Tulonge

Pamoja na serikali ya Marekani kuionya tovuti maarufu ya kutoboa siri
zilizoficha ya WikiLeaks kutoziweka nyaraka zake za siri hadharani kwa
kuwa maisha ya watu wengi yatakuwa hatarini, tovuti hiyo imezitoa
nyaraka hizo za siri na kuiweka hadharani sura halisi ya Marekani.

Nyaraka za siri za Marekani
zipatazo 250,000 zimeanza kuwekwa hadharani pamoja na serikali ya
Marekani kuionya tovuti ya WikiLeaks kuwa inavunja sheria na inayaweka
maisha ya watu wengi hatarini.
Tovuti ya WikiLeaks ambayo imebobea kwa kutoboa siri za ndani za
masuala mbalimbali duniani ilikabiliwa na mashambulizi ya hackers ambao
waliifanya tovuti hiyo ishindwe kupatikana online.
Hata hivyo nyaraka hizo za siri zimewekwa hadharani kama ilivyopangwa
kwa kutumia magazeti ya The Guardian la Uingereza, gazeti la New York
Times la Marekani, Der Spiegel la Ujerumani, El Pais la Hispania na
gazeti la Le Monde la Ufaransa.
Nyaraka hizo za siri huenda zikaharibu uhusiano wa Marekani na baadhi
ya viongozi wa nchi mbalimbali duniani ambao Marekani iliwapachika
majina mbalimbali ya kuwakashifu.
Miongoni mwa nyaraka hizo za siri hizo ni mazungumzo ya siri kati ya
Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia ambaye mara nyingi sana alikuwa
akiishinikiza Marekani ipigane vita na Iran ili kuziteketeza silaha
zake za nyuklia.
Taarifa hizo ziliendelea kusema kuwa Mfalme huyo wa Saudia
aliishinikiza Marekani iiwekee Iran vikwazo vikali vya kiuchumi na
kuwapiga marufuku viongozi wake kusafiri kimataifa.

Nyaraka hizo ziliendelea kusema kuwa Mfalme Abdullah aliungwa mkono na
Mfalme wa Bahrain, Hamad ibn Isa Al Khalifa na Mtawala wa Abu Dhabi,
Sheikh Mohammad bin Zayed ambao nao waliitaka Marekani iiteketeze Iran.
WikiLeaks pia ilitoa nyaraka ambazo zilisema kuwa Marekani kwa
kuwatumia maafisa wake kinyume cha sheria iliwapeleleza viongozi wa
baraza la Umoja wa Mataifa na hata kufikia kuchukua kwa siri alama za
mboni ya jicho na alama za vidole za katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
Ban Ki-moon.
Marekani pia ilifuatilia simu walizokuwa wakipiga, fax, email na tovuti walizokuwa wakizitembelea.

Miongoni mwa majina ya kashfa waliyopachikwa viongozi wa serikali
mbalimbali duniani, Marekani ilimuita Rais Mugabe wa Zimbabwe kuwa ni
"Kichaa Mzee", kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi ameitwa "Mtu wa Ajabu
Asiyeeleweka", wakati rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad amefananishwa
na Hitler.
Nyaraka nyinginezo zilielezea jinsi Marekani ilivyokuwa ikizishinikiza
baadhi ya nchi ziwachukue wafungwa wa kigaidi wa jela ya Guantanamo
Bay. Nchi ya Slovenia ililazimishwa imchukue mfungwa mmoja wa
Guantanamo Bay iwapo inataka kukutana na Rais Obama.
Nyaraka zaidi za siri zinazoonyesha jinsi Marekani ilivyokuwa ikivunja sheria za kimataifa zinaendelea kuchapishwa.

Views: 310

Reply to This

Replies to This Discussion

Jamaa wa wikileaks wanajiamini nn?

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*