Tulonge

Habari wapendwa!

Wakubwa shikamoni (japokuwa sipendi kusema "shikamoo"-ila kwa leo si mbaya), Wadogo zangu kama Dismas, na Angela inabidi mniamkie mimi kaka yenu. Vinginevyo nitawachukulia hatua za kimila.

Nimekuwa na wazo ambalo nimeona si vibaya kulileta kwenu, kwani bila ya nyie hakuna litakalowezekana juu ya wazo langu hili.

The thing is! Oh sorry, ngoja niongee Swahili, swala lenyewe ni kwamba; Kwa sasa tunaelekea kufunga ama kuumaliza mwaka-sasa nimeona ni jambo jema iwapo tutakutana pamoja kwa ajili ya kusheherekea na kubadilishana mawazo kwa yote kwa kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja. Ni matumaini yangu kuwa kila mmoja wetu angependa kumjua mwenzake "live" iwapo hajawahi kumuona "live". Nina amini kuwa ni jambo jema kwa watu kujamiiana, mfano mimi nilifurahi sana siku nilipojamiiana na Angela, aiseee.

Itakuwa ni wakati mwingine wa ku-restore friendship--lakini wakati tukifanya hilo, nisisitize jambo hapa. Wakati tupo pale kijiji cha jirani watu tulikuwa na umoja fulani ambao kwa namna fulani ulikuwa na manufaa makubwa. Lakini umoja ule umefifia kwa kiasi kikubwa sana. Sasa napenda kumuomba kila na mmoja wetu kujaribu kurudisha hali ile nzuri ya kupendeza iliyofanya tuwe zaidi ya marafiki.

Linapotokea jambo ambalo ni kawaida ku-share kwa misingi ya tamaduni zetu, na tufanye hivyo na tuwe tunamaanisha yale tunayoyasema.

Nisingependa kuongea mengi, kwani hii si makala bali ni mjadala. Kwa heshima na taadhima Nawasilisha kwenu wadau.

 

PamoJah!

Views: 1623

Reply to This

Replies to This Discussion

Nimekuelewa kaka,wazo nzuri sana.Ila inabidi uanze kusema wewe kabisa.

-Unadhani sherehe hiyo ifanyikaje? Aidha kwa kuchanga fedha halafu sherehe iandaliwe, au tukutane sehemu halafu kila mtu ataagiza kitu apendacho.

-Pia pendekeza kiwanja (sehemu) cha tukio,maana inaelekea wewe ni mtaalam sana wa haya mambo

-Kama tutachanga,pendekeza kiwango.

Ukishataja hayo sisi tutaanza kutoa maoni sasa.

Naunga mkono hoja! Ni jambo jema kujamiana! Natambua "umbali" wa wenzetu walio nje ya nchi, Lakini nahoja ya sis tulio ""nymbani" ila nje ya dar! Kwa upande wangu napenda na nitafurahi kuwepo kwenye tukio KAMA wakati utakao pangwa utaniruhusu kufika dar!! Mkisha kubaliana ni lini na wapi then nitajua kama nitaweza kufika.. Kila lakheri,

 

Pamoja sana!

mimi nimeipenda sana hii maana ndio mawazo yangu kila siku,  naunga mkono wote, waliotangulia,
Nami naunga mkono na mguu ingawa nilisinzia ndio naamka kutoka usingizini ila naunga mkono hoja sasa panga sehem gani? je ghalama inakuwaje? au Mr Tulonge anatazamini pambano? lol kama vp kila mbuzi ale urefu wa kamba yake.
naunga mkono hoja pia, ila natoa angalizo KWA SIYE TULIO NJE YA MKOA INABIDI TUPEWE TAARIFA MAPEMA YA TUKIO HILI ILI TUJUE TUNAWAAGAJE MABOSS WETU, na napenda hii iitwe "TULONGE GET TOGETHER PART FOR CELEBRATING 1YR"
Nakuunga mkono bro KUNAMBI Jr.

Marahaba Cha!

Umeeleweka uzuri mdogo wangu Cha, ingawa umechanganya chingereza na chiswahili , nimefurahia sana hoja yako...... Zikomo 

 

 

ohooo jambo jema, nami pia naunga kichwa na mikono na miguu

 

halafu kuwe na changamoto mbali mbali km..kukimbiza kuku, kuvutana kamba halafu na kula kukuz n.k lol

 

 

Hahahahaa sasa kwenye swala la kufukuza kuku.. ngoja nianze mazoezi maana itakuwa tabu kidogo.. hahahaa.. Safi sana lucie..  Alafu sisi wa huku Arusha tuwasiliane ili tuchukue usafiri mmoja! party inaanzia huku mpaka dar.. Ebwana hahaaa.. kama naiona vile!! Fanyeni maamuzi mapema tujue tunaaga vipi ofisini.. hahahaa

Lucie said:

halafu kuwe na changamoto mbali mbali km..kukimbiza kuku, kuvutana kamba halafu na kula kukuz n.k lol

 

 

Ha haa haaa... Lucie wangi itabidi kina Malaika nao wahudhurie ili wapate kukimbiza kuku.

Lucie said:

halafu kuwe na changamoto mbali mbali km..kukimbiza kuku, kuvutana kamba halafu na kula kukuz n.k lol

 

 

Wazo zuri sana hili maana limelenga starehe,na kama ilivyo kawaida ya starehe lazima ukubali Gharama maana ndugu Starehe na ndugu Gharama ni kama mtu na kaka yake toka nitoke.Hivyo tungependa kujua tunatakiwa kufanya nini ili tufanikishe PATI na hatimae tuweze kula chai na cha-PATI.

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*