Tulonge

Nani awatoze kodi wakina dada wanaojiuza gizani? Na hoji ile ni biashara halali au haramu? Km haramu mbona maeneo yao ya kazi yanafahamika wazi na hakuna hatua zozote za kisheria zinazo chukuliwa!! Basi nani awatoze kodi???

Views: 759

Reply to This

Replies to This Discussion

Hahahhahaa kodi tena, ngoja nitarudi kutoa maoni
haiwezekani kulipa  kodi kwa sababu hiko kinyume na haki za binadamu

ok!!!! sasa km ni kinyume na haki za binadam kwann ha2a za kisheria hazchukuliwi dhid yao.......???????

Kaka rudi mchango wako ni muhim.......

Tulonge said:
Hahahhahaa kodi tena, ngoja nitarudi kutoa maoni
huwezi kuchukua hatua  za kisheria wakati huna ushaidi wa kumtia hatiani,kwamba alikuwa akijiuza.Hanaweza kukushinda kwa hoja mfano anaweza kukuuliza una ushaidi wa kunikuta najiuza? wewe utasema ndio nimekukuta barabarani maeneo ya mwembe jini kinondoni,ucku mkiwa kikundi huku mmesimama na wanaume,Yeye atasema kuna sheria inayookataza mwanamke hasisimame na wanaume ucku.Huu ni moja tu ya mifano .vilevile hata ukitumia shrria ya uzururaji bado unaleta utata wa hoja,mzururaji ni yupi na unamtambuaje .hapa tunahita kukaa na wanasheria wetu ili kutazama kwa umakini sheria hasa ya kuwafanya wasifanye  shughuli hizo
yes! Dats hot!! Wanasheria wanatakiwa wakune vichwa!@jemedari.
Ni kweli wanasheria pmj na wadau wa haki za binadamu wanahitaji  waangalie kwa umakini zaidi hizi sheria ndogondogo zinazowagusa janii yetu ili waweze kutoa haki bila ya upendeleo aukukandamiza tabaka  fulani

Kutokana na matatizo (maradhi) yaliyopo katika jamii yetu ya Tanzania na Africa kwa ujumla hii biashara ya wadada kujiuza haipaswi kuhalalishwa.

Hata kama ikihalalishwa Tanzania na wadada hao kutafutiwa maeneo maalum ajili ya kazi yao na kulipa kodi kama wafanyavyo wenzao wa pale Amsterdam (Redlight District) nchini Uholanzi, bado haitawasaidia dada zetu wa kitanzania wanaojiuza kuwaweka katika mazingira mazuri kiafya, kiusalama na kiuchumi. Nasemea hivyo sababu Tanzania bado tuna mfumo dume kama nchi nyingi za Africa. Nilikwenda kikazi kusini mwa Africa miezi miwili na nusu iliyopita, wadada wanaojiuza ndio wanaoongoza kwa kuathirika na AIDS, kupigwa na wateja wao (wanaume) wababe wasiotaka kuwalipa na kujeruhiwa vibaya na wengine kuuawa wakiwa kazini (wanajiuza).

Tanzania na Africa kwa ujumla hatuna sheria kali juu ya maambukizi ya AIDS. Hapa Britain na nchi zote za north Europe & Scandinavia kuna sheria iwapo mtu ni HIV+ katembea/kalala na mtu bila ya kumwambia status yake (HIV+) ni kosa na mahakama ina uwezo wa kumtupa jela. Na pia iwapo mtu anajulikana ni HIV+ bado analala au kufanya mapenzi na watu ambao hana uhusiano nao ki-ndoa vile vile ana kosa la kueneza AIDS na anachukuliwa hatua kali.

Ahsante sana Mama malaika, kimsingi nakerwa sana na hawa akina dada bila kusahau wateja wao kwan nihatar sana na cjui 2nalipeleka wap taifa le2, viongoz wa serikali ye2 wanashndwa kuchukua ha2a za lazima ktk hili inasemekana 7bu ni kwamba hata wao ni waumin(wateja) wazuri kwa akina dada hao, mara nying nalifananisha suala hili na issue ya madawa ya kulevya kwan viongozi we2 ndio wafanya biashara wakubwa hakuna waku wazuia!! 2nahtaji kufunga na kuliombea taifa le2 linaangamia.
kweli kabisa kaka Jemedali, taifa le2 linaangamia!

Ujue haya mambo ya kujiuza (au niseme UFISADI WA MWILI) kwetu sisi ni irrational na hayakuweko kwenye jamii yetu ya Tanzania, hata kama ni kazi yampatia kipato kwa nini dada anaye randa randa usiku kujiuza asifanye biashara/shughuli nyingine kujipatia kipato kuliko kujiweka kwenye kazi yenye hatari kama hiyo? Mbona kuna kina dada/mama wengi tu wanafanya biashara ya kupika chakula, kuuza mkaa, kuparua samaki pale feli, etc. AIDS inafagia kweli kweli sub sahara Africa na hicho ndio kimepelekea kuwa na Watoto Yatima wengi sana. Nakumbuka miaka ya 1970s kitu mtoto Yatima kilikuwa nadra sana na wala sikuwahi kuwa na ndugu Yatima wakati huo kwani Yatima kipindi hicho walikuwa kwenye familia chache sana na wengi walilewa na masista kwenye mission/makanisa au na ndugu. Sasa Yatima wako kila kona ya Tanzania, na karibu kila familia ina watoto Yatima.

 

 Nimesikia kuwa wadada hao wanaojiuza usiku wengine ni wasomi tosha na wana kazi nzuri, na wengi wana watoto wanawaacha majumbani usiku wamelala. Sijui ndio tamaa  ya kutaka vingi (materialism) inawapelekea kufikia hatua hiyo maana wakuta msichana mdogo aendesha gari ukiangalia mshahara anaopata na kazi aliyonayo havitoshi kumuwezesha kununua gari au kununua fanicha za kifahari ndani ya nyumba yake.

Iwapo viongozi nao ni waumini (wateja) wa hawa wadada basi kwa hakika miaka 10 ijayo nchi yetu itaendeshwa na viongozi walio maana nasikia huko Dodoma kipindi cha mikutano ya Bunge la Jamhuri huwa kunatia kinyaa, viongozi wanakuwa kama mahayawani vile walioachiwa Hospital na kupewa uhuru wa kufanya majambo.

kweli kabisa Mama, tatizo wadada hawaridhki yaan wamejaa tamaa! Yaan inasikitsha sana kwan weng wao wanajitambua na wanajua madhara yake! Wanavyuo weng, huko bungen ndio kabisaaa! eeh Mungu okoa taifa hili... Cjui kizaz cha kesho kitakuaje?

Reply to Discussion

RSS

© 2019   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*