Tulonge

Kachaguliwa meya mpya wa mji fulani. Ili atoe shukrani zake na kuonyesha umaarufu wake akaamua kwenye ukuta wa jengo la meya lililokuwa katikati ya mji ichorwe picha ya mbuni. Meya akataka apatikane fundi maarufu wa kuchora. Alipopatikana meya na fundi mchoraji wakakubaliana. Kabla ya kushikana mikono kupasisha dili yule mchoraji akamwambia meya 'mkuu nina swali la mwisho kabla sijaanza kazi' meya akajibu nena fundi. Fundi:-mkuu kuyo mbuni unayemtaka awe kafungwa au awe huru? Meya akang'aka eh afungwe tena? watu watanielewa vibaya. Basi fundi akatoa mamirangi na vikorobwezo akachora mbuni makini. Kisha akamwita meya akamwuliza vipi meya hapo unaonaje? meya akasema mswano kabisa. Fundi akabeba vifaa vyake na kuondoka. Usiku mvua kali ikanyesha. Asubuhi meya alipoenda kazini picha ya mbuni haikuwepo akakasirika sana na kumwita fundi ajibu maswala na arejeshe pesa aliyolipwa. Fundi alipofika na kung'akiwa na meya fundi akanyanyua kichwa na kumjibu meya: - mkuu mbuni alikuwa huru ametoweka.

Views: 562

Replies to This Discussion

Teh teh teh teh, ina maana angefungwa asinge toweka

ha ha ha ah huyo fundi tapeli kweli.....teh teh teh teh....meya hapo lazima ajione mjinga

Hahahahahah! watu kama hawa adhabu yake ni kukata vidole vyote wasiweze kuchora tena...lol

fundi si alitumia rangi za maji kumchora mbuni.angetumia rangi zinazohimili maji mbuni asingekimbia. meya anapenda dezo bei rahisi

aaaaah fundi tapeli huyu.

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*