Tulonge

Habari wapendwa!

Wakubwa shikamoni (japokuwa sipendi kusema "shikamoo"-ila kwa leo si mbaya), Wadogo zangu kama Dismas, na Angela inabidi mniamkie mimi kaka yenu. Vinginevyo nitawachukulia hatua za kimila.

Nimekuwa na wazo ambalo nimeona si vibaya kulileta kwenu, kwani bila ya nyie hakuna litakalowezekana juu ya wazo langu hili.

The thing is! Oh sorry, ngoja niongee Swahili, swala lenyewe ni kwamba; Kwa sasa tunaelekea kufunga ama kuumaliza mwaka-sasa nimeona ni jambo jema iwapo tutakutana pamoja kwa ajili ya kusheherekea na kubadilishana mawazo kwa yote kwa kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja. Ni matumaini yangu kuwa kila mmoja wetu angependa kumjua mwenzake "live" iwapo hajawahi kumuona "live". Nina amini kuwa ni jambo jema kwa watu kujamiiana, mfano mimi nilifurahi sana siku nilipojamiiana na Angela, aiseee.

Itakuwa ni wakati mwingine wa ku-restore friendship--lakini wakati tukifanya hilo, nisisitize jambo hapa. Wakati tupo pale kijiji cha jirani watu tulikuwa na umoja fulani ambao kwa namna fulani ulikuwa na manufaa makubwa. Lakini umoja ule umefifia kwa kiasi kikubwa sana. Sasa napenda kumuomba kila na mmoja wetu kujaribu kurudisha hali ile nzuri ya kupendeza iliyofanya tuwe zaidi ya marafiki.

Linapotokea jambo ambalo ni kawaida ku-share kwa misingi ya tamaduni zetu, na tufanye hivyo na tuwe tunamaanisha yale tunayoyasema.

Nisingependa kuongea mengi, kwani hii si makala bali ni mjadala. Kwa heshima na taadhima Nawasilisha kwenu wadau.

 

PamoJah!

Views: 1768

Reply to This

Replies to This Discussion

Hakika  mr bonnielly umenena sahihi kabisa,tunachohitaji hapa ni muda wa kujiandaa na shughuli hiyo na si vinginevyo.kwani kuna watu wanatoka mbali na hapa na lzm tuwape muda na wao wajiandae.Huu muda wa wiki moja ni mdogo sana ,na hata hivyo hatujui watu wajiandae kwa  kiasi ngani?,nawaomba sana waratibu wa jambo hili kukaa na kuangalia maoni ya wanatulonge yale yanayofaa yafanyiwe kazi,tupo ktk kujenga jamii yetu ya wanatulonge na si kubomoa umoja huu,

Hahahahaha mama bwanaMama Malaika said:

Ha haa haaa... Lucie wangi itabidi kina Malaika nao wahudhurie ili wapate kukimbiza kuku.

Lucie said:

halafu kuwe na changamoto mbali mbali km..kukimbiza kuku, kuvutana kamba halafu na kula kukuz n.k lol

 

 

Hivi hiyo pati badooooooooo? au mnaahirisha hadi december?


Asante kwa maoni.
jemadari mimi said:

Hakika  mr bonnielly umenena sahihi kabisa,tunachohitaji hapa ni muda wa kujiandaa na shughuli hiyo na si vinginevyo.kwani kuna watu wanatoka mbali na hapa na lzm tuwape muda na wao wajiandae.Huu muda wa wiki moja ni mdogo sana ,na hata hivyo hatujui watu wajiandae kwa  kiasi ngani?,nawaomba sana waratibu wa jambo hili kukaa na kuangalia maoni ya wanatulonge yale yanayofaa yafanyiwe kazi,tupo ktk kujenga jamii yetu ya wanatulonge na si kubomoa umoja huu,

Asante kwa mawazo. Binafsi niseme nakuunga mkono Bwana Boniely.

Bonielly said:

jamani mtaniwia radh kidogo kwa mtazamo wangu, mimi kwa mtazamo ni kwamba hakuna kazi ndogo, achilia mbali sikukuu inayofuata ya mwezi wa kumi na mbili hilo linajulikana na tumelizoea, ninachotaka kusema mpaka sasa naona zoezi linasuasua sana hatujachagua kiwanja, bado, hatujajua tuhifadh kiwangogani ambacho mtu atakiweza, leo mnatoa mitazamo tu wiki moja mala wiki mbili, kifupi ni hivi, tujipange, tujiandae, tuhifadhi mpunga ili hiyo siku ikifika hata kama unatoka mbali au karibu uwe na uhakina na kujiamini kwa lolote lile, ninachojaribu kusema nashauri tu jamani, kama mtaona nakosea mtaniambia kwa utaratibu sio kwa ukali,

 

ni hivi tufanyeni mwisho jumaamosi au jumaapili ya mwanzo  wa mwaka wa 2012,,,,,, nasema hivyo kwa sababu hizi hapa, wikihii, bwana @cha, amtaarifu bwana @dis, wachague kiwanja, wiki inayofuata dada @angela na wakuu hawa wawili yani cha na dis, watasmini ni kiasigani kitakacho tosheleza kulipia hapo kiwanjani na matumizi ya mtu binafsi, ili kila mmoja achekeche kichwa chake apate jibu, halafu hizo siku zinazobaki kama mtu anacheza kamchezo kake, atakaficha kwa sababu anajua ni lini atahitajika kufika hapo, au ni lini tunakabidhi mpunga kwa muweka hazian,

kwahiyo mimi kwa mtazamo wangu tuacheni keshokesho zitakua nyingi mwisho wa siku,,,,,,,,,''''. nashauli tu kama mnaona nimekosea, mtaangalia, kwa sababu tunahitaji tupate mda mwingi wa kushauriana mambo mengi kwani haya maisha ya tanzania siyaelewi kabisa tunazidi kuumia mwishoe hata somalia itakua juu yetu watu watakufa wanajiona,

Lucie nafikiri tupeane muda, kama wadau walivyopendekeza.
Mambo mazuri hayahitaji haraka. Bonielly ametoa maoni mazuri sana. Naomba binafsi tumuunge mkono kwa hilo.
Lucie said:

Hivi hiyo pati badooooooooo? au mnaahirisha hadi december?

Bonielly Asante kwa maoni mazuri ambayo naamini kila mmoja wetu ameyaafiki kutokana na ukweli kwamba tunahitaji muda zaidi wa kufanya maandalizi. Asante sana kwa maoni.

Ninaisubiri kwa hamu siku hiyo

JAMANI TUPO PAMOJA WANDUGU MIMI NASUBILI TAREHE KAMILI TUU, CHA THE GREAT MARAHABA MDOGO WANGU

tutaisha kuungana mikono tu,,,,haya twendeni,,,,,

Reply to Discussion

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*