Tulonge

Habari ndugu members wa Tulonge.Bila shaka mko poa.mwenzenu kwa leo niko kijamii zaidi.Ningependa kuzungumza au kuongea kijamii zaidi kwa kutoa usia au ushauri wa kibusara wenye faida kwa wote ikiwa utafanyiwa kazi.Na ningependa kuanza namna hii kama ifuatavyo:

Kulingana na uzoefu wangu mdogo nilionao katika maisha haya ya dunia, ningependa kuwausia marafiki wote na watu huru mambo ambayo yakifanyiwa kazi huenda yakawa ni kinga madhubuti ya kumkinga mtu kutotumbukia katika shimo la matatizo,majuto na hasara ikiambatana na madhara.Usia wangu ni kama ifuatavyo:

Ndugu yangu, rafiki yangu, mwanadamu mwenzangu,chunga sana na zingatia sana kujiepusha na watu watano:

1-Jiepushe na kusahibiana na muongo, kwa sababu muongo ni mfano wa mazigazi (au mazingaombwe) ikusogezeayo kilicho cha mbali na kukuwekea mbali kilicho cha karibu.

2-Jiepushe na kusahibiana na muovu, kwa sababu muovu atakuuza kwa ajili ya jambo dogo au dogo sana zaidi ya dogo.

3-Jiepushe kusahibiana na bakhili, kwa sababu bakhili atakudhalilisha katika mali zake na kukufedhehesha na kukufukarisha kwa ufukara zaidi ya ulivyo.

4-Jiepushe kusahibiana na mjinga (mwenye upumbavu), kwa sababu mjinga akitaka kukunufaisha ndio anakudhuru.

5-Jiepushe kusahibiana na mkata udugu, kwa sababu mtu huyu nimemkuta akiwa ni mwenye kulaaniwa katika vitabu vitukufu vya Mwenyeezi Mungu Muumba.

Pia baada ya kujiepusha na hao watano zingatia kuchunga haki za watu unazotakiwa au ambazo ni wajibu kwako kuzitekeleza maana kufanya hivyo hupelekea kuwepo usalama kwa nafsi ya mtu , na hupelekea utu wa mtu kuonekana ikiwa atachunga haki za watu na kuwajali.

Si hivyo tu bali pia hupelekea mtu kusalimika na kuwa katika amani kwa kutofanyiwa ubaya, maana iko wazi kwamba ikiwa utazikanyaga haki za watu,ukawakandamiza,ukawa jeuri mbele yao,ukawafanyia uadui na kuwadhalilisha,zaidi ya hayo usiwatimizie haki zao unazotakiwa kuzitimiza kisheria au kiuanadamu,basi ujue kwamba kwa kufanya hivyo utakuwa unawafanya au unawaandalia watu hao mazingira ya kukulipizia kisasi cha ubaya, maana ubaya hulipwa kwa ubaya kama ambavyo uzuri hulipwa kwa uzuri.

Kisha zingatia kutomkubalia rafiki yako katika jambo ambalo madhara yake na majuto yatarejea kwake.Ukifanya hivyo utakuwa umemuokoa rafiki yako.WE - SITILI  -TUGEZA.

Mola awabariki.

Views: 433

Reply to This

Replies to This Discussion

Upo juu mkuu, nashukuru kwa ushauri.
safi sana il-ya uko sahihi mkuu ni ushauri mzuri kabis kwa kizazi chetu cha sasa
Dah! yaani wewe ni rafiki wa kweli naomba usiishie hapa.  ila mtu mjinga na mpumbavu ni yupi? au utamtambuwaje?
Asante sana! Tupo TUGEZA kabisa!
ahsante message delivery

Asante sana na Mungu akubariki pia!

Pamoko kama kawa!

Kaka @Omari:

kuhusu swali lako kunako mjinga au mpumbavu kwamba utamtambua vipi,ni rahiusi sana kaka.

Tunaposema mpumbavu tunaanisha mtu mwenye tabia ya upumbavu.Mpumbavu utamjua tu katika vitendo vyake,mpumbavu huwa hajui matokeo ya matendo yake.Hajui hili nikilifanya lina faida au lina hasara,yeye hufanya tu.Mtu kama huyu anaweza kufanya jambo kwa lengo na nia nzuri lakini matokeo ya jambo hilo yakawa ni madhara kwa nafsi yake au nafsi ya mtu mwingine.Lakini kama angelijua kuwa jambo fulani lina faida na jambo fulani lina hasara na madhara ukilifanya,basi hawezi kufanya mambo kw akubahatisha bali atafanya akiwa na uhakika kwamba ninalolifanya ni lenye manufaa au madhara.

 

Mfano: ni mfano tu wandugu: Mtu anayewaua watoto wake ili kukabiliana na hali ngumu ya maisha,mtu huyu ana nia nzuri katika kufanya jambo hilo,kwani anataka kutatua hali ngumu ya maisha inayo mkabili ili asiishi chini ya msitari wa ufukara,ndio lengo lake lake katika kuchagua kuwaua watoto wake,lakini uhakika wa kitendo hicho ni madhara kwake na kwa familia nzima kwa ujumla bali ni madhara pia kwa zile nafsi anazoziua.

 

Mtu huyu kunatokana na upumbavu wake alionao,wa kutojua ni kipi chenye manufaa na chenye madhara,ikawa ndio sababu iliyopelekea kufanya upumbavu huo wa kuwaua wanae.

 

Hivyo mtu kama huyu ni muhimu usisahibiane nae maana anaweza wakati wowote kukuletea madhara akidhani anakunufaisha.Na ukitaka kumjua mpumba zaidi mcheki anavyoutumia muda wake.mpumbavu huwa hajui thamani ya muda.

Nadhani utakuwa umeniget kaka Rafiki Omary.

anyway kama sijaeleweka nitajaribu kutoa maelezo tena ili nieleweke.

Amani kwa wote wa tulonge.

Reply to Discussion

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*