Kwa mara nyingine tena wastaafu wa jumuia ya Africa Mashariki watanda mbele ya Mahakama ya Kisutu kuendeleza mchakato wa madai yao. Tukio hili limeibuka baada ya kuendelea kupigwa danadana juu ya malipo yao
ambapo awamu ya kwanza walipewa kiasi kidogo tu ya malipo yao yote.
Wakili Semgalawe akijaribu kuwaelewesha wadai juu ya taratibu zinavyoendelea.
Akizungumza kwa uchungu sana mmoja wa wahanga hao alisema wamekuwa wakifanywa kama watoto wasio na akili. Kinachowashangaza zaidi ni kujitoa kwa Jaji wa kesi yao
wakati muafaka wa malipo yao haujafikiwa.Wanahisi hakuna dalili za kupata
malipo yao ndiyo maana hata Jaji wa kesi yao ameamua kujitoa.
Katika kuhakikisha wanapata majibu sahihi, walimuhitaji wakili wao Bw. Semgalawe afuatilie nini kinaendelea na awaletee majibu. Baada ya kufuatilia wakili huyo alirudi na jibu la kuendelea kushughulikiwa kwa suala
lao hadi kesho kutwa (Ijumaa) ndipo watapewa jibu la uhakika. Maelezo hayo
yalipelekea kelele kuzuka wakiamini ni jibu la kuwaridhisha ili waondoke, baadhi
wakiteta kuwa ameshapewa rushwa ili awe upande wa serikali. Ndipo mdai mmoja
alipoinuka na kusema “Na sisi tutaendelea kusubiri hapa hapa barabarani hadi
hiyo Ijumaa”. Kauli hii iliwafanya wadai wenzake kumshangilia kwa nguvu zote
kuonesha kwamba wamekubaliana na wazo lake.
Tulonge ilipotaka kujua kuhusu ushirikiano wa wadai hao juu ya kufuatilia suala la madai, walisem wao hukutana mtaa wa Keko hapa Dar es salaam kila alhamisi ili kujadili kuhusu madai ya fedha zao. Hivyo wana ushirikiano wa
karibu na serikali itegemee jambo kama hili
kuendelea kila mara endapo hawatapata fedha zao zote.
Wadai hao wamekufunga bara bara hiyo kuanzia saa 5 asubuhi leo. Hadi tulonge inaondoka eneo la tukio saa 10 jioni hakukuwa na muafaka juu ya suala hili. Iliacha wadai hao wakiwa wanalalamikia suala hili huku wakiendelea
kukaa katikati ya barabara.
Tags:
Kwa hili la wastaafu JK itabidi aidhinishe mkwanja kutoka hazina ili walipwe kwa sababu;
kwanza wameshinda kesi mpaka yule 'chief jaji' kujitoa inaonesha jinsi gani wastaafu walivyokuwa 'the right side'
Lakini pia kwa upande mwingine wa shilingi, huu ni wakati wa mwisho wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wanasema lala salama naamini serikali haitataka kutia dosari mwishoni itawalipa fedha zao. Lakini ikisema sizitaki mbichi hizi kama ilivyosema kwa walimu mwanzoni mwa mgogoro wao..........!!
............maoni... hebu tumrudishe jk na serikali yake sio tu amalizie muda wake bali amalizie ahadi alizoahidi 2005
wakati anaingia madarakani.
......................................CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEE........................................
© 2022 Created by Tulonge.
Powered by