Tulonge

WASTAAFU WA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI WAFUNGA BARABARA YA KIVUKONI KUDAI CHAO

Kwa mara nyingine tena wastaafu wa jumuia ya Africa Mashariki watanda mbele ya Mahakama ya Kisutu kuendeleza mchakato wa madai yao. Tukio hili limeibuka baada ya kuendelea kupigwa danadana juu ya malipo yao
ambapo awamu ya kwanza walipewa kiasi kidogo tu ya malipo yao yote.


 Wakili Semgalawe akijaribu kuwaelewesha wadai juu ya taratibu zinavyoendelea.
Akizungumza kwa uchungu sana mmoja wa wahanga hao alisema wamekuwa wakifanywa kama watoto wasio na akili. Kinachowashangaza zaidi ni kujitoa kwa Jaji wa kesi yao
wakati muafaka wa malipo yao haujafikiwa.Wanahisi hakuna dalili za kupata
malipo yao ndiyo maana hata Jaji wa kesi yao ameamua kujitoa.Katika kuhakikisha wanapata majibu sahihi, walimuhitaji wakili wao Bw. Semgalawe afuatilie nini kinaendelea na awaletee majibu. Baada ya kufuatilia wakili huyo alirudi na jibu la kuendelea kushughulikiwa kwa suala
lao hadi kesho kutwa (Ijumaa) ndipo watapewa jibu la uhakika. Maelezo hayo
yalipelekea kelele kuzuka wakiamini ni jibu la kuwaridhisha ili waondoke, baadhi
wakiteta kuwa ameshapewa rushwa ili awe upande wa serikali. Ndipo mdai mmoja
alipoinuka na kusema “Na sisi tutaendelea kusubiri hapa hapa barabarani hadi
hiyo Ijumaa”.
Kauli hii iliwafanya wadai wenzake kumshangilia kwa nguvu zote
kuonesha kwamba wamekubaliana na wazo lake.Tulonge ilipotaka kujua kuhusu ushirikiano wa wadai hao juu ya kufuatilia suala la madai, walisem wao hukutana mtaa wa Keko hapa Dar es salaam kila alhamisi ili kujadili kuhusu madai ya fedha zao. Hivyo wana ushirikiano wa
karibu na serikali itegemee jambo kama hili
kuendelea kila mara endapo hawatapata fedha zao zote.

 


Wadai hao wamekufunga bara bara hiyo kuanzia saa 5 asubuhi leo. Hadi tulonge inaondoka eneo la tukio saa 10 jioni hakukuwa na muafaka juu ya suala hili. Iliacha wadai hao wakiwa wanalalamikia suala hili huku wakiendelea
kukaa katikati ya barabara.


Wadai wakionekana kupinga baada ya kuambiwa muafaka wa malipo yao hadi Ijumaa.

 

Views: 523

Reply to This

Replies to This Discussion

Kwa hili la wastaafu JK itabidi aidhinishe mkwanja kutoka hazina ili walipwe kwa sababu;
kwanza wameshinda kesi mpaka yule 'chief jaji' kujitoa inaonesha jinsi gani wastaafu walivyokuwa 'the right side'
Lakini pia kwa upande mwingine wa shilingi, huu ni wakati wa mwisho wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wanasema lala salama naamini serikali haitataka kutia dosari mwishoni itawalipa fedha zao. Lakini ikisema sizitaki mbichi hizi kama ilivyosema kwa walimu mwanzoni mwa mgogoro wao..........!!
............maoni... hebu tumrudishe jk na serikali yake sio tu amalizie muda wake bali amalizie ahadi alizoahidi 2005
wakati anaingia madarakani.

......................................CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEE........................................
kwa hili wastaafu wanahaki ya kila sababu ya kudai chao kwa sababu wanashibishana mafisadi wakati waliojenga nchi awadhaminiwi ..........inamaana mheshimiwa akuliona hili kama vipi wakomae hapohapo wasikubali kudanganjwa mpaka kieleweke
Upo sawa Kadiri,moja ya sababu ambazo hupelekea majaji kujitoa katika ni kuona kuna uwezekano wa haki kutokutendeka,hivyo hujitoa ili uepusha matatizo upande wake.
Beyond words.. ina maana hawa wa staafu hadi leo hawajalipwa mafao yao???????? Viongozi Tanzania wanafanya nini jamani? Hawa wadai naamini wengi wao wameshafariki kufikia leo maana EAC ilivunjika zamani sana. Pesa wanayodai siajabu ni ndogo mno kulinganisha na pesa inayotumiwa na familia ya raisi Kakwete (mkewe na mwanae) kuzurula mikoani eti ajili ya campaign wakati hawa wastaafu ni moja ya hao wananchi wanaoenda kuwaona ambao raisi anahitaji kura zao ili arudi Ikulu.
Kafie mbele na CCM yako!!! WEZI WATUPU......

kadir msuya said:
Kwa hili la wastaafu JK itabidi aidhinishe mkwanja kutoka hazina ili walipwe kwa sababu;
kwanza wameshinda kesi mpaka yule 'chief jaji' kujitoa inaonesha jinsi gani wastaafu walivyokuwa 'the right side'
Lakini pia kwa upande mwingine wa shilingi, huu ni wakati wa mwisho wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wanasema lala salama naamini serikali haitataka kutia dosari mwishoni itawalipa fedha zao. Lakini ikisema sizitaki mbichi hizi kama ilivyosema kwa walimu mwanzoni mwa mgogoro wao..........!!
............maoni... hebu tumrudishe jk na serikali yake sio tu amalizie muda wake bali amalizie ahadi alizoahidi 2005
wakati anaingia madarakani.

......................................CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEE........................................

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*