Tulonge

Waswahili na Kiswahili msaada tafadhali!!!!!!

Naomba tafsiri ya sentensi hiiii katika kiswahili


"finish eating, and then I shall  eat you"

Views: 1367

Reply to This

Replies to This Discussion

Mkuu tulonge@,

Sentensi hiyo ni sahihi kabisa:utakapo sema Maliza kula,kisha nitakula wewe,yaani uko right na maanainaeleweka.Lakini utakapoweka neno mimi,ukasema: (Kisha nitakula wewe) haina maana hilo neno haliongezi chochote katika sentensi,ndio maana ni ile ile ukitizama lakini ukitizama kiundani zaidi utakuta neno mimi linaongeza msisitizo au linathibitisha zaidi sentensi yako,kwa hiyo inakuwa ni sentensi iliyokuwa Confirmed  zaidi kiasi kwamnba anayesikia sentensi hiyo atajua kwamba mtu yuko amemaanisha alichokizungumza na hatanii atafanya kweli.

Katika kiswahili wenyewe wanasema kurudia maneo kama vile sisi,mimi,wenyewe...katika sentensi,huwa ni kwa ajili ya kusistiza na kuthibitisha zaidi unachokizungumza.

Na ndio maana utasikia watu  wanapoaga kuondoka wanasema:

Sisi tunatoka!! Hawasemi tunatoka!.

Sisi hatujambo!

Wenyewe hawapo!, Mimi sijamuona!,Mimi sijala chakula!. Kisha wewe utakuja nyumbani!..........

Kwa ufupi,maneno hayo kuyaweka au kuyarudia kwenye sentensi yako kuna faida yake tena kubwa,hayatakuwepo  katika sentensi hivi hivi tu sawa na kutokuwepo kwake,bali  yanaongeza umuhimu fulani hivi katika maana,na umuhimu huo ni kuconfirm na kuimarisha zaidi sentensi yako kimaana.

Nimekusoma mkuu, mimi nitaenda kukuombea kazi baraza la kiswahili teh teh teh

Chalii_a.k.a_ILYA said:

Mkuu tulonge@,

Sentensi hiyo ni sahihi kabisa:utakapo sema Maliza kula,kisha nitakula wewe,yaani uko right na maanainaeleweka.Lakini utakapoweka neno mimi,ukasema: (Kisha nitakula wewe) haina maana hilo neno haliongezi chochote katika sentensi,ndio maana ni ile ile ukitizama lakini ukitizama kiundani zaidi utakuta neno mimi linaongeza msisitizo au linathibitisha zaidi sentensi yako,kwa hiyo inakuwa ni sentensi iliyokuwa Confirmed  zaidi kiasi kwamnba anayesikia sentensi hiyo atajua kwamba mtu yuko amemaanisha alichokizungumza na hatanii atafanya kweli.

Katika kiswahili wenyewe wanasema kurudia maneo kama vile sisi,mimi,wenyewe...katika sentensi,huwa ni kwa ajili ya kusistiza na kuthibitisha zaidi unachokizungumza.

Na ndio maana utasikia watu  wanapoaga kuondoka wanasema:

Sisi tunatoka!! Hawasemi tunatoka!.

Sisi hatujambo!

Wenyewe hawapo!, Mimi sijamuona!,Mimi sijala chakula!. Kisha wewe utakuja nyumbani!..........

Kwa ufupi,maneno hayo kuyaweka au kuyarudia kwenye sentensi yako kuna faida yake tena kubwa,hayatakuwepo  katika sentensi hivi hivi tu sawa na kutokuwepo kwake,bali  yanaongeza umuhimu fulani hivi katika maana,na umuhimu huo ni kuconfirm na kuimarisha zaidi sentensi yako kimaana.

Mh Mbona Hiyo Sentensi Mimi Siielewi!! Inakuaje Huyu Amkule mwenzie baada ya kumaliza kula

kweli hapa ngoma nzito mkuu ILYA sasa mbona upatanisho wa kisarufi unakataa! sijawahi kusikia mtu akisema hivyo.

Chalii_a.k.a_ILYA said:

E bwana eee,kumbe mtaa huu kuna kamjadala poa,nilikuwa sijachungulia sehemu hii,na sasa ni wakati wa kudondosha jibu kama ifuatavyo:

Finish Eating: Maliza kula

And then I shall eat you: Kisha mimi nitakula wewe.

Maliza kula,kisha mimi nitakula wewe!.

Hicho nadhani ndio kiswahili chake,hata ukiwauliza akina shigongo lazima nao waanguke kwenye jibu kama hilo.

Hapa nimegundua kinacho leta utata na kuonekana sentensi haijakaa kisarufi zaidi ni hako kaneno wewe mwisho wa sentensi yetu (Maliza kula,kisha mimi nitakula wewe!.), lakini ukweli nikwamba  lazima useme hivyo kama ilivyo(nitakula wewe).Ukithink twice sentensi hii: (nitakula wewe) inaonekana kama vile sentensi imeyumba yumba kwa kiasi fulani hivi,lakini hebu tuondoe tu hako kaneno wewe ,then tuweke neno (Embe) badala ya wewe,huoni sentensi inajipa!,hivyo hapo kinachoweza kuleta utata  ni neno wewe mwisho wa sentensi hiyo,na sababu kuu hasa ya hilo ni kwa kuwa sentensi kama hiyo hatuitumii sana katika maisha yetu ya kila siku kama vile tunavyotumia maneno/sentensi kama vile: Kula embe, kula tunda, kula nyama....ama  sentensi kama vile : Kula wewe !!!! ni nadra sana kuisikia sentensi kama hii vinywani mwa watu kutokana na kwamba mtu kuliwa ni kwa nadra sana,na hilo huweza kuchangia kuleta utata katika sentensi kama hiyo na kuonekana imeyumba,lakini tuchukulie wewe ni tunda miongoni mwa matunda,kama   Apple (tufaha) mfano,kisha sehemu ya wewe tuweke hilo Tufaha,hapo sentensi itakaa sawa na kutenga maa!.

Hahahah Mkuu Tulonge@,tena ukifanya hivyo utakuwa umefanya kitu cha mbolea sana na muhimu ,maana ninausongo na hilo baraza la kiswahili,we acha tu!

ngoja nidondoke na kibo alone, maliza kula kisha nikukule.

Hahahahaaaaaa nikukule tena? Manka hiko ni kichaga nn?

manka said:

ngoja nidondoke na kibo alone, maliza kula kisha nikukule.

Kila nikijaribu kuchambua tafsiri mbalimbali kama vile

1-Maliza kula, kisha mimi nitakula wewe

2-maliza kula, kisha mimi nikukule wewe

3-maliza kula, kisha mimi nikule wewe

nadhani wote tunakubaliana kuwa hii tafsiri haileti maana katika kiswahili, nadhani kauli ya mtu(kiumbe hai) kumtendea mtu mwingine au kiumbe kingine kitendo cha kumla katika wakati uliopo na unaoendelea haipo katika kiswahili, sijui ni kwanini na ndo maana nimeomba msaada.

Nimeumiza kichwa changu sana katika kufikiri lakini sijapata jibu. Ila nikijaribu kuangalia nyakati zingine kama ifuatavyo naona kuna kiswahili cha tafsiri hii,

Mfano:-

1- Alipomaliza kula naye aliliwa. (wakati uliopita timilifu)

2-maliza kula, kisha uliwe na mimi (wakati uliopo na ujao tegemezi)

3-Umalizapo kula,utaliwa na mimi (wakati ujao tegemezi)

Hitimisho

Ni vigumu kutafsiri neno kwa neno toka lugha moja kwenda lugha nyingine kwa kuwa miundo ya lugha hutofautina. hivyo kinachotakiwa ni maana ipatikane na siyo uwiano wa neno kwa neno.

mimi hapa ningetafsiri hii sentensi kama hivi.

 

maliza kula, kisha uliwe na mimi ( wakati uliopo na ujao- tegemezi )

 

Kama hukubaliani na mimi bisha kwa hoja.

 

 Kaka Don M@ mi nadhani ukitafsiri sentensi hiyo namna hiyo kama ulivyosema: (maliza kula, kisha uliwe na mimi), utakuwa umekwenda kinyume kabisa na muundo wa sentensi hiyo ya kimombo hapo juu kwenye mada,inayosema:"finish eating, and then I shall  eat you"

Tafsiri yako ingawa inapanata na sentensi hii nyekundu "kimaana" lakini haipatani nayo "kimuundo".Mi nadhani tafsiri yako inapatana na sentensi hii ya Bluu ifuatayo "kimaana na kimuundo":

"Finish eating, and then be eaten by me".

Hivyo tafsiri sahihi kwa mtazamo wangu inayoendana sawia na sentensi yetu kwenye mada ni hii inayosema hivi:

"Maliza kula  ,          kisha mimi nitakula wewe".
(Wakati uliopo)              (Wakati ujao)

Na neno linaloonyesha wakati ujao katika sentensi hii ya pili ni neno (ta),hivyo sentesni hii:Kisha mimi nitakula wewe,inajitosheleza kuelezea kuwa inakusudia wakati ujao.Kama ambavyo (na) hujulisha wakati uliopo,mfano: (Ninakula).

Halafu,si sahihi
kwamba kauli ya mtu (kiumbe hai) kumtendea mtu mwingine au kiumbe kingine kitendo cha kumla katika wakati uliopo na unaoendelea haipo katika kiswahili !!.

Sentesni kama hizo zipo Mfano: Mimi ninakula wewe. (I'm eating you ).Hii ni sentensi ya mtu kumtendea mtu mwingine katika wakati uliopo,maana yake inaeleweka na ipo katika Lugha ya kiswahili.Kauli tunayoweza kuisema ni hii kwamba:Baadhi ya sentensi kama hizi , zinapopatikana basi moja kwa moja zinachukua ile sura  ya jamii ya sentensi ambazo miundo yake huwa na utata,na  zipo kibao katika lugha ya kiswahili.

Na kinacholeta utata (kimaana) katika sentensi yetu (kwa mujibu wa tafsiri yetu) ni huyo mtendewa (wewe), utata huo unakuja kutokana na kwamba haijazoeleka kwa walio wengi au katika jamii kusikia mtu akiliwa na ndio maana kuna u-strange fulani hivi katika sentensi kwa anayeisikia.

Lakini kwa watu wenye tabia ya kula watu wengine ,mfano mzuri (vampires) hawaoni ustrange wowote kwenye sentesi kama hiyo,kwao ni sawa na kusema (Nitakula embe) !!.Hivyo sentensi haina makosa kisarufi,iko sawa na inaendana kimaana na kimuiundo na sentesi yetu isemayo:

"finish eating, and then I shall  eat you"

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*