Habari wapendwa!
Wakubwa shikamoni (japokuwa sipendi kusema "shikamoo"-ila kwa leo si mbaya), Wadogo zangu kama Dismas, na Angela inabidi mniamkie mimi kaka yenu. Vinginevyo nitawachukulia hatua za kimila.
Nimekuwa na wazo ambalo nimeona si vibaya kulileta kwenu, kwani bila ya nyie hakuna litakalowezekana juu ya wazo langu hili.
The thing is! Oh sorry, ngoja niongee Swahili, swala lenyewe ni kwamba; Kwa sasa tunaelekea kufunga ama kuumaliza mwaka-sasa nimeona ni jambo jema iwapo tutakutana pamoja kwa ajili ya kusheherekea na kubadilishana mawazo kwa yote kwa kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja. Ni matumaini yangu kuwa kila mmoja wetu angependa kumjua mwenzake "live" iwapo hajawahi kumuona "live". Nina amini kuwa ni jambo jema kwa watu kujamiiana, mfano mimi nilifurahi sana siku nilipojamiiana na Angela, aiseee.
Itakuwa ni wakati mwingine wa ku-restore friendship--lakini wakati tukifanya hilo, nisisitize jambo hapa. Wakati tupo pale kijiji cha jirani watu tulikuwa na umoja fulani ambao kwa namna fulani ulikuwa na manufaa makubwa. Lakini umoja ule umefifia kwa kiasi kikubwa sana. Sasa napenda kumuomba kila na mmoja wetu kujaribu kurudisha hali ile nzuri ya kupendeza iliyofanya tuwe zaidi ya marafiki.
Linapotokea jambo ambalo ni kawaida ku-share kwa misingi ya tamaduni zetu, na tufanye hivyo na tuwe tunamaanisha yale tunayoyasema.
Nisingependa kuongea mengi, kwani hii si makala bali ni mjadala. Kwa heshima na taadhima Nawasilisha kwenu wadau.
PamoJah!
Tags:
pamoja na kuikumbuka pati, itabidi duwakalibishe wazee wa dini kwa ajili ya kuiombea nchi yetu maana inapokwenda sio mishahara haijapanda dola imepanda,,,,,, vyakula viko juu, mishahara hata tetesi kwamba itapanda lini, hakuna, pati tuko pamoja, lkn maandalizi mapema basi tujue jinsi ya kujipanga sisi tuliopo hapa mjini dar, na walioko mikoani, ili tushiriki nao kwa sababu hao wa mikoani ndio wanachangamoto kubwa, naamini kwamba iko siku tutapanga kwenda kuifanyia mkoani alioko kwenye mkoa huo ndio atakaekuwa mwenyeji wetu, na kuhusu kufukuza kuku itakuwa nzuri, mwaka huu dar, tutafukuza kuku, mwakani arusha, tutafukuza ng"ombe, mwaka mwingine, mtwara tutafukuza, panya, na mwaka utakao fuata inaweza kufanyika hapa zanzibar tutafukuza kitimoto,,,,, asanteni kwa kunisikiliza,,,
mie naunga mkono hoja, cha muhimu kwa sasa ni kuwasilisha hapa mapendekezo ya hiyo shughuli halafu tutayaangalia kama yanakizi. na kuhusu kukimbiza kuku natoa muongozo kabisa AWE KUKU WA KIZUNGU, kuku wa KIENYEJI kimbizeni wenyewe

Hahahahahahaaa acha uvivu Chaoga.Naona unataka kuku wa kizungu ili umkamate huku unatembea.
-Halafau Cha anataka upendekeze eneo la shughuli sababu wewe ni mutoto ya mujini waweza jua eneo zuri, ukizingatia uchumi wetu nk. Siyo upendekeze Kempiski, utaenda mwenyewe.
chaoga said:
mie naunga mkono hoja, cha muhimu kwa sasa ni kuwasilisha hapa mapendekezo ya hiyo shughuli halafu tutayaangalia kama yanakizi. na kuhusu kukimbiza kuku natoa muongozo kabisa AWE KUKU WA KIZUNGU, kuku wa KIENYEJI kimbizeni wenyewe
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by