Siku moja kwenye daladala mtoto wa nursery akiwa ndani ya daladala akaanza kuimba hivi "
Kama baba angezaliwa Jogoo na Mama Kuku mimi ningekuwa kifaranga.
Kama baba angezaliwa Ng'ombe dume na mama jike mie ningekuwa ndama.
Kama baba angekuwa nguruwe na mama nguruwe nami ningelikuwa nguruwe.
Konda akaona huu uzushi akamwambia we dogo mbona unatuzingua na huo wimbo wako je baba yako angekuwa MLEVI na mama yako MALAYA ungekuwa nani?
Mtoto akajibu ningekuwa "KONDA" kama wewe watu wote wakavunjika mbavu kwa vicheko
Tags:
Hahahahaahahaaa konda alitaka kujifanya kujua,akakutana na mjuaji zaidi yake. Ina maana Baba wa huyo konda ni mlevi na mama yake ni malaya teh teh teh safi sana dogo.
Hahahahahah....duh hiyo tamu....huyo konda agekuwa Magufuli angempandishia dogo nauli ya Daladala tehtehteh!!
Hah ahhaa haa......safi sana hii nimependa, pia imeniongezea siku za kuishi maana nimecheka sana.....hasa kwa hao makonda huwa wanajifanya wajuaji sana, sasa aipatikana.
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by