Tulonge

Hebu niwaulize watu wazima na vijana .WIVU ni nini ?

Jee,TUNAUWEKA katika nafasi gani ndani ya mapenzi ya watu.Ni haki mume kulilia wivu mkewe au kinyume chake.Inakuwaje ,basi kuonekana mkorofi bwana anapokuwa na wivu kwa mke.

HEBU leteni fikra kwa uoni wenu.

Kwaheri....

Views: 632

Reply to This

Replies to This Discussion

Wivu ni dalili ya kumpenda zaidi mwenzi wako. Kama wewe ni muaminifu na unamjali mpenzi wako, lazima utakuwa na wivu juu yake. Kinachotakiwa huo wivu usiupe nafasi saaaaaana hadi ukapitiliza, hapo utakuwa unaharibu sasa.

Kama wewe humpendi na siyo muaminifu kwa mpenzi wako, hauta muonea wivu hata kidogo hata ukimkuta anazini na mtu mwingine.

Kwa kifupi ktk mapenzi wivu lazima uwepo na nimoja la ishara ya kupendana ila usizidi sana.

kwanza wivu ni sunna pili wivu nikuonyesha kuwa unampenda kwa dhat na hutaki kumegewa 3 kitu wivu kimeumbwa na Mungu yaani sio k2 cha kuigiza kipo ndani ya moyo wa m2 na wengine huuguwa kabisa kwa k2 wivu yaani wanakuwa wagonjwa kwa wivu.

 Sasa inakuwaje, BIBI kulalamika tabia ya wivu wa mume.Na huwa ile raha ya kuishi inakuwa mtihani.

 

Ama huseme Bibi -MAPENZI HAYAJUI au amezoea kuwa huru kama mnyama pori inakuwaje, asee !

 

Na wivu ni BIBI tu afanyiwe wivu - hakuna BIBI kufanya wivu kwa bwana.

Mbona binaadamu wa sasa hawaeleweki...

Tafadhali, ENDELEA

jamani jamani "wivu wivu"

wivu ni ugonjwa mbaya sana tena sana, watu wakipendana halafu ukaingiwa na wivu basi shughuli ipo

hakuna atakaye mwamini mwenzie, tena wanaume walio wengi  ndo wana wivu sana, mbaya omba usikutane na mwanaume ambaye anataka cmu yako wewe iwe yake namaanisha kuwa msg ikiingia asome yeye cmu ikipigwa weka loudspeaker nae asikie jamani unaweza ukampata mwanaume wa namna hiyo utalia na maisha yako kila cku yatakuwa ya mashaka jamani wivu ni kitu cha kawaida watu kuoneana! 

Marehemu bibi yangu siku zote alikuwa anambia "Wivu ni SUNA", na kuwa.... "Ni haki mume kulilia wivu mkewe, na pia mke kulilia wivu mumewe". Sikuelewa bibi mantiki yake hadi pindi nilipoolewa na mume wangu ndio nikaelewa bibi alikuwa ana maanaisha nini. Mume hata akupende vipi na kukuamini bado ka-wivu katakuwapo tu.

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*