Tulonge

Kati ya Rais Obama na Rais Sarkozy, ni nani anaweza kuvumilia uongo.?!

 

Katika mazungumzo yao binafsi yaliyonaswa na waandishi wa habari bila ya wao kujua wala kutambua, viongozi wa Ufaransa na Marekani Nicolas Sarkozy na Barack Obama walimtaja Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamini Netanyahu kuwa ni mtu mrongo na kidhabi ambaye hawezi kustahamilika.

Kituo cha habari cha jarida la Ufaransa Le Nouvel Observateur kimeandika kuwa katika mazungumzo hayo binafsi Sarkozy alimwambia Obama kwamba :"Hawezi kukutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu na kwamba ni mtu mrongo na kidhabi".

Obama alimjibu kwa kusema kwamba "naye pia analazimika kumstahamili Netanyahu kila siku". Habari hiyo imefichuliwa na kituo cha habari cha Arret sur inages.

Wakati wa mazungumzo hayo yaliyofanyika kandokando ya mkutano wa kundi la G20 nchini Ufaransa, vipokea sauti vinavyowekwa masikioni (headphones) vinavyotarjumu lugha mbalimbali vilifunguliwa mapema na kutolewa kwa wandishi habari na baadhi ya waandishi hao waliokuwa tayari waweviweka masikio walisikia mazungumzo hayo ya Sarkozy na Obama.

Mtandano wa Arret sur inages umesema kuwa katika mazungumzo hayo Barack Obama alimlaumu Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy kutokana na hatua ya Ufaransa ya kupigia kura ya ndiyo suala la Palestina kupewa uanachama kamili katika shirika la UNESCO na akasema hakutarajia kwamba Ufaransa ingechukua msimamo kama huo!.

Chanzo: Kiswahili.irib.ir
-------------------

Uchambuzi wa habari hii:

Mheshimiwa Rais Obama, inaonekana kaisha choshwa sana na uongo wa Benjamin Netanyahu waziri mkuu wa Utawala ghasibu wa Israel, lakini pia inaonekana anamiliki uwezo mkubwa wa kuvumilia uongo wa Netanyahu.

Ama Mheshimiwa Rais Sarkozy yeye pia kaisha choshwa sana na uongo wa Netanyahu na inaonekana hamiliki uwezo wa kumvumilia yeye na uongo wake. Kivipi ? !, -----kinamna hii kama ifuatavyo:

Utakapo itaamuli na kuitafakari vizuri kauli ya Rais wa Ufaransa Mr.Sarkozy anapomsifu Netanyahu kuwa ni 'mrongo na kidhabi',kisha ukalitaamuli jawabu la Mh. Obama kwa Sarkozy aliposema "Nami nalazimika kumstahamili Netanyahu kila siku", utagundua kwamba Obama hapingani na Sarkozy bali anakubaliana na kauli ya Rais huyo wa Ufaransa.

Na utagundua kuwa Rais Sarkozy sio wa kwanza kuutambua au kuugundua urongo wa Netanyahu,bali hilo Rais Obama alishaligundua kitambo kuwa Netanyahu huyu ni muongo kupita maelezo. Na ndio maana akasema:'Hata mimi namvumilia kila siku' (kwa maana kwamba: 'Hata yeye anamvumilia yeye na uongo wake kila siku' ).Wote wawili wanaafikiana kwa kauli moja kuwa mtu huyu anakera na uongo wake.Lakini wanatofautiana katika nukta hii moja kama ifuatavyo:

Tofauti iliyopo kati ya Sarkozy na Obama ni 'kuvumilia Uongo'.

 

Mr.Sarkozy yeye anasema hawezi kabisa kuvumilia uongo wa Netanyahu, lakini Mr.Obama anasema anajitahidi kuuvumilia kila siku.Yaani hata leo hii amevumilia,na kesho ataendelea kuvumilia tu,kesho kutwa wembe ni ule ule.
-----------------------------------

Na: Chalii_a.k.a_IL-YA

Views: 370

Reply to This

Replies to This Discussion

hahahahahaha.. hawana cha kumfanya wanaishia kusemea pembeni!

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*