Tulonge

Kitabu hiki ni baadhi ya vitabu vya jifunze Kiswahili Fasaha ambavyo vimesaidia sana mashuleni wanafunzi kujifunza kiswahili fasaha. Unakumbuka vitabu vingapi?? 

Mie nakumbuka hicho juu cha Paulo na hivi hapa (titles)
1) Fikiri na Sadiki
2) Kibanga ampiga mkoloni
3) Bulicheka na nduguze
4) Twende tukawinde Ngedere

Wewe unakumbuka vingapi pamoja na hadithi zake? je vitabu vipi vya mashairi unavyokumbuka? Tukumbusheni jamani. LOL.....

 

Iwapo kuna mtu anajua wapi nitaweza kupata na kununua vitabu hivi na vinginevyo vya kiswahili naomba aniambie nahitaji ajili ya kufundishia watoto wangu. Pia vitabu vya mashairi ya kiswahili

Views: 2694

Reply to This

Replies to This Discussion

Duuh! umenikumbsha mbali sana, mimi siju hata vinapatikana wapi hivyo vitabu.

Ona hii stori, nadhani ndiyo ya Kibanga ampiga mkoloni.

KIBANGA AMPIGA MKOLONI

Zamani za ukoloni, palitokea Mzungu mmoja. Mzungu huyo hakuwa mtu mwema. Alikuwa mkali na mkatili sana. Kwa ajili ya ukatili wake watu walimwita mkoloni. Wanancgi wote walimchukia sana popote pale alipokwenda.


Mzungu huyo alikuwa Bwana Shamba. Alikuwa na bakora iliyokuwa imetengenezwa kwa mkwaju. Kila alipokwenda kukagua mashamba, alikuwa na bakora hiyo mkononi. Alipendelea sana kuitwa "Bwana Mkubwa". Mkolono huyo alifurahia sana kupiga watu. Aliwapiga watu waliposhindwa kupalilia mashamba. Aliwapiga pamba yao ilipokuwa chafu. Aliwapa taabu sana.

Katika kijiji cha Kwachaga, Wilaya ya Handeni, alikuwapo mzee mmoja aliyeitwa Kibanga. Mzee huyu alikuwa mwenye nguvu, hodari na shujuaa. alikuwa fundi wa mieleka. Ingawa alikuwa mwenye nguvu, alikuwa mpole. Hivyo watu wa Kwachaga walimpenda na kumtegemea kuwaongoza vitani.

Siku moja yule Mzungu alifika Kwachaga kukagua mashamba ya mihogo. Jumbe pamoja naye wakatembelea mashamba. Kwa bahati mbaya mwaka ule haukuwa na mvua ya kutosha. Kwa hiyo mihogo haikustawi. Kila wakati yule Mzungu alipotazama mashamba alitikisa kichwa na kufoka. Mwisho akamwagiza Jumbe kuitisha mkutano wa watu wote wa kijij. Waliporudi kijijini Jumbe akapiga mbiu. Watu wote wakakusanyika. Walipofika tu, yule Mkoloni akaanza kuwatukana, akawaambia, "Ninyi watu weusi ni wavivu sana. Hamfanyi kazi sawa sawa. Mashamba yenu ni mabaya sana". Jumbe akataka kumjibu ili kumweleza kwa nini mihogo haikustawi. Kabla hajamweleza yule Mzungu alimrukia na kumpiga kofi. Kisha akasema, "Sitaki kijibiwa na wewe, mvivu wa wavivu". Watu wote wakakaa kimya. Hakuna aliyeweza kufanya kitu.

Kibanga akajitokeza, akasimama. Akamtazama yule Mkoloni kwa dharau sana. Kisha akamwuliza, "Kutuita sisi wavivu ndiyo nini? Na kumpiga Jumbe wetu mbele yetu, maana yake nini?"

Kabla ya kumaliza kusema, Mkoloni aliamka kitini kwa hasira , akataka kumpiga Kibanga. Alishika bakora yake mkononi. Akasedma, "Nitakuadhibu vibaya kima we! Unajifanya kuwa shujua? Huwezi kucheza na bwana mkubwa. Nitakupiga, kisha utakwenga jela miezi sita." Lakini Mkoloni hakuwahi kumwadhibu Kibanga. Aliadhibiwa yeye. Kabla ya kumfikia, Kibanga alimpiga chenga. Kisha akamrukia, akamnyangánya bakorta yake. Akaitupa, ikaokotwa na vijana, wakaificha.Kibanga alimshika yule Mzungu akamwambia. "Wewe umezoea kutoa amri kila siku, lakini leo utashika adabu, mbwe wee!" Papo hapo alimnyanyua juu na kumbwaga chini, puu! Yule Mkolono akaumia sana. Kabla ya kuamka, Kibanga alimwinua tena na kumbwaga chini kama furushi la pamba. Akamkalia.Hapo yule Mkoloni akawa hana la kufanya. Bila ya bakora alikuwa hana nguvu. Akaomba radhi akilia, "Samahani! Naumia! Nihurumie! Sitafanya tena hivyo." Kibanga alimjibu kwa dharau, "Sikuachi mbwa wee! Leo utakiona cha mtema kuni! Ulijiona una nguvu. Leo nitakutengeneza."Wazee wakamshika Kibanga na kumwomba asimpiga tena. Akamwacha. Kwa shida yule Mkoloni akajikokota kwenda hemeni. Alikuwa amejaa vumbi huku damu zikimtoka. Wazee wengine wakamfuata nyuma. Walinyamaza kimya, wakimhurumia. lakini vijana walifurahi sana.

Baadaye waliimba wimbo wa kumsifu Kibanga.Jioni yule Mkoloni aliomba radhi kwa wazee. Mzee mmoja akasimama na kumwambia, "Umefanya vizuri kuomba radhi, nasi tunaipokea. Lakini tangu leo usijivunie ubwana. Jivunie utu. Ninyi wakaoloni mna kiburi. Mnatudharau. Kama ungetuuliza tungekuambia kwa nini migogo haikustawi. Haya yote yamekupata kwa sababu ya kiburi chako. Katika nchi hii tuanaamini kuwa kiburi si maungwana".Baada ya hapo wazee wakamsamehe, lakini hawakumpa bakora yake. Ikabaki nyumbani kwa Jumbe. Yule Mkoloni akaondoka. Tangu siku hiyo hakufika tena Kwachaga. Kila mara alipokutana na watu aliyakumbuka maneno ya yule mzee, "Kiburi si maungwana".Siku hizi kijiji cha Kwachaga kina maendele mazuri ya kilimo na mifugo. Maendeleo yote yamepatikana kwa sababu ya uongozi bora wa Serikali ya wananchi.

Nimekifuma sehemu, hiki ndicho kitabu chenye hadithi ya Kibanga Ampiga Mkoloni.Nimekosa picha kubwa

Duh!! Kijana naona na wewe umo.. Lol!!! Asante kwa kutukumbusha hiyo Hadithi ya Kibanga!

Mama M umerudisha kumbukumbu nzuri sana!! Sijui kweli wapi tunaweza vipata hivi vitabu lakini ngoja tufanye utafiti labda tunaweza vifuma mahali flan..

mimi nakumbuka hadithi ya Fikiri na sadiki, wimbo wa fikiri baada ya kupatwa na njaa ulikuwa hivi

  Fikiri mimi masikini, uvivu wangu nyumbani

  Sadiki sasa ashiba, chakula kingi kwa baba,

  nirudi tena kwa baba, nakufa hapa kanini?

duh Dismas ulikuwa umekiifadhi hicho kitabu, au ulikariri hadithi yote?

Dismas wewe hatari, unakumbuka yote. Mzungu alishika adabu yake. Ha haa haaaa......

Asante sana Dismas kwa hadithi nzuri yenye hekima na busara..... 'Kiburi si maungwana'
 
Tulonge said:

Nimekifuma sehemu, hiki ndicho kitabu chenye hadithi ya Kibanga Ampiga Mkoloni.Nimekosa picha kubwa

Dixon nitahsukuru na kufurahi sana, hata kama vimetumika viko vichakavu ili mradi viwe na kurasa zake zote ndani. LOL..... 

Mie kwangu hivi vitabu vilinisaidia sana kiswahili ukizingatia kiswahili nilijifunzia shuleni, nilikuwa navisoma hadi nikirudi nyumbani tena kwa kwa kukalili. LOL.... 
 
Dixon Kaishozi said:

Mama M umerudisha kumbukumbu nzuri sana!! Sijui kweli wapi tunaweza vipata hivi vitabu lakini ngoja tufanye utafiti labda tunaweza vifuma mahali flan..

Mama Manka bado una kumbukumbu...

Teh teh teh Manka siwezi kariri hadithi lote hilo, nina mambo mengi ya kukariri kwa sasa. Nimeikuta sehemu tu kwenye net ndo nikaiweka hapa.

manka said:

duh Dismas ulikuwa umekiifadhi hicho kitabu, au ulikariri hadithi yote?

Dah mmenikumbusha mbali sana Enzi za sizitaki mbichi hizi na Ile ya kalamu mbili zimemshinda fisi

Mimi nakikumbuka kitabu cha kiswahili "Juma na Uledi", "Eva na Musa" na "Hawafu mwenye nguvu"

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*