Tulonge

Wadau wa Biashara/Huduma za Utalii Tanzania, nawasalimu kwa upendo. naomba kutoa mawazo yangu. Hivi kwa nini kusiwe na umoja wa kweli utakaoleta maendeleo ya haraka katika sector ya Utalii???? Pamoja na kwamba bei ni siri ya mtu, mbona kusiwe na kima cha chini katika bei zetu? Tukiwa waaminifu katika hili, kwa nini kila mdau asiwe na maendeleo makubwa kiuchumi kila mwaka? Kwa mfano, tukikubaliana wote kwamba, kupanda mlima Kilimanjaro isiwe chini ya dola 2,000 kwa kichwa, halafu kila watalii wakiuliza bei wasipate chini ya hapo, je, hawatapanda mlima? Tunaposhusha sana bei, tunainyima Serikali yetu mapato (Kodi) na sisi wenyewe tunajinyima mapato. Competition zisizo na tija zinaturudisha nyuma. kwa wanaojua Biashara, naamini wananielewa. Hii itatuwezesha kununua magari bora ya kuwahudumia wateja kila mwaka, vifaa vya camping, na hata kujenga hoteli zetu wenyewe, bila kusahau kuweka familia zetu na mazingira katika hali bora zaidi kila mwaka. TAFAKARI.

Views: 760

Reply to This

Replies to This Discussion

Wazo zuri dada Hellen, naona ukiwa karibu na http://tulonge.com/profile/JeathvinSafaris itakua poa sana.Naona mambo yenu yanaendana.

 wazo lako kweli ni zuri Dada helen, tatizo linakuja kwa hao wanaohusika na company za utalii biashara ya utalii wanaichukulia serious  au wapo tu wagange njaa?, maana kwa sasa TZ kila kampuni inayojihusisha na utalii inabei yake ya huduma na hili linafanya bishara kukosa ushindani, miye naona mngeweka bei moja ushindani uwe kwenye ubora wa huduma, mtalii achague kutokana na ubora wa huduma na siyo unafuu wa bei.

Wazo ni jema sana, ila shida ni kwamba waliosshikilia makampuni ya utalii wengi ni watu wa nje (Foreigners) ambao hawako tayari kufanya kwa maslahi ya kwetu hata kidogo. na kwanza wakisikia kampuni ya mzawa wataifuatilia sana kuona kama kuna kasoro wapate kukuharibia. sasa kuhusu baadhi ya watanzania wenzangu sio waelewa na unakuta sisi kwa sisi tunapigana vita bila sababu. ni shida na ukiangalia sana utaona sio tu upande wa utalii bali katika nyanja zote watanzania tunabaguana sana wenyewe kwa wenyewe na ndo maana maendeleo yanakua madogo sana. 

Nini kifanyike ili umoja huu ufanye kazi???? Mawazo yenu muhimu, kisha tutayapeleka kwenye vyama vya wadau wa Utalii Tanzania.

Duuh ngoja nitoke safari , nikitulia kwangu nitakupa maelezo kuhusu hili...maaana hapa kuna mambo mengi  ya wazi inabidi yaangaliwe......mfano ondoeni commission muone kama mtapata wageni....wale mashanti watakula wapi?....wekeni vikwazo vigumu na ushuru mzito kwa wageni wanofungua kampuni na kuleta watu wa nchi zao tu na lugha zao, wakati pembeni wana kazi kama za NGO...acheni kumpigia mzungu magoti wakati ni binadamu kama ndugu yangu mjita.....!

Huwezi kupanga bei moja ya mlima kwani; kuna route tofauti na zote sio cocacola route!...siku za kupanda pia zinatofautiana kutokana na route

Kuna watu wanapitia machame then wanataka kupitia ile sehemu ya hatari ya Glaciers....hiyo ni bei tofauti...etc etc   etc

watu wana njaaa so akipata faida kidogo anachapa kazi

Ushauri:....badala ya kufikiria kitu kama dola 2000 kwa kupanda mlima...bora watu mjipange na iwekwe bei fixed  kama tuseme  $350(eg) per day per pax na ni kwa route zote.....think?????

Ngoja nitoke trip nimalizie hapa my Sister

Enzi hizo mpinzani alikua Zara(tena ndo kalikua kanaanza)....na Sunny safaris.........tulistaaafu maana pesa ya season ina laaaana...hahahahahaha  ....naona imeanza kukutia presha maana msimu ndo huu tehtehteh

Mwisho kwa leo:  Wazungu hawana pesa siku hizi kama zamani...wamefulia...niulize mimi niliye jikoni..au muulize sister  Mama malaika  au Eddie na wengineo.....tourism is slowly dying.  Simba, tembo chui n.k wote mmeuza wamejaa huku Zoo. unalipa Euro 5 unaona kila mnyama tena hata ukitaka kushinda huko ni pouwaaaa tu hadi wafunge

Sasa kama Mwafrika huku anafanya kazi  alafu mshahara wake sometime unazidi wa mwenzake mzungu(positionwise)  unategemea nini.     Kuna wazungu ombaomba wakishuka bongo wanaitwa sir wakati vishuka...teeeh...... I WILL BE BACK!!!!

Nimekupata. Ila kuna mahali ambapo hukunielewa. Kupanga bei haimaanishi zifanane katika route zote. Nilitolea mfano tu wa route moja. Kila route ina mipango yake, Camping na Huts ni tofauti, camping zenyewe pia bado zinatofautiana. Minimum ya kila route, mtu apandishe awezavyo, ila asishuke chini ya....... Wageni wakicheck website, wakituma inquiries, namna yoyote wakakuta hakuna Kampuni inayopandisha chini ya........ hicho tutakachokuwa tumekubaliana, wataacha kuja? Mimi nimefanya kazi kwenye Kampuni moja ya Wafaransa Arusha, watalii walikuwa wanatumia dola 12,000$ kwa kichwa kuhudumiwa na kampuni ile. Ile Kampuni ikizikamata hizo 12,000$, inamlipa Tour Operator wa Moshi au Arusha dola 970 za mlima Marangu route (mwaka 2006), inakodi magari ya safari dola 170$ kwa siku, siku 4 tu, kisha inawarudisha airport wanarudi kwao. Mapesa mengi wanabaki nayo, wanatulipa sisi wenye njaa zetu kiduchuuuu!!!! Ilikuwa inaniuma sana. Pamoja na wazungu kufilisika sasa hivi, sio kiasi hiki!!!

Unachokisema ni ukweli mtupu, yani saivi hii biashara imekuwa ngumu sana ni kama imeingiliwa na vimelea..hiyo yote ni kutokana kutokuwa na msimamo na umoja katika biashara hii kila mtu anapanga bei yake....sasa huu sio ushindani wa biashara huku ni kushindwa kuimudu biashara......TUJIPANGE!!

Umesema kweli kaka. Imagine, sisi ndio wenye mbuga za wanyama, n.k. lakini wajanja wanazifaidi kuliko sisi. Hali hii mpaka lini? Halafu ukienda kulalamika mahali, huyo unayemlalamikia hana muda wa kufuatilia sababu wengi wanajua nini kinachoendelea, na wanakata tamaa. Si kwamba watu wote hawafahamu. Ila nani atamfunga paka kengele? Wanaacha watu wajifanyie vyovyote tu, ili wawatawale vizuri. Wanajua tukiungana, hawataweza kuponyoka. Ile formula ya 'divide and rule' inafanya kazi sana kwenye maendeleo ya watu. Tukiwa tumegawanyika, hatuna umoja, hata sauti zetu hazisikiki. Lakini kama tungekuwa na umoja, tungepata 'nguvu ya hoja.' Ubinafsi umezidi. Mtu anaridhika tu kwa sababu anapata mkate wake wa kila siku na familia yake. Hafikiri baadaye watoto na wajukuu zetu watakuwa katika hali gani, wakati ambapo pato lote litakuwa limehamia nje, hapa zinabaki pesa za uendeshaji tu!! Tusije tukakumbuka shuka wakati kumekucha.

Unajua tatizo la nchi hii.........Loading.........Please try to restart your Computer so as to view this comment.

Still Loading.
Mwenye macho asikie, na mwenye masikio aone.
Unajua tatizo la nchi hii.........Loading.........Please try to restart your Computer so as to view this comment.

Still Loading.
Mwenye macho asikie, na mwenye masikio aone.

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*