungana na mdau Mjata Daffa, kipatikane kituo chenye uhitaji maalum; tujulishane wote tujipange kwenda huko kutoa msaada. Kwa namna hiyo hata ambao hawajachangia basi watapata fursa hiyo.

Tulonge... kama unaweza toa kwenye mjadala uwe wa wote na sio kwenye kundi tu. Kuna watu wengi sana wamejiunga na Tulonge mwaka jana na hivi sasa na hawajui chochote kuhusu Tulonge na mchango wa watoto yatima. Na hata kwa waliojiunga zamani siajabu baadhi yao watakumbuka kuchangia.

Me naunga mkono hoja ya Mjata Daffa siku ya kutowa zawadi hiyo tuwaombe wana tulonge wote walio karibu wavunje shuhuli zao siku hiyo wajitokeze kwa ari mpya nguvu mpya kasi ya ajabu pia siku hiyo mtu mwenye nguo za wanawawe haziwatoshi aje nazo zitawasaidia wengine mwenye viatu abebe unajuwa kuna wengine nguo zipo ndani hajui azipeleke wapi? sasa ipo sehem ya kupeleka njoo nazo siku hiyo kama una gunia la mchele chota hata kilo 5 njoo nazo zitasaidia nafikiri hiyo italeta hamasa kwa wadau kuchangia na pia itakuwa na maana kubwa kushinda na watoto yatima kuliko kukutana beach hayo ni yangu maoni.

Daffa- Nimekusoma mkuu, nitatafuta kituo cha kupeleka mchango huo halafu nitawajuza wadau ili tupeleke kwa pa1

Mama Malaika- Huu mjadala haupo kwenye kundi la watoto yatima,upo kwenye category ya JAMII.Kila mdau wa tulonge na asiye mdau anaweza uona.

Omari- Umenena la maana, si lazima tupeleke fedha zilizochangwa tu.Mdau mwenye chochote anaweza kuja nacho ili tukawape watoto hao

Mawazo mazuri toka kwa wadau hasa Mama Malaika, na Mjata. Mimi niongezee tu kwa kusema kitakachopatikana ndicho tukipeleke kwa waalengwa. We don't have to be rich to help them. Kwa kuwa njia imeshaoneshwa na waliotangulia kwa kuchangia kiasi hicho cha pesa; nafikiri ni vyema hili likawekwa wazi kwa kuupandisha mjadala huu pale front page ili iwe rahisi kwa kila mdau kuuona na kuchangia mawazo ama pesa, ama chochote ambacho mdau anaona kitafaa kwa watoto. Na ikifika siku ambayo ni lazima sasa tupange, wateuliwe wadau angalau watano hivi ili waende kujumuika na watoto. I hope wapo watu watakao kuwa teyari kwa ajili ya kwenda kupeleka kile kilichopatikana kwa wapendwa watoto. Nimalizie tu kwa kusema kuwa Mkuu wa Kijiji; ombi langu kwako ni kuuweka mjadala huu kama ulivyo pale front page ili kila mdau auone kiurahisi. Naamini wapo wengi ambao wako teyari kuchangia chochote kwa ajili ya watoto ila hiki kitu inawezekana kabisa hakijulikani masikioni ama machoni pao. lingine ni kwa wadau kwa ujumla kuwa; tuwasaidie watoto-haina maana uchangie milioni moja, bali chochote kile.

Mungu ambariki kila mmoja wetu.

Inshaallah!

Zikomo (asante) .... Cha the Great!

Cha the Great said:

Nimekuelewa, shukrani

Tulonge said:

Daffa- Nimekusoma mkuu, nitatafuta kituo cha kupeleka mchango huo halafu nitawajuza wadau ili tupeleke kwa pa1

Mama Malaika- Huu mjadala haupo kwenye kundi la watoto yatima,upo kwenye category ya JAMII.Kila mdau wa tulonge na asiye mdau anaweza uona.

Omari- Umenena la maana, si lazima tupeleke fedha zilizochangwa tu.Mdau mwenye chochote anaweza kuja nacho ili tukawape watoto hao

tatizo letu Watanzania tupo mstari wa mbele kuchangia sherehe, mfano harusi, party kama vile TULONGE FUNGA MWAKA PARTY (sijui imeishia wapi party yenyewe), lakini when it comes kuchangia mfano elimu, au hata watoto waishio mazingira magumu; most of us huwa tuna-stand aside and look! It's amazing. Huu mjadala ungekuwa unahusu mambo ya kuselebuka, kila mtu angechangia mjadala huu! lakini kwa kuwa ishu ni ya kuchangia watoto, wengine wanajifanya hawauoni. Jamani-- tusiwe wepesi tu katika kusheherekea tu kwa kulewa na kula vyuku. Tuchukue muda kidogo kutoa sadaka kwa MUNGU mfano kuchangia na kushiriki kujumuika pamoja na watoto waishio mazingira magumu kama baadhi ya wadau walivyopendekeza. Niwape pongezi wote walio changia fedha hizo zilizopatikana. Na mimi nipo njiani kuchangia.

Wito wangu kwa wadau wote ni kwamba-- tuchangie watoto. CHA anasema we do not have to be rich to help them, na mimi naungana naye.

Asanteni wote!

Duh.. Hivi huwa tunachangia vipi vile?? hebu tukumbushe zile namba zetu za MPESA na tigo pesa tutupie kidogo tunachopata kuliko kwenda kulipia nanihiii..hahahhaha

alfan acha uhuni--yaani leo umesahau namba ya kuchangia? Ingekuwa namba ya kumtafuta nanihii wa Morogoro
nahisi ungetoa dau la hata laki moja kwa yeyote atakayefanikisha kukpatia namba ya simu. Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha I hope utachangia mapea, asante sana kwa niaba ya Dismas Hiza (Mkuu wa Kijiji cha Tulonge).

PamoJah katika kusaidia jamii.
  Alfan Mlali said:

Duh.. Hivi huwa tunachangia vipi vile?? hebu tukumbushe zile namba zetu za MPESA na tigo pesa tutupie kidogo tunachopata kuliko kwenda kulipia nanihiii..hahahhaha

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*