Tulonge

Jamaa ni muhudumu wa Mortuary sasa anajitambulisha kwenye harusi, my name is Kamugisha am working with Muhimbili, infwact my profweshinally yangu nahudumia watu ambao madaktari wameshindwa kunusuru uhai wao. Na leo nimekuja na BMW lakini BENZI nimemuachia mama koku atakuja badaye...

Views: 1515

Replies to This Discussion

Hahahahahaaa hv ni kweli hawa jamaa wanapenda kujiweka juu sana?

Teheteheteheteeeeee, yaani hawa watani wangu bwana wanapenda saaaaana kujitoplize!! kuna mmoja tuko nae ofsn duh, akianza kujisifia mtalala mtaamka  hajamaliza, mpk mmoja mmoja anaondoka anabaki mwenyewe ndo ananyamaza ila mkiendelea kumsikiliza yaani jua litatoka mpk litazama bado anajisifia yeye na familia yake wakati ana maisha ya kawaida tu ya kubadilisha mboga! ila pia sio wote ila wengi wao ni type hizo za "leo nimekuja na BMW lakini BENZI nimemuachia mama koku atakuja baadaye..."

Ha haa haaa... Baba Koku chiboko, anikumbusha bwana mmoja jirani ya mama yangu mdogo. Huyo bwana ni mhaya.... apenda kujisifia sana kwa sana. Na hutaka muda wote kuongea english hata ukimjibu chiswahili mara zote bado aendelea na english utasema hakijui kazaliwa UK or US, nasikia hajawahi toka nje ya TZ na aliishia O-Level lakini alivyo na misifa na ukikutana naye njiani utafikiri ni muhishimiwa au tajiri fulani vile. Na kila wakati nasikia aazima magari. Hata Bill Gates mzungu wa watu tajiri akisimama na huyo mhaya waweza sema Bill Gates ni driver wa mhaya. Ha haa haaa.....

Hahahaaa.. Tupo juu hamta msemaje..  Hahahaa.. ndo yale yale ya "dont try me - eti usinijaribu mimi" mara utasikia "me and brother photocopy togeza - eti mimi na kaka yangu tunafanana" hahahaa..

Hahahahhahhahahaaa Dixon umenichekesha. Eti photocopy togeza

Dixon Kaishozi said:

Hahahaaa.. Tupo juu hamta msemaje..  Hahahaa.. ndo yale yale ya "dont try me - eti usinijaribu mimi" mara utasikia "me and brother photocopy togeza - eti mimi na kaka yangu tunafanana" hahahaa..

Ha haa haaa... kama ulikuwepo vile. Wanangu hawakuweza muelewa yule bwana, hasa Malaika hana subira kila sekunde alikuwa anamuuliza "what do you say? I can't understand you". Namvuta mkono lakini mtoto hasikii. Ha haa haa

Kumbe na wewe DIXON ni mhaya? Sikujua, samahani sana kwani mwakani nakuletea Malaika na Denzil huko Arusha. Ha haa haaaaa....

Itabidi siku moja nikatembelee Bukoba nijionee mwenyewe... maana umenivunja mbavu na ya "me and brother photocopy togeza.

Ha ha ha ha haaa.. Hii ndiyo tulonge bwana.. yani najaribu kukumbuka stori moja hivi , JUMA na KASIMU wame lala kitanda kimoja alafu KASIMU akawa anavuta Mto wa JUMA ;

Kwa msisitizo kuonyesha kingereza anakiweza basi Juma akawa ana muita "KASIMU"

you Ka-telefon .. ka-telefon  .. dont smoke my river... akimaananisha "we Kasimu kasimu .. usivute mto wangu"

Ha ha ha haaa

Hahahahah hata me nina rafikiangu 1 hao wakina Kamugisha nimchizi wangu kweli ananipigiaga cm nimpitie sehem naenda but kabla sijafika anawaambia watu alionao nimempigia cm deleva wangu anakuja kunichukuwa kweli muda c mrefu nafika kumchukuwa jamaa walikuwa wanamuamini sasa kuna siku nilipita halafu pale kuna mtu ananijuwa washkaji wakaanza kusema deleva wa Kamugisha  huyo kapita yule jamaa anaenijuwa akawapa mkanda wote washkaji walimptoa maana mchizi wangu. Dis anamjuwa na hapendi kukutana nae maana anamjuwa mambo yake ya kujikweza kama huna huna tu hata ufanyeje. ila ndivyo walivyo tuwachukulie kama walivyo huo ndio utofauti wa wanaadam TABIA.

Ha haa haa haa haaa.... DIXON waniua kwa kucheka. Ha haa haa haa haa haaa 

Dixon Kaishozi said:

Ha ha ha ha haaa.. Hii ndiyo tulonge bwana.. yani najaribu kukumbuka stori moja hivi , JUMA na KASIMU wame lala kitanda kimoja alafu KASIMU akawa anavuta Mto wa JUMA ;

Kwa msisitizo kuonyesha kingereza anakiweza basi Juma akawa ana muita "KASIMU"

you Ka-telefon .. ka-telefon  .. dont smoke my river... akimaananisha "we Kasimu kasimu .. usivute mto wangu"

Ha ha ha haaa

Huyo mchizi wako ni chiboko. Sasa alijisiaje baada ya kujua wewe umemgundua akuita driver wake? 

Omary said:

Hahahahah hata me nina rafikiangu 1 hao wakina Kamugisha nimchizi wangu kweli ananipigiaga cm nimpitie sehem naenda but kabla sijafika anawaambia watu alionao nimempigia cm deleva wangu anakuja kunichukuwa kweli muda c mrefu nafika kumchukuwa jamaa walikuwa wanamuamini sasa kuna siku nilipita halafu pale kuna mtu ananijuwa washkaji wakaanza kusema deleva wa Kamugisha  huyo kapita yule jamaa anaenijuwa akawapa mkanda wote washkaji walimptoa maana mchizi wangu. Dis anamjuwa na hapendi kukutana nae maana anamjuwa mambo yake ya kujikweza kama huna huna tu hata ufanyeje. ila ndivyo walivyo tuwachukulie kama walivyo huo ndio utofauti wa wanaadam TABIA.

yaani nilivyoambiwa kuwa nikimfuata mchizi naenda kama driver nilicheka kisha nikamuacha kama alivyo maana ndivyo walivyo utawafanyaje? na me sijamwambia kuwa ananifanya driver wake nimemuacha aridhike yeye ndivyo alivyo hawezi kubadilika.

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*