Tulonge

Na Vitusi Ngiliule

Hivi huyu dada atakua anaitwa nani? Nilijiuliza moyoni lakini cha kushangaza, hata kabla sijapaza sauti kumuuliza nilistaajabu kusikia akinijibu,”ooh..!najua unahitaji kunifahamu kwa jina,hilo lisikuumize kichwa, naitwa Idaya”. Mapigo yangu ya moyo yalizidi kunienda kasi nikimstaajabu huyu dada,jinsi alivyoweza kuyatambua mawazo yangu hata kabla ya kumwambia. Nilimjibu huku nikitetemeka,”Asante dada kwa kunifahamisha jina lako”, naye akaniitikia kwa kutikisa kichwa chake, kama ishara ya kukubaliana na nilichokisema. Niliangaza macho huku na huko kuwatazama abiria wengine, nikidhani ya kuwa wanafahamu kilichokua kikiendelea kati yangu mimi na yule dada, lakini abiria wote walionekana wako bize na mambo yao, hii ilionyesha dhahiri ya kuwa walikua hawafamu chochote.

Ndugu msomaji wangu najua utakua unajiuliza maswali mengi sana, labda kwa nini sikuchukua maamuzi ya kuhama hiyo siti. Hata mimi pia nilikua na hilo wazo la kuhama, lakini jambo la kushangaza nilikua mzito sana katika kufanya maamuzi hayo, hivyo nikabaki kama mtu ambaye haelewi cha kufanya.

Wakati yote hayo yakiendelea, basi lilikua linaingia maeneo ya chalinze, niliingiza mkono wangu mfukoni na kutoa ile simu aliyonikabidhi mama,ili nimjulishe kaka ya kuwa tumekaribia kufika, lakini jambo la kushangaza nilipojaribu kupiga ile namba ya kaka haikuweza kupatikana, kiukweli nilikua sijawahi kufika jiji la Dar. Ila nilikua nazifahamu baadhi ya sehemu kama vile chalinze, kibamba.., lakini kwa kuhadithiwa tu, hivyo sikuwa mwenyeji wa jiji hili. Nilijaribu tena kumpigia simu lakini hali ilikua ni ile ile tu. Wakati nikiwa bado nimeishikilia ile simu ghafla nikasikia,”Ondoa shaka Erick, wala hakijaharibika chochote kwa kuwa upo na mimi hata kama kaka yako hapatikani”,ilikua ni sauti ya yule dada akiongea huku akinitazama usoni. Nilihisi kama vile naota kwa yale yote yaliyokua yakiendelea mle ndani ya basi. “Aah ah ah.., hamna shida dada Hidaya”, nilimjibu huku nimeshikwa na kigugumizi. Alitabasamu halafu akaingiza mkono kwenye pochi yake na kutoa miwani mieusi kisha akaivaa. Wakati huu hakuzungumza chochote, lakini aliendelea kutabasamu huku akiegamia siti yake kwa kulaza kichwa chake.

Wakati yote haya yakiendelea ghafla nilipata wazo la kumpigia simu mtoto wa shangazi yangu,ambaye kwa kipindi hicho nilimuacha nyumbani Dodoma kwani alikuwa amekuja kumsalimu mama.Niliitafuta namba yake haraka kisha nikajaribu kumpigia, lakini nayo haikupatikana hivyo ilinibidi niwe mpole kama mtu aliyemwagiwa maji. Nilishusha pumzi kisha nikaegemea siti yangu.Ilikuwa inaelekea majira ya sita mchana wakati tunaiacha chalinze, abiria wote walikuwa kimya sana mle ndani ya basi kuashiria ya kuwa wamechoka kwa safari. Lakini wakati nikiwa nimetulia kwenye siti yangu ghafla nilihisi nimepewa kitu mfano wa pini, ilikua iking’aa sana na kuvutia.


Itaendelea jumatatu ijayo..

Views: 799

Replies to This Discussion

Naisbiria part 5 kwa hamu. naona kama j3 mbali sna

Yani kastori kakianza kunoga unakakatisha!!!! Haya bwana ngoja tuvute subra!!! teheee

teh teh Dixon endelea kufuatilia, j3 si mbali

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*