Tulonge

Habari wapendwa!

Wakubwa shikamoni (japokuwa sipendi kusema "shikamoo"-ila kwa leo si mbaya), Wadogo zangu kama Dismas, na Angela inabidi mniamkie mimi kaka yenu. Vinginevyo nitawachukulia hatua za kimila.

Nimekuwa na wazo ambalo nimeona si vibaya kulileta kwenu, kwani bila ya nyie hakuna litakalowezekana juu ya wazo langu hili.

The thing is! Oh sorry, ngoja niongee Swahili, swala lenyewe ni kwamba; Kwa sasa tunaelekea kufunga ama kuumaliza mwaka-sasa nimeona ni jambo jema iwapo tutakutana pamoja kwa ajili ya kusheherekea na kubadilishana mawazo kwa yote kwa kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja. Ni matumaini yangu kuwa kila mmoja wetu angependa kumjua mwenzake "live" iwapo hajawahi kumuona "live". Nina amini kuwa ni jambo jema kwa watu kujamiiana, mfano mimi nilifurahi sana siku nilipojamiiana na Angela, aiseee.

Itakuwa ni wakati mwingine wa ku-restore friendship--lakini wakati tukifanya hilo, nisisitize jambo hapa. Wakati tupo pale kijiji cha jirani watu tulikuwa na umoja fulani ambao kwa namna fulani ulikuwa na manufaa makubwa. Lakini umoja ule umefifia kwa kiasi kikubwa sana. Sasa napenda kumuomba kila na mmoja wetu kujaribu kurudisha hali ile nzuri ya kupendeza iliyofanya tuwe zaidi ya marafiki.

Linapotokea jambo ambalo ni kawaida ku-share kwa misingi ya tamaduni zetu, na tufanye hivyo na tuwe tunamaanisha yale tunayoyasema.

Nisingependa kuongea mengi, kwani hii si makala bali ni mjadala. Kwa heshima na taadhima Nawasilisha kwenu wadau.

 

PamoJah!

Views: 1768

Reply to This

Replies to This Discussion

 Hii ni kitu safii sana ambacho kinahitaji kuungwa mkono na wanatulonge wote,nadhani bonny , angela,Dismas,chaliia.k.aJLYA  ,mnahitaji kuwa wanakamati wa shughuli hii

wazo ni nzuri sana sana nimekubaliana nalo na sasa nasubiri maelekezo ili niweze kutekeleza kile mtakachopanga kuhusu kufanikisha shughuli hii.

Hii kitu kwa nini isiitwe tulonge fungua mwaka, ambapo watu tutakuwa tukijadiliana ama kubadilishana mawazo kwa yale yalitopita kwa mwaka wa 2011 na kujadiliana nini kifanyike kwa mwaka huo unaokuja. Maana yangu ni kwamba- wale wote ambao ni wageni mfano mimi tutakuwa na nafasi nzuri ya kushiriki hasa ukizingatia tupo nje ya Dar kwa sasa. Maana yake nyingine ni kwamba badala ya kufanyika mwaka huu mwishoni ifanyike mwakani mwanzoni. Sijui mnaonaje wadau? Ni mawazo yangu tu si lazima yatekelezwe.

kwanza karibu ktk kijijini hiki cha tulonge @zainabu, 2, ikiweka picha hapo mbele itapendeza zaidi, 3, ushauri wako ni mzuri sana kwa sababu maana ya group ni kushauriana, kusaidiana, kupendana, kufundishana, anaepotea kumrudisha na kumuonyesha njia, naamini tutakapokutana kwa pamoja tutaweza kufanya makubwa sana tusiyoyategemea ya kujenga jamii na hata nchi pia, kwa sababu kila mmoja ana mawazo yake, na na hata kukijenga kijiji kikawa si kijiji tena na ukawa mji na hadi nchi, maana hatutapungua tutaongezeka na ikawa mfana wa magroup mengine na watu wakawa na shauku ya kuingia tu sio kutoka,

 

ni mtazamo wangu,,,

Nakubaliana na wewe  Bonielly kwa mtazamo  wako wa maana juu ya umoja wetu wa tulonge,tunahitaji kuwa kitu kimoja ktk raha na shida.Hata wahenga wa zamani wamesema kidole kimoja hakivunji chawa na wengine wakasema umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.wengine wakaongeza  undugu  si kufafana ila kusaidiana.Nadhani nimeeleweka na wanatulonge wote .

Haya ni maoni ya mdau mmoja ambaye anapatikana kule Dodoma, na hivi ndivyo alivyoniandikia kupitia page yangu:

At 10:57pm on November 16, 2011, Silas A. NtiyamilaSilas A. Ntiyamila said…

Jamani kwema humu, mheshimiwa Cha mimi napenda kushiriki tena sana. Mi ningependekeza tufanye Jumamosi ya tarehe 3 Desemba ili angalau watu wawe wamejaa mifukoni kusudi sisi wa mbali tupate nauli na kidogo ya kupata maji njiani. Tuko pamoja

Leo ni Tarehe 22-11-2011, ni siku kama 3 tu zilizobaki ili ifike siku iliyopendekezwa na Dickson na wengine kadhaa, lakini bado sijaona mwitikio thabiti wa tarehe hiyo. Mimi naungana na Silas, hata kama si kwa tarehe hiyo. Ila siku zisogezwe mbele kidogo, na kampeni ya  kuhamasisha wadau nitaianza kutoka sasa, ili party yetu iwe ya kipekee zaidi. Haya ni maoni yangu, kama kuna maoni tofauti basi kila mtu achangie maana wanasema "TWO HEADS ARE BETTER THAN ONE." PamoJah!

Naona mzee Silas hataki kukosa, hamna noma tumpe shavu.

Nami nampa shavu mdau Silas. Ni vizuri kufanya hiyo party kipindi watu wanapesa nauli kutosha (Mshahara) hasa ukizingatia kwa wale walio nje ya Dar. 

Bongo ingekuwa karibu natamani nami ningehudhuria.

Naunga mikono na miguu pamojah we can.

 

Naunga hoja! hapo tumesogeza wiki moja mbele. Nadhani ni wazo zuri kwani siku zimekimbia lakini muamko wa wanakijiji umekuwa mdogo sana kwa jinsi mimi nilivyoona. CHA, kampeni hazijasomeka kabisa!!

TWENDE KAZI SASA!!

Amani kwa wote!

Ni kweli kabisa mwamko wa wanatulonge ni mdogo ktk kuitikia mwito huu,lkn siwezi kuwalaumu kwa sababu ya mihangaiko ya kutafuta ridhiki ya kila siku  imewabana sana na kingine mwezi wa12 ni mwezi ambao wengi wanakuwa ktk harakati nyingi za sikukuuu za xmass na mwaka mpya.

Suala la wengine kukaa nje ya dar ni la muhimu sana kuangaliwa jinsi ya kuwasaidia na kuwapa maelekezo jinsi ya shunghuli itakavyokuwa,kipi kinatakiwa kufanikisha jambo hilo,muda wa shughuli yenyewe kuanza,iliwale wa maeneo ya moro,pwani na znz waweze kuja siku hiyohiyo ya tukio

jamani mtaniwia radh kidogo kwa mtazamo wangu, mimi kwa mtazamo ni kwamba hakuna kazi ndogo, achilia mbali sikukuu inayofuata ya mwezi wa kumi na mbili hilo linajulikana na tumelizoea, ninachotaka kusema mpaka sasa naona zoezi linasuasua sana hatujachagua kiwanja, bado, hatujajua tuhifadh kiwangogani ambacho mtu atakiweza, leo mnatoa mitazamo tu wiki moja mala wiki mbili, kifupi ni hivi, tujipange, tujiandae, tuhifadhi mpunga ili hiyo siku ikifika hata kama unatoka mbali au karibu uwe na uhakina na kujiamini kwa lolote lile, ninachojaribu kusema nashauri tu jamani, kama mtaona nakosea mtaniambia kwa utaratibu sio kwa ukali,

 

ni hivi tufanyeni mwisho jumaamosi au jumaapili ya mwanzo  wa mwaka wa 2012,,,,,, nasema hivyo kwa sababu hizi hapa, wikihii, bwana @cha, amtaarifu bwana @dis, wachague kiwanja, wiki inayofuata dada @angela na wakuu hawa wawili yani cha na dis, watasmini ni kiasigani kitakacho tosheleza kulipia hapo kiwanjani na matumizi ya mtu binafsi, ili kila mmoja achekeche kichwa chake apate jibu, halafu hizo siku zinazobaki kama mtu anacheza kamchezo kake, atakaficha kwa sababu anajua ni lini atahitajika kufika hapo, au ni lini tunakabidhi mpunga kwa muweka hazian,

kwahiyo mimi kwa mtazamo wangu tuacheni keshokesho zitakua nyingi mwisho wa siku,,,,,,,,,''''. nashauli tu kama mnaona nimekosea, mtaangalia, kwa sababu tunahitaji tupate mda mwingi wa kushauriana mambo mengi kwani haya maisha ya tanzania siyaelewi kabisa tunazidi kuumia mwishoe hata somalia itakua juu yetu watu watakufa wanajiona,

Reply to Discussion

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*