Tulonge

Una lipi la kuchangia kuhusu kilichomtokea Raisi Kikwete Jangwani??

Nadhani tulipata habari kuhusu kuanguka kwa Raisi Kikwete wakati alipokuwa akiwahutubia wanachama wa CCM katika uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho kikongwe Tanzania. Mengi yamezungumzwa juu ya hili tukio. Baadhi walilichukulia kama suala la kawaida,wapo walio lihusisha imani za kishirikina pamoja na mengine mengi yaliyozungumzwa.
Wewe unalipi la kusema juu ya hili?

Views: 1159

Reply to This

Replies to This Discussion

Pamoja na maelezo yako mazuri kaka, mimi bado nataka kujua kama tatizo hilo linamtokea mtu specific mara kwa mara haina hatari yoyote kwa maisha yake!? Kwa rais Kikwete ile haikuwa mara yake ya kwanza kuanguka, ndani ya miaka mitano ameshaanguka mara nne.

ahmad kombo said:
Kaka ile inaitwa Vasovagal Syncope au Vasovagal Response.
Syncope husababishwa na low blood pressure inayosababisha damu kuwa chache kwenye ubongo.
hii husababishwa na mtu KUSIMAMA KWA MUDA MREFU, EMOTIONAL STRESS( sehemu ya joto na watu wengi)
kulala kitandani kwa muda mrefu,arousal or stimulation ie SEX,km vile wanawake wanavyozimia akishapiga bao nafikiri umeshwahi kusikia hii.
Sababu nyingine ni Kucheka sana,kusimama kwa ghafla unapokuwa umekaa chini au kulala,kumeza kitu kwa haraka, NJAA, kichefuchefu na kutapika, wakati wa kukojoa(nafikiri umeshwahi kusikia mtu ameanguka chooni,amezimia wakati anakojoa), kuoga maji ya baridi sana less tha 10 Degree Celcius, kuona damu nyingi au mtu kushuhudia ajali na kuona watu wamekatikakatika, ukiwa kileleni sn juu ya mlima nk.
INAKUWAJE??? Km mtu amepatwa na moja au zaidi ya sbb zilizotajwa hapo juu,ubongo unajibu kupitia NUCLEUS TRACTUS SOLITARIUS ambayo yenyewe inasababisha parasympathetic activity ya Tenth Cranial Nerve (VAGUS NERVE mshipa wa fahamu namba kumi kutoka kwenye ubongo) na ndo maana ikaitwa Vaso-vagal syncope,yaani VASO--ni Blood vessel,na Vagal--ni vagus nerve.Mshipa huu wa fahamu unapeleka na kurudisha fahamu toka maeneo ya shingo,kifua na kiwiliwili yaani kooni,moyo,mapafu, mrija mkubwa wa damu wa kiwiliwili (Abdominal Aorta) ,tumboni , nk.Kwa hiyo hii Solitary Nuclear ya ubongo inapokuwa activated yenyewe inatuma ujumbe kwa mrija mkubwa wa damu (Aorta) kupitia hii VAGUS NERVE,na kuuambia kuwa utanuke na kufanya damu nyingi kwenda maeneo ya kuanzia kifuani mpaka miguuni na kusababisha damu chache kwenda ubongoni hivyo kumfanya mtu azimie kwa kukosa damu ya kutosha kwenye ubongo na hivyo huanguka.
Hii haihitaji dawa mtu akinguka,jaribu kumlaza chali kwa dkk kadhaa atarudi km kawaida au kama inachukua muda basi jaribu kunyanyua miguu yake kwa juu na utengeneze nyuzi 90 kati ya kiwiliwili na miguu(kama vile unamvalisha mtoto aliyelala kitandani nguo/nepi au kwa wale wanaojua,jinsi ya kumvua mschana Jeans akiwa amelala kitandani lazima anyanyue miguu kwa juu kidogo) Hii husaidia damu kurudi kichwani kwa urahisi na hapo mgonjwa atakuwa amepata nafuu.
Kwa hiyo ile iliyompata mheshimiwa mimi naamini ni hii VASOVAGAL SYNCOPE ambayo ni kitu cha kawaida sana kwa watu wanaofanya kazi sana kwa sababu ya uchovu au kusimama mbele ya watu wengi au NJAA.
Kaka nashukuru sana kwa kunielewesha na kunifumbua macho, sasa ninaona. Tunafurahi sana kuwa na watu muhimu kama wewe hapa kijijini kwetu.
ahmad kombo said:
Nashukuru kaka.Syncope inasababishwa na damu kuwa chache ubongoni,kwa hiyo km inatokea mtu amepatwa na tatizo hilo lkn likaisha ndani ya "Reperfusion time window" basi mtu ata-recover completely hata km itatokea mara tatu kwa mwezi si tatizo.Kinachoangaliwa ni kwamba ubongo haujaathirika.
Reperfusion time window ni muda ambao chembechembe za ubongo zinaweza kustahamili kabla hazijafa(Infarction) kwa kukosa Oxygen na Glucose.Na muda huu hauzidi dakika tano,kwa hiyo kama ubongo ukikosa damu kwa zaidi ya dakika moja mtu huwa anazimia lkn ataweza kunyanyuka na kuwa katika hali ya kawaida lakini ikiwa ni muda mrefu inasababisha cells za ubongo kufa(Cerebral Infarction a.k.a stroke) ambazo baadae husababisha matatizo makubwa katika ubogo.
Cha maana hapa ni kuangalia ni kitu gani kilichosababisha hiyo SYNCOPE kwa Mheshimiwa Rais,km sababu itakuwa ni miongoni mwa nilizozitaja hapo mwanzo basi hata kama imemtokea mara kumi haina tatizo ilimradi tu kila inapotokea awe anapata fahamu ndani ya "Reperfusino Time Window".Lakini kama kuna sababu nyingine kwa mfano matatizo ya moyo(Yaani Moyo unashindwa kusukuma damu vizuri kwenda kwenye ubongo) au Cerebral embolism(yaani kama kuna mafuta kwenye mirija ya damu ya ubongo au uvimbe nk) basi anahitaji tiba ya magonjwa hayo kwa maana Syncope inaweza kusababishwa na ugonjwa au Normal physiological mechnism ya mwili.Ili kutibu inabidi utibu ugonjwa(kama imesababishwa na ugonjwa) au km imesababishwa na mambo ya kawaida ya kila cku kama uchovu basi unatakiwa kupumzika,kama ni joto basi ukakae kivulini,kama njaa ukale,kama umeshtushwa basi ulale nk,yaani uondoe ile sababu tu then mtu atakuwa ok.
Kwa hiyo tukizungumzia kilichomtokea Mheshimiwa yaani SYNCOPE kwa mtazamo wangu naona ni kawaida tu na hakina matatizo yoyote.Labda swali litakuja juu ya kilichosababisha(kama ni uchovu na njaa tu au ugonjwa wa moyo au ubongo),lkn pia naamini hakuna tatizo kwa sababu kama angekuwa na matatizo makubwa Madaktari wake wasingemshauri kuendelea na kazi ngumu kama anazofanya sasa.Na ikumbukwe pia kama ingesababishwa na magonjwa ya ubongo asingeweza kunyayuka ndani ya dakika tano, huwa inachukua mpaka masaa24,na kama ingekuwa moyo pia ingechukua muda mrefu mpaka kunyanyuka na asingeweza kuendelea na kile alichokuwa akikifanya.
Nafikiri umenipata kaka,kama kuna mahali hujaelewa let me know.
Jamani mnaandika maneno mengi sana wengine wavivu kusoma!!!!!!!
Hakuna lolote,hao wanarogana tu.
Mungu humuonesha binadamu ni kitu gani kinaweza tokea mbele, kwa kutumia ishara. Ndo mana kuna wakati unaweza taka kutoka kwako, moyo ukawa unasitasita, na mara nyingi ukiukaidi au kupuuza zile hisia, lolote linaweza tokea, kule unakokwenda au kule ulikotoka. Mwaka 1995, Mwalimu Nyerere, alimkataa KIKWETE kwa kisingizio kuwa umri wake ni mdogo, lakini ile haikuwa sababu, Mwalimu aliona mbali sana juu ya mtu huyu. Mwaka 2000 ni huyu huyu Kikwete aliyeanguka pale Jangwani katika kampeni zake, kipindi hiki tena ameanguka, zote hizi zilikuwa ishara tulizopewa na tunazoendelea kupata kuwa mtu huyu hafai. bado wa Tanzania hawatumii ishara hizi kuzinusuru. Tatizo wengi wana masikio lakini hawasikii, wana macho lakini hawaoni.

Mwenye macho aone na mwenye masikio asikie

CHA 29:7 na kuendelea.
Kweli kabisa kaka, hapo niko pamoja na wewe. Mtu mmoja aanguke jukwaani mara nne tena kwa aibu vile kweli! Hiyo ni ishara tosha kutoka kwa Mungu.

Cha the Great. (true Rasta) said:
Mungu humuonesha binadamu ni kitu gani kinaweza tokea mbele, kwa kutumia ishara. Ndo mana kuna wakati unaweza taka kutoka kwako, moyo ukawa unasitasita, na mara nyingi ukiukaidi au kupuuza zile hisia, lolote linaweza tokea, kule unakokwenda au kule ulikotoka. Mwaka 1995, Mwalimu Nyerere, alimkataa KIKWETE kwa kisingizio kuwa umri wake ni mdogo, lakini ile haikuwa sababu, Mwalimu aliona mbali sana juu ya mtu huyu. Mwaka 2000 ni huyu huyu Kikwete aliyeanguka pale Jangwani katika kampeni zake, kipindi hiki tena ameanguka, zote hizi zilikuwa ishara tulizopewa na tunazoendelea kupata kuwa mtu huyu hafai. bado wa Tanzania hawatumii ishara hizi kuzinusuru. Tatizo wengi wana masikio lakini hawasikii, wana macho lakini hawaoni.

Mwenye macho aone na mwenye masikio asikie

CHA 29:7 na kuendelea.
inaamaana hali hii usubilia uchaguzi tu?

George said:
Kaka nashukuru sana kwa kunielewesha na kunifumbua macho, sasa ninaona. Tunafurahi sana kuwa na watu muhimu kama wewe hapa kijijini kwetu.
ahmad kombo said:
Nashukuru kaka.Syncope inasababishwa na damu kuwa chache ubongoni,kwa hiyo km inatokea mtu amepatwa na tatizo hilo lkn likaisha ndani ya "Reperfusion time window" basi mtu ata-recover completely hata km itatokea mara tatu kwa mwezi si tatizo.Kinachoangaliwa ni kwamba ubongo haujaathirika.
Reperfusion time window ni muda ambao chembechembe za ubongo zinaweza kustahamili kabla hazijafa(Infarction) kwa kukosa Oxygen na Glucose.Na muda huu hauzidi dakika tano,kwa hiyo kama ubongo ukikosa damu kwa zaidi ya dakika moja mtu huwa anazimia lkn ataweza kunyanyuka na kuwa katika hali ya kawaida lakini ikiwa ni muda mrefu inasababisha cells za ubongo kufa(Cerebral Infarction a.k.a stroke) ambazo baadae husababisha matatizo makubwa katika ubogo.
Cha maana hapa ni kuangalia ni kitu gani kilichosababisha hiyo SYNCOPE kwa Mheshimiwa Rais,km sababu itakuwa ni miongoni mwa nilizozitaja hapo mwanzo basi hata kama imemtokea mara kumi haina tatizo ilimradi tu kila inapotokea awe anapata fahamu ndani ya "Reperfusino Time Window".Lakini kama kuna sababu nyingine kwa mfano matatizo ya moyo(Yaani Moyo unashindwa kusukuma damu vizuri kwenda kwenye ubongo) au Cerebral embolism(yaani kama kuna mafuta kwenye mirija ya damu ya ubongo au uvimbe nk) basi anahitaji tiba ya magonjwa hayo kwa maana Syncope inaweza kusababishwa na ugonjwa au Normal physiological mechnism ya mwili.Ili kutibu inabidi utibu ugonjwa(kama imesababishwa na ugonjwa) au km imesababishwa na mambo ya kawaida ya kila cku kama uchovu basi unatakiwa kupumzika,kama ni joto basi ukakae kivulini,kama njaa ukale,kama umeshtushwa basi ulale nk,yaani uondoe ile sababu tu then mtu atakuwa ok.
Kwa hiyo tukizungumzia kilichomtokea Mheshimiwa yaani SYNCOPE kwa mtazamo wangu naona ni kawaida tu na hakina matatizo yoyote.Labda swali litakuja juu ya kilichosababisha(kama ni uchovu na njaa tu au ugonjwa wa moyo au ubongo),lkn pia naamini hakuna tatizo kwa sababu kama angekuwa na matatizo makubwa Madaktari wake wasingemshauri kuendelea na kazi ngumu kama anazofanya sasa.Na ikumbukwe pia kama ingesababishwa na magonjwa ya ubongo asingeweza kunyayuka ndani ya dakika tano, huwa inachukua mpaka masaa24,na kama ingekuwa moyo pia ingechukua muda mrefu mpaka kunyanyuka na asingeweza kuendelea na kile alichokuwa akikifanya.
Nafikiri umenipata kaka,kama kuna mahali hujaelewa let me know.
Du! Ndio leo nasikia hii habari ya mwenyekiti wa CCM kuanguka. Kutokana na maelezo ya waliopita, iwapo kaanguka hadharan mara nne, je huko nyumbani ndani kwake je? Siajabu nyumbani kaanguka mara nyingi tu. Hapa siwezi sema mengi, na siamini kama ni imani za kishirikina. Watu tunatembea na maradhi na tukumbuke kuwa maraisi wote wanaoingia Ikulu hawawezi kuwa na afya sawa.

Jamani iwapo mtu unajiskia umeamka vibaya ni vyema kupunguza majukumu au ikibidi pumzika hadi ujisikie nafuu. Na kama hali inaendelea basi bora umuone doctor. Pia tukumbuke kuwa mazingira ya kazi au tunayoishi, familia na n.k. vinaweza sababisha stress na wengi wetu tusijielewe kuwa tuna tatizo hilo. Watu tumeumbwa tofauti kuna wengine wanamudu matatizo wengine hawezi. Nikirudi upande wa JK, naweza sema kuwa yawezekana campaign imechangia kuanguka kwake maana hapo tukumbuke wagombea hawalali wanahangaika mchana na usiku kutafuta mbinu ya kukushawishi wewe mwananchi kwani ni wewe ndiye mwenye uwezo wa kuwapa hayo madaraka kupitia kura yako ya ndio.

JK angekuwa UK, doctors wake wangemshauri apunguze majukumu. Na siajabu deputy wake angeshika nafasi yake kugombea uraisi na yeye kupumzika. Cheo cha kuongoza nchi ni dhamana kubwa sana na ni kazi ngumu sana + kuongoza CCM. Tatizo viongozi wetu barani Africa hawana utamaduni huo wa kuachiana madaraka wanataka hadi muda wao wa kuchaguliwa uishe. Mfano mzuri ni yule raisi wa Nigeria aliyefariki mwaka huu na Dr. Kamuzu Banda kipindi alipopata mental breakdown.

Samahanini kwa kiswahili kibovu
Cha the Great una akili sana wewe kama Denzil the Africanus.

Mwalimu Nyerere alikuwa na natural power ambayo ilimwezesha ku-evaluate & analyse
mambo mengi sana kipindi alipokuwa hai na sasa tunayashuhudia TZ. Nakumbuka kipindi cha uhai wake alilaani vikali soko huria (Free Market) na kusema ni "ulaghai na ujanja ujanja tu wa watu wachache kutaka kujinufaisha" na kuwa soko huria halitodumu. Watu sasa hivi wanatafuta kila mbinu hata kuuza nyumba zao ili mradi tu wapate ubunge ili waweze fanya biashara zao kwa urahisi, wezi toka nchi za magharibi nao wamegeuza TZ ndio soko la mwenda wazima na kuja kuiba mali asili zetu na kuacha zilizoko nchini kwao kama reserve (e.g. diamond and gold in Canada).

cite>Cha the Great. (true Rasta) said:
Mungu humuonesha binadamu ni kitu gani kinaweza tokea mbele, kwa kutumia ishara. Ndo mana kuna wakati unaweza taka kutoka kwako, moyo ukawa unasitasita, na mara nyingi ukiukaidi au kupuuza zile hisia, lolote linaweza tokea, kule unakokwenda au kule ulikotoka. Mwaka 1995, Mwalimu Nyerere, alimkataa KIKWETE kwa kisingizio kuwa umri wake ni mdogo, lakini ile haikuwa sababu, Mwalimu aliona mbali sana juu ya mtu huyu. Mwaka 2000 ni huyu huyu Kikwete aliyeanguka pale Jangwani katika kampeni zake, kipindi hiki tena ameanguka, zote hizi zilikuwa ishara tulizopewa na tunazoendelea kupata kuwa mtu huyu hafai. bado wa Tanzania hawatumii ishara hizi kuzinusuru. Tatizo wengi wana masikio lakini hawasikii, wana macho lakini hawaoni.

Mwenye macho aone na mwenye masikio asikie

CHA 29:7 na kuendelea.
CHA umetoa pinti kali sana,inaelekea ww niwa CHADEMA.
Kiswahili safi hicho Mama Malaika. Acha kujishusha
Te tehe tehe tehe! Alfan, kama gazeti la Mzalendo ingekuwa ndio mtihani wa kupata ajira, nahisi ungekosa ajira nyingi.

Alfan Mlali said:
Jamani mnaandika maneno mengi sana wengine wavivu kusoma!!!!!!!

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*