Tags:
Mimi nilikua sipendi kabisa wasichana, hata kukaa nao tu. Ila kwa sasa nimebadilika kidogo ndiyo maana nikamtandika mimba mmoja hahhhahahaaaaa.
Halafu nilikua nanyonya kidole kikubwa, sijui kilikua na utamu gani? ila niliacha zamani, siku hz sinyonyi teh teh teh
tehe tehe@ tulonge nilisoma na kijana mmoja hadi kidato cha 4 ananyonya kidole halafu alikuwa anakimbiza mbaya, cha kushangaza yeye alikuwa mwalimu akiingia darasani ndiyo ananyonya dole lake mpaka anajisahau akisemeshwa hasikii, msichana akienda kwenye dawati lake anahama yaani muoga wa wasichana.
Tulonge said:
Mimi nilikua sipendi kabisa wasichana, hata kukaa nao tu. Ila kwa sasa nimebadilika kidogo ndiyo maana nikamtandika mimba mmoja hahhhahahaaaaa.
Halafu nilikua nanyonya kidole kikubwa, sijui kilikua na utamu gani? ila niliacha zamani, siku hz sinyonyi teh teh teh
hahahaaa!! watu mmepita mengi sana, mimi nilikuwa muongeaji sana baba yangu alikuwa akiniita mabureka, pia nilikuwa siogopi kupigana japo nilikuwa napigwa, kitu ambacho sitakisahau nikiwa darasa la 4 nilinusurika kubebwa na mafuriko baada ya kutoroka shuleni na kwenda kuongelea mto mmoja unaitwa mto malala huko meru, uliopo barabara ya moshi, arusha, mama mmoja alikuwa akipita juu darajani aliniona akapiga kelele nikaokolewa, pia nilikuwa sipendi kutumwa nikitumwa lazima nisababishe mkasa, kitu ambacho kilifanya nikanuniana na mwalimu nikiwa darasa la tano akiingia darasani mimi natoka tunapishana mlangoni hadi kipindi chake kiishe ndiyo niingie, kisa alinituma maji nikayatemea mate wanafunzi wenzangu wakanisemea akaniingiza kichwa kabatini makalio yakabaki nje akanichapa viboko 72, nikamwambia sikupendi.
hahahaa @ alfani hao majamaa zako kama wanaendana na wangu, kwani akiona watoto wa kike anaanza kuwalilia, wa kiume wala hana habari nao.
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by