Tulonge

Zile za kusimuliwa, Vp bado kuna zingine hujaacha mpaka leo na zinakuletea matatizo yoyote? Kama una mtoto je ameadapt tabia zako za utoto?

Views: 1251

Reply to This

Replies to This Discussion

Mim nilikua naitwa kichwa cha mviringo na alieni2nga nae wakawa wanamwita hvyo hvyo.

Nilikua nikikatazwa kusema ki2, ujue ntakisema2 ila ctakisema direct nilikua nafikisha ujumbe kwa kuimba, tena indirect.

Niilikua m2ndu, tena u2ndu wa watoto wakiume, mkorofi na ngumi kwa sana. Nilikua nachokoza sehem afu natoka nduki mpaka hm wakinikamata napigana.

Czan kama kuna ki2 nimekua nacho. Ila mama akianzaga kunihadithia nahis mwanangu atalelewa na wafanyakaz wa3 kama akirith tabia zangu za utoto

Mimi kwa kweli nilikuwa mpole lakini mtundu wa kupindukia huwezi kusikia nimepigana lakini vituko na kupenda watoto wakike ndio zangu...tehetehetehetheteheteh.nahisi watoto wangu wote wamerithi maana wasimuone msichana mzuri tu wanaanza kujichekeshachekesha ila mmoja ni mgomvi kushinda maelezo....

wenye watoto wa kike wake mkao wa kulinda maana hawa jamaa ni noma...tehtehetehetehete :)

Alfan..... kumbe Dismas anasema ukweli tabia yako kupenda vimwana, nilifikiri anakusingizia. Na hata ile issue ya Mbagala aliyoisema sasa naanza kuamini kuwa ni ya kweli.



Alfan Mlali said:

Mimi kwa kweli nilikuwa mpole lakini mtundu wa kupindukia huwezi kusikia nimepigana lakini vituko na kupenda watoto wakike ndio zangu...tehetehetehetheteheteh.nahisi watoto wangu wote wamerithi maana wasimuone msichana mzuri tu wanaanza kujichekeshachekesha ila mmoja ni mgomvi kushinda maelezo....

wenye watoto wa kike wake mkao wa kulinda maana hawa jamaa ni noma...tehtehetehetehete :)

Hahaha Alfan watoto wako ni balaa. Itabid wazaz wenye mabint mbona wafuge mbwa!
Mim timbwil langu lilianzia kwenye mimba wakajua kidume ndo kinazaliwa kumbe kadada loh! Story nazopata kuhusu mim mwanangu akirith lazima nimpatie wafanyakaz wa3. Peke yangu ntamgawa.

Mimi nilikua sipendi kabisa wasichana, hata kukaa nao tu. Ila kwa sasa nimebadilika kidogo ndiyo maana nikamtandika mimba mmoja hahhhahahaaaaa.

Halafu nilikua nanyonya kidole kikubwa, sijui kilikua na utamu gani? ila niliacha zamani, siku hz sinyonyi teh teh teh

Hhhaahahahhahahaaaa mama M mimi nilikwambia, huyo Alfan ni nomaa kwa mabinti. Halafu huwa wanamfuata wenyeweeee, sijui ana kamzizi?

Hahahahahaaaa! mimi bwana nilikuwa mpole sana alafu nilikuwa ninaonewa sana, kila aliyejisikia kunidunda alinidunda nami nalia nakaa kimya.

wakati huo tulikuwa tunachezaga mchezo wa mama na baba, wa kujenga kijumba mimi nilikuwaga ndio mtoto nilikuwa natumwaga kwenda kuiba mchele maharage, na nyanya vitunguu magengeni nilikuwa mtundu kinoma mbishi, nakumbuka siku moja nilienda kuiba mchele kwenye duka moja la mchaga nilipewa kibano ndio ulikuwa mwanzo na mwisho wa kuiba maana nilikula kibano mala mbili kule dukani halafu ikavuja home nilikula mikanda, mpaka nikapata homa,

ila envi ya utoto nakumbuka vingi sana nilikuwa mtundu sana yani mpaka nilitaka kufa mala mbili ya kwanza tulitoroka shule tulienda kuvua samaki kwenye mto unaitwa mto mbiki, ndoana yangu ilikwama chini ya maji nilifikiri kina ni kifupi nilitaka kwenda kuitoa wewe,,,, mungu pekeake ndio kaninusuru wenzangu wote walitimua mbio na kwenda kutoa taarifa shuleni walikuja walimu na wanafunzi, mimi nilitoka kitambo wawimbi yalinitupa nje nilivyotoka nilitimua home,,, hiyo siwezi kusaha,

ingine nakumbuka nilikuwa nawinda ndege nilitaka kufa na nyuki hiyo nayo ni mungu pekee maana nyuki walinivaa mwili mzima we acha tulikuwa na mdogo wangu kitambo, hizo zinanifanya nisisahau utoto,

Mie nilikuwa mpole, mwenye huruma na mkimya sikupenda kuongea na nilipenda kukaa ndani muda wote na nilicheza na ndugu zangu au binamu ambao walikuja nyumbani kwetu. Tabia hiyo nilikuwa nayo hadi nakua kwani nimeanza kuongea kiasi na kuwa na marafiki kipindi namalizia Secondary School.

Pia kipingi cha utoto nilikuwa sipendi kabisa kabisa kukanyaga maji iwe ndani au nje au kupita kwenye mvua na matope. Mama yangu na walezi wangu (marehemu bibi na babu) walikuwa wananisimulia kuwa tokea naanza kutembea nilikuwa nalia sana hadi nabebwa nikiona maji chini. Tabia hiyo kutopenda/kutotaka kukanyaga maji chini imeendelea hadi ukubwani. Mume wangu anapokuwa jikoni anapika akishamaliza kupika na shughuli zote za usafi wa jiko anahakikisha kaacha kitchen floor kavu maana anajua mkewe hapendi wet floor. Na hata tukiwa wote wawili tunapika kwa pamoja anakuwa makini sana kutomwaga maji chini ovyo ovyo....

Ila watoto wangu watundu balaa ingawa wa kike anapunguza utundu. Pia wana maswali na wadadisi utafikiri wakubwa kitu ambacho kimenifanya nami niwe naongea sasa kwani wakikuuliza swali ni kwamba uwape jibu sahihi lililokamilika la sivyo watakushona kwani hawasahau kitu. Usiombe kukutana nao kwani hawana mgeni au mzee. Ha haa haaa...... 

Ha haa haa haa haa haa haa haaa.......................... DISMAS sasa nimekuamini ulivyoniambia kuwa ALFAN alitolewa mita kule Mbagala baada ya kufumaniwa usiku wa manane. Ha haa haa haa

Tulonge said:

Hhhaahahahhahahaaaa mama M mimi nilikwambia, huyo Alfan ni nomaa kwa mabinti. Halafu huwa wanamfuata wenyeweeee, sijui ana kamzizi?

Reply to Discussion

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*