Tulonge

Una kipi cha kusema juu ya serikali ya TZ kuhusu milipuko ya mabomu kwa mara ya pili?

Siku chache zimepita toka milipuko ya mabomu kutokea katika kambi ya jeshi Gongo la Mboto.Hii ni mara ya pili kwa tukio kama hili kutokea baada ya lile la mwaka 2009 huko Mbagala.
Mimi nilidhani lile tukio la Mbagala lingekuwa ni fundisho tosha na kuifanya serikali yetu kuwa makini sana na uhifadhi wa mabomu ili yasilipuke tena. Hata kama ilikuwa ni lazima yalipuke,tahadhari zingechukuliwa ili jamii isiathirike.

Unalipi juu ya hili.

Views: 561

Reply to This

Replies to This Discussion

Kwa mtazamo wangu...ile ni ajali kama ajali nyingine...najua kuna wenzetu wametangulia mbele ya haki...ila yote ni mipango ya mwenyenzi mungu. Inatubidi tuwe a mawazo  chanya!......

Kusema kweli kuna upuuzi umefanyika...ajali hii ingekuwa imetokea nchi zenye ustaarabu yaani wahusika wangejiuzulu mara moja...bongo watu wameanza uswahili! Watu wamepoteza maisha wengine wamepoteza mali zao na wengine wamebaki vilema wengine wamebaki wajane wengine wamebaki yatima.....yaani mtari utakuwa mrefu nikiendelea kutaja.

Yaani ukifikiria na kujiuliza unaweza kuweka gas tube mchagoni  unapolala?

Vifaa vya vita/silaha huwezi ukaweka karibu na watu wanapoishi. Huo ni upuuzi mtupu!

Kwa ajili ya mtu na akili yake fupi angalia watu walivyopata shida!

Na walaani sana watu wenye tabia hizi1

Ku sema ukweli uzembe wa watanzania wachache hasa walioshiba ndo unachingia kwa mambo kama hayo, kila kitu kinachukuliwa poa ni siasa hata pasipohitajika siasa labda kwa sababu hatuwezi kufanya kama wa misri na wa libya ila inauma sana Diana kuona kitendo cha hatari kama hicho kinajirudia.

Kinga bora kuliko tiba -

msimamo uwe huo lakini kungojea janga litufike hasara ndio hio na tunajiona kwa kiasi gani maisha ya watanzania yalivyo hatarini.....

Reply to Discussion

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*