Wengi wetu tumezoea kula vyakula tulivokula kwa mazoea tunamoishi. Unaenda ugenini au nchi ya ugenini, siku ya siku wakutana na wenyeji na wanakukaribisha nyumbani kwao kwa chakula mchana au jioni. Baada ya chakula kuwekwa mezani kama ilivyo pichani hapa juu unauliza hicho kwa sahani ni nini? Unaambiwa na wenyeji wako ni panya wa porini kabanikwa kwa moshi na ndio chakula cha asili cha wenyeji wako.
Wana TULONGE naomba mnambie..... Je iwapo ni wewe utafanya nini? Utasema wazi chakula cha namna hiyo hujakila toka kuzaliwa hivyo hupendelei kula utabakia njaa? Au utajitahidi kula na kuwa polite kwa wenyeji wako?
Tags:
Doh!ni kweli wengi wetu tumezoea kula chakula cha aina moja ambacho tumekizowea,ila ni vizuri pia kujifunza kutoka kwa wengine kama hakikudhuru,mimi hapo mbona ningekula angalau nijue tu hata test yake.mbona mzungu anaweza kula mlenda na ugali kwa mikono.
Mary umesema kweli.... mie nimejikuta nakula vyakula vingi sababu ya safari zangu. Na mara nyingi najisikia aibu kukataa kwani watu wamehangaika kupika. Panya pori wa kuchoma nimemla tena mtamu sikutegemea.
Ukienda ROMA fanya kama WAROMANI wafanyavyo!!! vinginevyo utakufa kwa njaa bure!
duh japo nitastuka kidogo lakini, nitajaribu kwani hapo sina jinsi ndiyo kwanza nipo ugenini,
Kama wao wanakula na mimi nakula tu. Kwanza wagogo wa Dodoma wanagonga sana hawa panya na hawafi wala nini.
Dismas.. sikujua wagongo wanakula hawa panya pori ila nilisikia watu wa mkoa ya Mtwara sijui Lindi wanakula panya. Panya wanaliwa nchi nyingi maana Mozambique, Malawi, Zambia na Zimbabwe wanakula panya pori.
Magere na mama Manka ni kweli, ugenini unaogopa na hasa ukiwa na njaa unakula. LOL....
umesahau ule msemo kuwa kiingicho si najisi ila kitokacho
Mmmmmmh unaweza jilazimisha ili ule 7bb wenyeji wanakula ila ukikumbuka unakula panya unaweza rudisha chenji (kutapika)
haaa mama malaika....nasikia watamu hao kama nyama ya kuku......Ila wanaoliwa ni wale wa porini wanaojitafutia chakula wenyewe...nafanafa na mbegumbegu
Ha haa haa haaa..... jamaa kanifurahisha aliposema "njomba hii kitu kunoga hawa". Naona wachina wakifika sehemu hii wanafurahi sana maana wao wanakula vyote hadi mbwa.
Gratious Kimberly said:
haaa mama malaika....nasikia watamu hao kama nyama ya kuku......Ila wanaoliwa ni wale wa porini wanaojitafutia chakula wenyewe...nafanafa na mbegumbegu
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by