Habari wapendwa!
Wakubwa shikamoni (japokuwa sipendi kusema "shikamoo"-ila kwa leo si mbaya), Wadogo zangu kama Dismas, na Angela inabidi mniamkie mimi kaka yenu. Vinginevyo nitawachukulia hatua za kimila.
Nimekuwa na wazo ambalo nimeona si vibaya kulileta kwenu, kwani bila ya nyie hakuna litakalowezekana juu ya wazo langu hili.
The thing is! Oh sorry, ngoja niongee Swahili, swala lenyewe ni kwamba; Kwa sasa tunaelekea kufunga ama kuumaliza mwaka-sasa nimeona ni jambo jema iwapo tutakutana pamoja kwa ajili ya kusheherekea na kubadilishana mawazo kwa yote kwa kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja. Ni matumaini yangu kuwa kila mmoja wetu angependa kumjua mwenzake "live" iwapo hajawahi kumuona "live". Nina amini kuwa ni jambo jema kwa watu kujamiiana, mfano mimi nilifurahi sana siku nilipojamiiana na Angela, aiseee.
Itakuwa ni wakati mwingine wa ku-restore friendship--lakini wakati tukifanya hilo, nisisitize jambo hapa. Wakati tupo pale kijiji cha jirani watu tulikuwa na umoja fulani ambao kwa namna fulani ulikuwa na manufaa makubwa. Lakini umoja ule umefifia kwa kiasi kikubwa sana. Sasa napenda kumuomba kila na mmoja wetu kujaribu kurudisha hali ile nzuri ya kupendeza iliyofanya tuwe zaidi ya marafiki.
Linapotokea jambo ambalo ni kawaida ku-share kwa misingi ya tamaduni zetu, na tufanye hivyo na tuwe tunamaanisha yale tunayoyasema.
Nisingependa kuongea mengi, kwani hii si makala bali ni mjadala. Kwa heshima na taadhima Nawasilisha kwenu wadau.
PamoJah!
Tags:
Nimekuelewa kaka,wazo nzuri sana.Ila inabidi uanze kusema wewe kabisa.
-Unadhani sherehe hiyo ifanyikaje? Aidha kwa kuchanga fedha halafu sherehe iandaliwe, au tukutane sehemu halafu kila mtu ataagiza kitu apendacho.
-Pia pendekeza kiwanja (sehemu) cha tukio,maana inaelekea wewe ni mtaalam sana wa haya mambo
-Kama tutachanga,pendekeza kiwango.
Ukishataja hayo sisi tutaanza kutoa maoni sasa.
Naunga mkono hoja! Ni jambo jema kujamiana! Natambua "umbali" wa wenzetu walio nje ya nchi, Lakini nahoja ya sis tulio ""nymbani" ila nje ya dar! Kwa upande wangu napenda na nitafurahi kuwepo kwenye tukio KAMA wakati utakao pangwa utaniruhusu kufika dar!! Mkisha kubaliana ni lini na wapi then nitajua kama nitaweza kufika.. Kila lakheri,
Pamoja sana!
Marahaba Cha!
Umeeleweka uzuri mdogo wangu Cha, ingawa umechanganya chingereza na chiswahili , nimefurahia sana hoja yako...... Zikomo
ohooo jambo jema, nami pia naunga kichwa na mikono na miguu
halafu kuwe na changamoto mbali mbali km..kukimbiza kuku, kuvutana kamba halafu na kula kukuz n.k lol
halafu kuwe na changamoto mbali mbali km..kukimbiza kuku, kuvutana kamba halafu na kula kukuz n.k lol
halafu kuwe na changamoto mbali mbali km..kukimbiza kuku, kuvutana kamba halafu na kula kukuz n.k lol
© 2021 Created by Tulonge.
Powered by