Tags:
Kweli kabisa kaka, hapo niko pamoja na wewe. Mtu mmoja aanguke jukwaani mara nne tena kwa aibu vile kweli! Hiyo ni ishara tosha kutoka kwa Mungu.
Cha the Great. (true Rasta) said:Mungu humuonesha binadamu ni kitu gani kinaweza tokea mbele, kwa kutumia ishara. Ndo mana kuna wakati unaweza taka kutoka kwako, moyo ukawa unasitasita, na mara nyingi ukiukaidi au kupuuza zile hisia, lolote linaweza tokea, kule unakokwenda au kule ulikotoka. Mwaka 1995, Mwalimu Nyerere, alimkataa KIKWETE kwa kisingizio kuwa umri wake ni mdogo, lakini ile haikuwa sababu, Mwalimu aliona mbali sana juu ya mtu huyu. Mwaka 2000 ni huyu huyu Kikwete aliyeanguka pale Jangwani katika kampeni zake, kipindi hiki tena ameanguka, zote hizi zilikuwa ishara tulizopewa na tunazoendelea kupata kuwa mtu huyu hafai. bado wa Tanzania hawatumii ishara hizi kuzinusuru. Tatizo wengi wana masikio lakini hawasikii, wana macho lakini hawaoni.
Mwenye macho aone na mwenye masikio asikie
CHA 29:7 na kuendelea.
Du! Ndio leo nasikia hii habari ya mwenyekiti wa CCM kuanguka. Kutokana na maelezo ya waliopita, iwapo kaanguka hadharan mara nne, je huko nyumbani ndani kwake je? Siajabu nyumbani kaanguka mara nyingi tu. Hapa siwezi sema mengi, na siamini kama ni imani za kishirikina. Watu tunatembea na maradhi na tukumbuke kuwa maraisi wote wanaoingia Ikulu hawawezi kuwa na afya sawa.
Jamani iwapo mtu unajiskia umeamka vibaya ni vyema kupunguza majukumu au ikibidi pumzika hadi ujisikie nafuu. Na kama hali inaendelea basi bora umuone doctor. Pia tukumbuke kuwa mazingira ya kazi au tunayoishi, familia na n.k. vinaweza sababisha stress na wengi wetu tusijielewe kuwa tuna tatizo hilo. Watu tumeumbwa tofauti kuna wengine wanamudu matatizo wengine hawezi. Nikirudi upande wa JK, naweza sema kuwa yawezekana campaign imechangia kuanguka kwake maana hapo tukumbuke wagombea hawalali wanahangaika mchana na usiku kutafuta mbinu ya kukushawishi wewe mwananchi kwani ni wewe ndiye mwenye uwezo wa kuwapa hayo madaraka kupitia kura yako ya ndio.
JK angekuwa UK, doctors wake wangemshauri apunguze majukumu. Na siajabu deputy wake angeshika nafasi yake kugombea uraisi na yeye kupumzika. Cheo cha kuongoza nchi ni dhamana kubwa sana na ni kazi ngumu sana + kuongoza CCM. Tatizo viongozi wetu barani Africa hawana utamaduni huo wa kuachiana madaraka wanataka hadi muda wao wa kuchaguliwa uishe. Mfano mzuri ni yule raisi wa Nigeria aliyefariki mwaka huu na Dr. Kamuzu Banda kipindi alipopata mental breakdown.
Samahanini kwa kiswahili kibovu
Te tehe tehe tehe! Alfan, kama gazeti la Mzalendo ingekuwa ndio mtihani wa kupata ajira, nahisi ungekosa ajira nyingi.
Alfan Mlali said:Jamani mnaandika maneno mengi sana wengine wavivu kusoma!!!!!!!
CHA umetoa pinti kali sana,inaelekea ww niwa CHADEMA.
jifunze sana:
Mara ya kwanza alisema Uchovu wa Safari
Mara ya pili walisema Uchovu wa Kampeni 2005
Mara ya tatu wamesema ni Sukari na Swaum 2010
Ni kweli jifunzeni Siasa raha sana unadanganya hata madaktari
Jamani mnaandika maneno mengi sana wengine wavivu kusoma!!!!!!!
Hahhaha mie na ww kumbe tupo sawa duh
Alfan Mlali said:Jamani mnaandika maneno mengi sana wengine wavivu kusoma!!!!!!!
© 2022 Created by Tulonge.
Powered by