Tulonge

Tulonge yakabidhi zawadi ya viatu kwa watoto wa kituo cha watoto yatima Kigamboni (KCC)

Ile zawadi ya viatu kwa kwa kituo cha watoto yatima Kigamboni (KCC) imekabidhiwa jana (23/01/2012). Zawadi hii imepatikana kutokana na michango ya wadau wa tulonge kwa watoto yatima ambayo imekua ikitolewa tangu lilipoanzishwa kundi la kuchangia watoto yatima hapa tulonge. Bofya hapa kuona wadau waliochangia.

Uamuzi huu wa kununua viatu kwa watoto yatima wa Kigamboni umechukuliwa baada kujadiliwa kwenye mjadala huu (Bofya kuona mjadala).

Wadau waliowakilisha Tulonge ni Tulonge (Dismas) na Jeath. Zawadi hii ilikabidhiwa kwa uongozi wa KCC na baadae kugawiwa kwa watoto. Jumla ya pea 55 za viatu vya watoto ilikabidhiwa kwa viongozi hao.

Shukrani za dhati zilitolewa kwa wadau wote wa tulonge toka kwa Uongozi wa KCC.

Tulonge akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili na kufanya mazungumzo mafupi na uongozi wa KCC. Kushoto ni Katibu wa KCC Mr. George

Viatu vilianza kufunguliwa.

Tukiendelea kufungua viatu

Mtoto akivalishwwa kiatu

Tulonge akimvalisha mtoto kiatu

Mgao ukiendelea

Tulonge na baadhi ya watoto baada ya kutinga viatu vipya.Unawaona wengine wameshika ndara zao mikononi baada ya kupata mali mupya.

Aliyeshika bomba ndiye mdau wa tulonge (Jeath) ambaye nilienda naye kukabidhi zawadi hiyo. Hao weupe ni wageni toka nje ambao walitembelea kituo.

Views: 1310

Attachments:

Reply to This

Replies to This Discussion

Safi sana mkuu kwa kufikisha msaada japo ni mdogo kwa wahusika. Najua kuna ambao walikuwa na mashaka kwamba michango itafika kwa wahusika. Hii imewathibitishia kuwa tuko seriaz na tukiamua kuungana pamoja na kwa moyo mmoja tunaweza kuwasaidia watoto wengi zaidi wenye kuhitaji msaada wetu. Pamojah sana wadau na tujipange kwa kupiga hatua nyingine kubwa zaidi ya hii. God Bless Us, God Bless Tulonge!

Dismas kwa kweli umetuwakilisha. Mungu akubaliki zaidi ya hapo.

Tupo pamoja wadau,napenda kuwashukuru na nyie katika kuonesha ushirikiano juu ya hili suala.

Hapo sawa, maana nilifikiri utakuwa umezitia kwenye Account yako binafsi hizo pesa.

hongera sana bwana dismas na wadau wote wa tulonge, next time mtushirikishe na sisi wa mikoani tunaweza kujikunakuna na kuzidisha furaha ya watoto hawa.

Big up mkuu.Pamoko

Safiiiiiiiiiiiii sana hii

huo ni mfano wa kuigwa jamani, hongeleni na mungu awazidishie.

nilikuwa sijaona kitu hii kka,dah,imetulia sana kaka tulonge.Hongera mno.

Hongera Dis!

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*