Tulonge

Habari wapendwa!

Wakubwa shikamoni (japokuwa sipendi kusema "shikamoo"-ila kwa leo si mbaya), Wadogo zangu kama Dismas, na Angela inabidi mniamkie mimi kaka yenu. Vinginevyo nitawachukulia hatua za kimila.

Nimekuwa na wazo ambalo nimeona si vibaya kulileta kwenu, kwani bila ya nyie hakuna litakalowezekana juu ya wazo langu hili.

The thing is! Oh sorry, ngoja niongee Swahili, swala lenyewe ni kwamba; Kwa sasa tunaelekea kufunga ama kuumaliza mwaka-sasa nimeona ni jambo jema iwapo tutakutana pamoja kwa ajili ya kusheherekea na kubadilishana mawazo kwa yote kwa kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja. Ni matumaini yangu kuwa kila mmoja wetu angependa kumjua mwenzake "live" iwapo hajawahi kumuona "live". Nina amini kuwa ni jambo jema kwa watu kujamiiana, mfano mimi nilifurahi sana siku nilipojamiiana na Angela, aiseee.

Itakuwa ni wakati mwingine wa ku-restore friendship--lakini wakati tukifanya hilo, nisisitize jambo hapa. Wakati tupo pale kijiji cha jirani watu tulikuwa na umoja fulani ambao kwa namna fulani ulikuwa na manufaa makubwa. Lakini umoja ule umefifia kwa kiasi kikubwa sana. Sasa napenda kumuomba kila na mmoja wetu kujaribu kurudisha hali ile nzuri ya kupendeza iliyofanya tuwe zaidi ya marafiki.

Linapotokea jambo ambalo ni kawaida ku-share kwa misingi ya tamaduni zetu, na tufanye hivyo na tuwe tunamaanisha yale tunayoyasema.

Nisingependa kuongea mengi, kwani hii si makala bali ni mjadala. Kwa heshima na taadhima Nawasilisha kwenu wadau.

PamoJah!

Views: 1768

Reply to This

Replies to This Discussion

Mkuu Cha tunaomba utoe mwongozo juu ya hii ishu.Rejea maoni ya Severin hapo juu.
hata mimi naunga mapaja yote mawili lakini sisi tulioko mwisho wa dunia tufanyeje na hali na uwezo ni mdogo. itakuaje?

pamoja na kuikumbuka pati, itabidi duwakalibishe wazee wa dini kwa ajili ya kuiombea nchi yetu maana inapokwenda sio mishahara haijapanda dola imepanda,,,,,, vyakula viko juu, mishahara hata tetesi kwamba itapanda lini, hakuna, pati tuko pamoja, lkn maandalizi mapema basi tujue jinsi ya kujipanga sisi tuliopo hapa mjini dar, na walioko mikoani, ili tushiriki nao kwa sababu hao wa mikoani ndio wanachangamoto kubwa,  naamini kwamba iko siku tutapanga kwenda kuifanyia mkoani alioko kwenye mkoa huo ndio atakaekuwa mwenyeji wetu, na kuhusu kufukuza kuku itakuwa nzuri, mwaka huu dar, tutafukuza kuku, mwakani arusha, tutafukuza ng"ombe, mwaka mwingine, mtwara tutafukuza, panya, na mwaka utakao fuata inaweza kufanyika hapa zanzibar tutafukuza kitimoto,,,,, asanteni kwa kunisikiliza,,,

Nimewapata ndugu, jamaa na marafiki! Kwa kuzingatia maoni ya Kunambi, Dixon, Lucie na wengine wote--napenda kupendekeza kuwa siku ya kufanyika sherehe hiyo iwe mwishoni mwa mwezi wa November ama mwezi wa 11. Kuhusu eneo, nafikiri ndugu yetu Bwana Chaoga atatusaidia kwa hilo, ilimradi liwe tulivu na lenye amani. Nimefurahi sana maoni ya Lucie ya kwamba kuwe na changamoto ya kufukuza kuku--nimefurahi kwa sabu Lucie si ajabu hata kufukuza sisimizi kwake ni shughuli pevu. Naomba tuendelee kujadili ili tufikie muafaka. Amani kwenu wote!
Chaoga rejea maoni ya Cha hapo juu, tunahitaji muongozo wako
Kuhusu gharama nafikiri kila mmoja ale kitu kulingana na mahitaji yake, maana isije tukalazimishana kula sahani mbili wakati wengine matumbo yetu ni ya kula sahani moja. Maana yangu ni kwamba kila mtu atajilipia, mimi siku hiyo nitakunywa soda "moja tu" halfu Dismas atanilipia, maana naona matangazo front page yapo. Tehe tehe tehe tehe tehe! PamoJah kama Bunduki na Muharifu!
Hahahhaaaa mimi nitakuja na mihogo yangu mitatu na maji kunywa toka nyumbani. Sasa hiyo hela ya kukununulia wewe Cha soda sijui itatoka wapi.Labda mwambie Alfan
mie naunga mkono hoja, cha muhimu kwa sasa ni kuwasilisha hapa mapendekezo ya hiyo shughuli halafu tutayaangalia kama yanakizi. na kuhusu kukimbiza kuku natoa muongozo kabisa AWE KUKU WA KIZUNGU, kuku wa KIENYEJI kimbizeni wenyewe
Hahahahahaaa..  kuku wa KIENYEJI NOMAAA..  Naunga mkono kuku wa kisasa !! kwani hata baada ya "chupa" kadhaa bado kunauwezekano wa kushiriki pambano..

chaoga said:
mie naunga mkono hoja, cha muhimu kwa sasa ni kuwasilisha hapa mapendekezo ya hiyo shughuli halafu tutayaangalia kama yanakizi. na kuhusu kukimbiza kuku natoa muongozo kabisa AWE KUKU WA KIZUNGU, kuku wa KIENYEJI kimbizeni wenyewe
hahahahaa.. tupo pamoja kaka bonielly.. ila unaonaje kama tukianza mwaka huu sisi tunao toka nje ya dar nyie muwe wenyeji wetu kwa malazi na shughuli nzima? ili mtakapo kuja huku kwetu na sisi tufanye kama mtakavyo tufanyia ?

Bonielly said:

pamoja na kuikumbuka pati, itabidi duwakalibishe wazee wa dini kwa ajili ya kuiombea nchi yetu maana inapokwenda sio mishahara haijapanda dola imepanda,,,,,, vyakula viko juu, mishahara hata tetesi kwamba itapanda lini, hakuna, pati tuko pamoja, lkn maandalizi mapema basi tujue jinsi ya kujipanga sisi tuliopo hapa mjini dar, na walioko mikoani, ili tushiriki nao kwa sababu hao wa mikoani ndio wanachangamoto kubwa,  naamini kwamba iko siku tutapanga kwenda kuifanyia mkoani alioko kwenye mkoa huo ndio atakaekuwa mwenyeji wetu, na kuhusu kufukuza kuku itakuwa nzuri, mwaka huu dar, tutafukuza kuku, mwakani arusha, tutafukuza ng"ombe, mwaka mwingine, mtwara tutafukuza, panya, na mwaka utakao fuata inaweza kufanyika hapa zanzibar tutafukuza kitimoto,,,,, asanteni kwa kunisikiliza,,,

Hahahahahahaaa acha uvivu Chaoga.Naona unataka kuku wa kizungu ili umkamate huku unatembea.

-Halafau Cha anataka upendekeze eneo la shughuli sababu wewe ni mutoto ya mujini waweza jua eneo zuri, ukizingatia uchumi wetu nk. Siyo upendekeze Kempiski, utaenda mwenyewe.

chaoga said:

mie naunga mkono hoja, cha muhimu kwa sasa ni kuwasilisha hapa mapendekezo ya hiyo shughuli halafu tutayaangalia kama yanakizi. na kuhusu kukimbiza kuku natoa muongozo kabisa AWE KUKU WA KIZUNGU, kuku wa KIENYEJI kimbizeni wenyewe
Hii tamu jamani, lazima nije.Namkimbiza kuku halafu nikimkamata namchinja hapo hapo.

Reply to Discussion

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*