Tulonge

Unawezaje kutafauticha baina ya UTAMU na RAHA ?

 

Utamsikia mtu asema ,"naona utamu...... ama naona raha......"

 

SEMA usikike !!!

Views: 1527

Reply to This

Replies to This Discussion

Nadhani unamaanisha kutofautisha SIYO kutafauticha. Kabila gani wewe?

 

UTAMU unauhisi baada ya kuonja/kula kitu. Kama ukilamba sukari utahisi UTAMU.

RAHA inapatikana baada ya kutendewa kitendo ambacho kitaufanya mwili uburudike.Unapofanya mapenzi na mke/demu wako, ile unayoihisi ni RAHA siyo UTAMU.

 Kwa kifupi RAHA huwezi ipata kwa kula kitu.

 

Yangu ni hayo wadau, kama nimekosea nirekebisheni.

Kuna kibao kimoja cha kizazi kipya kinachonifanya siku zote nisikie utamu kinachokwenda kwa jina la : 'NASIKIA UTAMU', cha kijana mmoja kutoka nchini Kenya maarufu kama MR BUGZ.

Nadhani kijana huyu alikimaanisha utamu unaotokana na mapenzi,alikuwa hamaanishi kwamba labda  alikula mhogo mtaa wa kati ndio akasikia utamu.haiwezekani kwamba kijana alikusudia maana hiyo,bali alikuwa amelenga mbali.Hakuna shaka kwamba utamu hutokana na kula kitu kitamu. 

Lakini hata kama utamu ni neno linalotumika katika kula vitu vitamu,hiyo siyo sababu ya kutolitumia neno hilo sehemu zingine kwa kuazima,kama ambavyo watu hushirikiana katika masha yao, hivyo hivyo ndivyo hata maneno yanavyoshirikiana katika kufikisha ujumbe kwa hadhira,hivyo si watu wenye uhusiano wakaribu bali pia hata maneno nayo yanauhusiano wa karibu wa kimaana ndio maana utaona maneno yanatumika namna hii.

Hivyo si vibaya kutumia neno utamu sehemu ya raha ukimaanisha kwamba raha unazozihisi ni sawa na utamu unaouhisi pindi ulapo kilicho kitamu.Na ndio maana utasikia kaka fulani anasema;DEMU WANGU MTAMU,akimaanisha kuwa demu wake anampa raha zaidi.

Nadhani hivi ndivyo ilivyo kwa ufupi,ngoja nisikilizie na ufafanuzi wa wengine.

Joan ! nie ni mswahili wa kisiwani ,Zanzibar LUGHA yetu ni kiswahili as our mother tongue

 

Mimi nilidhani, Tamu ni peke yake inapatikana katika ULIMI kama ndio kiungo kinachotafautisha ladha ( taste) ingawaje ushiriki wa mate na ubongo ndio hisia za utamu zinapatikana. Achana na usanii wa KIZAZI KIPYA ambao niwapotoshaji wakubwa wa lugha.Wasanii wa ZILIPENDWA pekee walifanya kazi hiyo ya kujali matumizi ya lugha- MFANO : juma kilaza,shaaban marijan,salum abdala,n.k

 

Raha IKO MOYONI - si pekee yake sex activity iletayo raha tu. Ila kuna vitu vingi vinavyomletea raha mtu.

Nimalizie ,hapo muda mwengine naweza kuongelea RAHA Kimaana,mazingira na vitu mbali mbali.

 

KWAHERI !!!

Shukran wadau kwa hili nimeambulia kitu hapa kwani hata ningeulizwa sijui ningejibu nini? Ustaadh Babengwa nakusubiria kwa hamu uje umalizie kuongelea RAHA.. maana tumesikia UTAMU tu atiii.

Shukran wadau kwa hili nimeambulia kitu hapa kwani hata ningeulizwa sijui ningejibu nini? Ustaadh Babengwa nakusubiria kwa hamu uje umalizie kuongelea RAHA.. maana tumesikia UTAMU tu atiii.


RAHA ni hisia za moyo ambazo zinamfariji mtu ajisikie furaha,kupumua,kuburudika,kupumbaa kiasi ajitambue au asijitambue.

Ni yeye peke yake, mwenye raha ataweza kuwa na maelezo sahihi kwa wakati wa raha zake labda kukuelezea,INGAWAJE kila mwenye raha atakuwa na maelezo tafauti,hisia tafauti baina ya yeye na mwengine lakin itabakia ni raha yake.

Wache niyagaie mifano yepi yanampa raha mtu ni mengi ziyamalizi :
  1. KULALA 2. KUONGEA 3. KUNYWA 4. KUVUTA 5.KUTEMBEA 6. KUSIKILIZA 7. KUWA KATIKA KITENDO CHA NDOA 8. KUJISAIDIA( KWENDA HAJA) N.K

Hayo, hapo kufanyika yakamletea RAHA mtu ingawaje wakati mwengine yakaleta KARAHA- HILI linategemea sana - mazingira ya tukio, wakati wa tukio yaani utayari na  mtu kutenda .

 

Niongeze kimfano kidogo kati ya haya mambo niliyoyapa nambari nachukua moja tu.

Kila Mtu anadhani kitendo cha kujamiana kinaleta RAHA.

Hapana-ili kilete RAHA lazima izingatiwa - MAZINGIRA,UTAYARI NA WAKATI.

Sidhani, usiku wa manane umvamie mke aliyelala ukaomba jambo hili litazua RAHA ni KARAHA kwa vile hayo MAMBO MATATU yalipaswa yazingatiwe.

Mama Malaika ,hii habari ni yako ingawa ni faida ya yeyote due to what extent ,being impress what I was talking about....HAHAHAHA!

Baadae !

Shukran.... nimefurahishwa ni mifano uliyotoa imesaidia kuelezea vizuri nini maana ya RAHA

Ahsante sana ,Mama Malaika kwa kufurahishwa nami.......

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*