Tulonge

Habari wapendwa!

Wakubwa shikamoni (japokuwa sipendi kusema "shikamoo"-ila kwa leo si mbaya), Wadogo zangu kama Dismas, na Angela inabidi mniamkie mimi kaka yenu. Vinginevyo nitawachukulia hatua za kimila.

Nimekuwa na wazo ambalo nimeona si vibaya kulileta kwenu, kwani bila ya nyie hakuna litakalowezekana juu ya wazo langu hili.

The thing is! Oh sorry, ngoja niongee Swahili, swala lenyewe ni kwamba; Kwa sasa tunaelekea kufunga ama kuumaliza mwaka-sasa nimeona ni jambo jema iwapo tutakutana pamoja kwa ajili ya kusheherekea na kubadilishana mawazo kwa yote kwa kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja. Ni matumaini yangu kuwa kila mmoja wetu angependa kumjua mwenzake "live" iwapo hajawahi kumuona "live". Nina amini kuwa ni jambo jema kwa watu kujamiiana, mfano mimi nilifurahi sana siku nilipojamiiana na Angela, aiseee.

Itakuwa ni wakati mwingine wa ku-restore friendship--lakini wakati tukifanya hilo, nisisitize jambo hapa. Wakati tupo pale kijiji cha jirani watu tulikuwa na umoja fulani ambao kwa namna fulani ulikuwa na manufaa makubwa. Lakini umoja ule umefifia kwa kiasi kikubwa sana. Sasa napenda kumuomba kila na mmoja wetu kujaribu kurudisha hali ile nzuri ya kupendeza iliyofanya tuwe zaidi ya marafiki.

Linapotokea jambo ambalo ni kawaida ku-share kwa misingi ya tamaduni zetu, na tufanye hivyo na tuwe tunamaanisha yale tunayoyasema.

Nisingependa kuongea mengi, kwani hii si makala bali ni mjadala. Kwa heshima na taadhima Nawasilisha kwenu wadau.

 

PamoJah!

Views: 1722

Reply to This

Replies to This Discussion

Hahahahahahah Chaoga acha hizo lazima tununuwe kuku wa kijiji kama kawaida kijijini hatufugi kuku wa wee 4

tunakimbiza kuku wa kienyeji atakamkamata wake pia nilikuwa na wazo kuhusu chakula kama kawaida ya wanakijiji kukiwa na sikukuu huwa wanakusanya vyakula kila nyumba kisha wote wanakaa pamojah na kula wote

so iweje wanakijiji cc tule tofauti? wazo langu tuandae chakula na maji au soda kwa pamojah kama m2 anataka maji ya ilala atatumia mfuko wake mwenyewe hayo nimawazo yangu na kama kaida ya wana vijiji wafanyavyo kwenye sherehe,sikukuu ktk mambo yote ya furaha.

kwa sababu muda wa hiyo tarehe bado uko mbali kidogo, ngoja tuanzae kupelelza sehemu ambayo tulivu na yenye nafasi, na ambayo itakuwa ni rahisi kwa kila kufika
kaka cha mbona uko kimya tunakusubili wewe muda unasonga, haurudi,

Chaoga ndio tulikuwa tunasubiri atupe muongozo wa sehemu gani tulivu na amani itakayofaa kwa ajili ya shughuli yetu. Na ningemuomba Chaoga afanye hima ili kutupa taarifa mapema ya ni wapi tutakuwa kwa jili ya shughuli hiyo. Mengine tutahabarishana ndani ya wiki mbili hizi. Kingine ambacho ningeomba ni kwa kila atakayetaka kushiriki atoe taarifa uwepo wake. Ninaomba kila mmoja atende lile atakalohubiri, na isiwe kinyume.

Nina imani mambo yatakuwa mazuri zaidi!. nitafurahi sana kuwaona woote, hasa wale ambao sijawahi kuwaona.


Bwana Bonielly tunamsubiri Chaoga ili mambo mengine  yaendelee!. Tupo pamoja kama Kuku na Chipsi.
Bonielly said:
kaka cha mbona uko kimya tunakusubili wewe muda unasonga, haurudi,
Bwana OMary wazo lako ni zuri sana, na ninafikir haya yoote yajadiliwe ndani ya wiki mbili hizi.

Omary said:

Hahahahahahah Chaoga acha hizo lazima tununuwe kuku wa kijiji kama kawaida kijijini hatufugi kuku wa wee 4

tunakimbiza kuku wa kienyeji atakamkamata wake pia nilikuwa na wazo kuhusu chakula kama kawaida ya wanakijiji kukiwa na sikukuu huwa wanakusanya vyakula kila nyumba kisha wote wanakaa pamojah na kula wote

so iweje wanakijiji cc tule tofauti? wazo langu tuandae chakula na maji au soda kwa pamojah kama m2 anataka maji ya ilala atatumia mfuko wake mwenyewe hayo nimawazo yangu na kama kaida ya wana vijiji wafanyavyo kwenye sherehe,sikukuu ktk mambo yote ya furaha.

jamani itabidi muangalia mahali ambayo isiwe juu kihivyo maana naamini wengine watatoka nje ya dar, wasishindwe kufika, iwe sehemu ambayo ni saizi ya watanzania wote sio watanzania wachache,,,hilo ni wazo tu,,,,,

Yani boni wazolako nila ukweli.. na siku yenyewe iangaliwe ili tuweze kuwasili na kurudi mikoani tutokako na kuendelea na kazi ya ujenzi wa taifa kama kawaida.. yani siku ambayo inaudhurika..Bonielly said:

jamani itabidi muangalia mahali ambayo isiwe juu kihivyo maana naamini wengine watatoka nje ya dar, wasishindwe kufika, iwe sehemu ambayo ni saizi ya watanzania wote sio watanzania wachache,,,hilo ni wazo tu,,,,,
Nafikiri Dismas, Alfani, na Angela wapewe jukumu la kupanga siku ambayo itakuwa mwishoni mwa mwezi huu kwa ajili ya "TULONGE FUNGA MWAKA PARTY".  siku ambayo kweli itakuwa ni nzuri kwa kila aliye Mtanzania. Ama kwa wale walio nje ya Dar na wangependa kushiriki, nafikiri itakuwa ni vyema na haki kwa wao kushauri siku ambayo wanafikiri ni nzuri. Dixon, Lucie, na Silas. Dada Mama M, najua uko PamoJah nasi kimawazo, ningependa/tungependa kusikia neno muhimu toka kwako.
Kwa upande wangu.. Siku ambayo nadhani itakuwa inatufaa sote na ni ya mwishow wa mwezi huu ni j'mosi ya tarehe 26. Ambayo kwa sisi wa nje ya dar tuombe Ruhusa makazini kwetu ikiwezekana Ijumaa tuanze safari ya kuja dar ili jmosi tushiriki na j2 tujirejeshe tutokako ili j3 tuweze report kwa waajili wetu. Natumaini na natarajia kuudhuria sherehe hiyo kupata nafasi ya kukutana uso kwa uso na wanakijiji wenzangu.. Tuombe uzima! PamoJah.
Dixon amechangia vzr sana. Wadau wengine mnasema?

Hata mimi naunga mkono maoni ya Dixon. I hope wengi wataafiki hili ili kuweza kwenda sambamba na mawazo ya Dixon.

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*