Alizaliwa 18 July 1918 na kufariki 5 December 2013 akiwa na umri wa miaka 95. Amekuwa Rais wa Afrika Kusini kwa miaka minne tu yaani toka 1994-1999.
Nilibahatika kumuona Nelson Mandela alipokuja Tanzania--wakati huo akiwa na Julius Nyerere pale uwanja wa Taifa, Dar Es Salaam. Alikuwa akipunga mkono akiwa katika gari ya wazi pamoja na Nyerere.
Inawezekana wengi wenu hamjabahatika kumuona moja kwa moja--Ila iwapo mngebahatika kumuona na kupata nafasi ya kumuuliza maswali, ni maswali gani matano ambayo mngemuuliza Mzee Madiba?
Tags:
MImi nadhani hata mdau angekua na swali moja la kumuuliza alitupie hapa.Maana najua kuna baadhi ya wadau maswali matano ni mengi sana. Ila kama mtu ana maswali matano atupie tu. Mtu kama Severin kwa vyovyote hawezi kuwa na maswali matano kwa mwana siasa teh teh
Baada ya mtu mzalendo kama yeye afrika kabaki nani?
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by