Tulonge

Nchini Uingereza kuna mume akabiriwa na shitaka mahamakani la kum-baka mkewe wa ndoa.

Kisa chenyewe kiko hivi; mume na mkewe walikuwa chumbani katika burudani (michezo ya kikubwa) ya hapa na pale mume akashindwa kuvumilia mzuka umempanda na kutaka kumuingilia mkewe kimwili kufanya tendo la ndoa lakini mke akamkatalia mumewe kuwa hajisikii kufanya tendo la ndoa. Mume baada ya kukataliwa na mkewe basi akaamua kumlazimisha mkewe na kumuingilia kwa nguvu. Na mke huyo asema mumewe kazidi kwani karibu miaka miwili sasa mumewe anakuwa anam-baka. Kesi kama hizi zimekuwepo kila wakati nchini Uingereza na waume mara nyingi kuhukumiwa kwa kubaka wake zao.

 

Haya kwa wadau wa Tulonge naomba kusikia toka kwenu....... Je, huu ni ubakaji????

 

Views: 1558

Reply to This

Replies to This Discussion

Alalalalaala! Ni kosa kubwa mno kitendo hicho kukisifu kwa sifa hiyo ya ubakaji.Huyu ni mume wake na huyu ni mke wake,kwa vyovyote vile tendo la ndoa litakavyofanyika (hata kwangumi) baina ya wanandoa , huwezi kulisifu kwa sifa hiyo  ya ubakaji.

Ubakaji hauwi kwa watu waliokuwa na uhusiano wa kindoa,bali ikiwa uhusiano wa kindoa haupo,basi kitendo hicho akikifanya kitaitwa ubakaji.

Hilo mosi,pili,mume ana haki zake katika ndoa,na mke ana haki zake katika ndoa.Miongoni mwa haki za mume katika ndoa kutoka kwa mkewe ni mke kumtimizia mumewe kila atakapomuhitajia (kimapenzi).Kwa maana kwamba mke hutakiwi kisheria kumkatalia mumeo pindi atakapotaka chakula cha usiku.Ukikataa kumtimizia mumeo alichokitaka,basi jua kwamba unamkasirisha sana Mungu wako kwa kuikalia kinyume na haki haki ya mumeo.

Sheria inayotizama masuala ya ndoa inasema:Mke inabidi aijitoe mzima mzima kwa mumeo,kwa maana kwamba aitoe huduma hiyo kwa mumewe mzima mzima pasina kipingamizi chochote.

Na miongoni mwa haki za mke kutoka kwa mumewe,ni mume kuhakikisha anatimiza kile kitu tunachokiita kwa kimombo: (Alimony), yaani masuala yanayohusiana na mtunzo ya mke,kama vile kumnunulia mavazi,matibabu,chakula,na vitu kama hivyo.Hilo ni jukumu la mume,hivyo Mume: He must spend on his wife.

Ikiwa mume hakutekeleza haki hiyo kwa mkewe,basi nae atakuwa anamkosema Mola wake na kumkasirisha sana,kwa kule kutoitimiza haki na kuifikisha kwa mwenye nayo ambaye ni mkewe.Na ikitokea mume akapuuzia haki ya mkewe basi hapo mke nae anaweza kuipuuzia haki ya mumewe,kama vile kutia kufulia maeneo muhimu mpaka pale mume nae atakapoamua kumjali.Lakini ikiwa mume anaitekeleza inavyotakiwa  haki yake mkewe,basi ni kosa kubwa kwa mkewe kutia kufulia,na akifanya hivyo, basi mke huyo kuwa kafanya dhambi kubw ambele za Mungu,na  ataulizwa na Mola wake kwanini aliikanyaga haki ya mumewe???!!!.


Naomba kuishaia hapa.

Hahahahahaaa ngoja nicheke kwanza halafu nitarudi, hiyo kesi ikiisha huyo mwanamke abebe kilicho chake arudi kwao.

Nitarudi tena kuchangia.

Huko ni kutafutiana sababu.. yani wamecheza ilemichezo.. hamu imekuja alafu anasema hajisikii ? NGOJA NA MIMI NITATUDI... hah ahahahahaaaa

haaaaaaaaaaaaa!!!  HEEEE SASA ANACHEZA HALAFU ANAFIKA GOLINI ANAGOMA KUFUNGA, ?  HAYA BABA NAYE AMWISHITAKI KWA KOSA LA KUCHEZA NA HISIA ZAKE.

Andiko linasema utaachana na wazazi wako utafuatana na Mume,Mke wako pia mtakuwa mwili mmoja sasa iweje? mwili huu mmoja viungo vinabaguana? pia mwanamke hana umiliki wa mwili wake isipokuwa nai wa mumewe na mume umiliki wa mwili wake ni wa mkewe pia katika ndoa wameahidiana kupeana bila kikomo na ni dhambi kunyimana neta kubwa sana sema mahakama haziendi na amri za MUNGU ndiomana zanzibar kuna mahakama za kaadhi hizi zinafuata maandiko

ila nilichokiona hapa hakuna mapenzi kama kweli mapenzi yangekuwepo yasingetokea haya pia me ningemshauri baba kama kaona be mkubwa kagoma angemuacha aende kutafuta nyumba ndogo ajiburudishe tena angetoka muda huohuo aliponyimwa angevaa shati na kutokomea kusikojulika na ukija humgusi mikausho mikali

mhhh nimecheka lakini si kumdharau huyu mama ila ni jinsi gani alivo mpumbavu, unajua kumnyima mumeo tendo la ndoa unapunguza baraka ndani ya familia. ingekuwa huyu mwanaume hamuombi tendo akifika yeye anapanda tuu lol hapo ingekuwa case lakini anamuomba na yeye anajisikia sifa anamkatalia wakati kuna wengine hawaombwi mpaka wewe mwanamke ujisogezesogeze weeeee ndo mwanaume ageuke, huo wala si ubakaji na huyo mwanaume lazima hiyo case atashinda labda asijue kuongea. yani  i wish ningekuwa huyo mwanaume kitendo cha hukumu kutoka ni virago vyake mimi na yeye basi tena.

Ngoja nitarudi baadaye kidogo kuchangia. ngoja kwanza nikapate glass ya Konyagi pale the Bucket, maana nipo ndani ya Arusha.

Mmmmmmmh Makubwa, mambo ya chumbani huwa yana mipaka yake ya chumbani humo humo na si nje ya hapo, kweli mnaweza pishana situ kwa tendo la ndoa, kwa mambo mengi tu mkiwa humo ndani, ila mwisho wa yote nyie wawili ndo wakusettle sio watu wa nje, ukiona mwenzako amekukosea na hana mood nzuri yanini malumbano? si wako? subiri atakuwa sawa tu hata km sio siku hiyo hiyo then mnaelezana kinagaubaga, ila mmmmh kumshitaki mume kwa tendo la ndoa kuwa kakubaka? alitaka mumewe aende wapi sasa km sio kwake, akipata nyumba ndogo, oooh mume wangu hanipendi, si unamnyima? swala la msingi ni maandalizi ili kila mmoja awe tayari kwa tendo!

Halfu mimi mke wangu akininyimaaaaaaaaaaaa!!!!.

Ha haaa... mbona yaelekea hujamalizia sentence yako?


Chalii_a.k.a_ILYA said:

Halfu mimi mke wangu akininyimaaaaaaaaaaaa!!!!.

Ukisikia ukichaa wa wanawake wa kiingereza ndio uhuu wakuburuzana hadi kwa Pilato baada ya kuanza uchokozi. Halafu cha kushangaza unakuta wanawake huwa wanashinda case kwenye mahakama za waingereza. Hivi hii kweli ndio Women's Right(s) au ndio ku-abuse Women's Right(s)? 

Vijana baadhi weusi wenye tabia nzuri kuheshimu ndoa zao wanaooa wanawake wazungu baada ya muda utaona wanaanza kulalamika kuhusu wake zao, mke ndio wenye maamuzi hivyo mume ukimlazimisha mkeo basi unajikuta umepelekwa kwa Pilato. 

Ndio nakubali iwapo unaumwa au una tatizo hujisikii na kumwambia baba Chanja mapema lazima atakuelewa, na hata siku moja hawezi kutumia nguvu sababu mtu anayekupenda kweli atakuvumilia ingawa sio siku zote uwe unatafuta sababu.

hahahahahah mama umenichekesha Baba chanja!, halafu mama kwenye kuandika kiswahili unamshinda hata mr tulonge ila kuongea live dah! tulonge anakuacha njiapand maana tulonge anaongea kiswahili cha keko magurumbasi,mwanga lol weee hapo huambui kitu.

 

Reply to Discussion

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*