Tulonge

Tulonge yakabidhi zawadi ya viatu kwa watoto wa kituo cha watoto yatima Kigamboni (KCC)

Ile zawadi ya viatu kwa kwa kituo cha watoto yatima Kigamboni (KCC) imekabidhiwa jana (23/01/2012). Zawadi hii imepatikana kutokana na michango ya wadau wa tulonge kwa watoto yatima ambayo imekua ikitolewa tangu lilipoanzishwa kundi la kuchangia watoto yatima hapa tulonge. Bofya hapa kuona wadau waliochangia.

Uamuzi huu wa kununua viatu kwa watoto yatima wa Kigamboni umechukuliwa baada kujadiliwa kwenye mjadala huu (Bofya kuona mjadala).

Wadau waliowakilisha Tulonge ni Tulonge (Dismas) na Jeath. Zawadi hii ilikabidhiwa kwa uongozi wa KCC na baadae kugawiwa kwa watoto. Jumla ya pea 55 za viatu vya watoto ilikabidhiwa kwa viongozi hao.

Shukrani za dhati zilitolewa kwa wadau wote wa tulonge toka kwa Uongozi wa KCC.

Tulonge akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili na kufanya mazungumzo mafupi na uongozi wa KCC. Kushoto ni Katibu wa KCC Mr. George

Viatu vilianza kufunguliwa.

Tukiendelea kufungua viatu

Mtoto akivalishwwa kiatu

Tulonge akimvalisha mtoto kiatu

Mgao ukiendelea

Tulonge na baadhi ya watoto baada ya kutinga viatu vipya.Unawaona wengine wameshika ndara zao mikononi baada ya kupata mali mupya.

Aliyeshika bomba ndiye mdau wa tulonge (Jeath) ambaye nilienda naye kukabidhi zawadi hiyo. Hao weupe ni wageni toka nje ambao walitembelea kituo.

Views: 1362

Attachments:

Reply to This

Replies to This Discussion

Waoooh,safi sana wadau watulonge kwa kuonyesha moyo wa upendo kwa wadogo na ndugu zetu.

Kweli kizuri ule na wenzio.Naamini kipindi kingine tutajipanga na kufanya vizuri zaidi ya hapo.BIG UP TULONGE PIPOZZ.PamoJa we can!!

SAFI SANA HII....NIMEPENDA SANA NA KUFARIJIKA SANA TU!

HONGERA SANA WADAU WOTE KWA MOYO WENU KWA HAWA WATOTO. PIA HONGERA SANA MKUU TULONGE KWA KUANZISHA SWALA ZURI KAMA HILI LA KUWAJALI WATOTO HAWA WASIO NA WAZAZI.

safii sanaa,,kutoa ni moyo si utajiri

Hongera Sana Wanatulonge wote mliofanikisha zoezi hili kwa njia moja au nyingine. Mungu Awabariki.

Hingera sana kwa kuwakilisha tulonge na hongera kwa wale wote mliotoa michango, Mungu awazidishie.

nimeipenda hii sasa hebu tukumbushe zile namba za akaunti ili tuanze tena kupunguza chupa za konyagi...

hongera sana Dismas, hakika umebarikiwa

YEEEEEEEEES  hongera saana kawa kutumia muda wako n kutuwakilisha..... Hii ilikua ni idea nzuri...tena kama Mary alivyosema....tunabidi tuendelee kujipanga ili next time tufanye poa zaidi ya hapa.  I feel so happy to see children happy!

   chaoga acha vituko...hahahahaha...acc. imefungwa kwa muda!!!

Hongera sana kaka Dis,kusema ukweli nimependa sana ziara hiyo katika kituo hicho maana ni ziara iliyoshiba.naweza kusema ingawa niko mbali lakini umeniwakilisha kaka maana ziara imekwenda kwa anuani ya Tulonge.Nitakuwa mchoyo wa fadhila ikiwa nitashindwa kusema many senksi kaka.

Amen!


 
Dixon Kaishozi said:

Hongera Sana Wanatulonge wote mliofanikisha zoezi hili kwa njia moja au nyingine. Mungu Awabariki.

Peace & Blessings to you Dismas!!! Imenitia furaha moyoni.

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*