Tulonge

Na Vitus Ngiliule

Ilikua inaelekea majira ya saa nne asubuhi, kwa muda huu tulikua tunaingia morogoro na mara tu baada ya kuwasili tuliingia moja kwa moja katika kituo cha mabasi ya shabiby. Watu wengi walitelemka kwa ajili ya kuchimba dawa (kujisaidia haja ndogo) pamoja na kula chakula pia. Tulipewa muda wa kama dakika kumi na tano tu kufanya mambo yote hayo. Wakati huo nilikua bado nipo ndani ya basi nikisubiri msongamano wa watu upungue,nilijaribu kugeuka upande wangu wa kushoto ili nimtazame yule dada lakini cha ajabu sikumuona na nilipo jaribu kuangaza macho upande wa mbele sikuweza kumuona pia. Nilijiuliza maswali mengi sana, amewezaje kushuka haraka wakati bado kuna msongamano mkubwa wa watu? Nilijisemea moyoni kisha nikanyanyuka kutoka kwenye siti yangu na kuanza kusogea taratibu kuelekea chini, kwani watu walikua wamekwisha pungua sasa.

Nilipofika chini nilielekea maeneo ya kuchimba dawa na mara baada ya hapo nikaongoza moja kwa moja hadi sehemu ya chakula. Niliagiza chipsi mayai pamoja na soda ya pepsi. Vyote hivi viligharimu kiasi cha shilingi elfu moja na mia tano. Lakini wakati nikiingiza mkono mfukoni kutoa fedha kwa ajili ya malipo,yule muhudumu alikataa kupokea ile fedha na kusema kuwa tayari nimeshalipiwa. Alinijibu huku akinyoosha kidole kwa yule mtu aliyenilipia, nilishtuka kidogo mara tu baada ya kumuona huyo mtu aliyenilipia hiyo fedha kwani alikua ni yule dada niliyekua nimekaa naye siti moja. Nilimhoji yule muhudumu naye akasema ya kuwa yule dada alikuja na kumkabidhi shilingi elfu moja mia tano, na kudai ya kuwa kuna kijana mmoja atakuja kuchukua chipsi mayai pamoja na soda ya pepsi, hivyo alivyo niona tu kutokana na mahitaji yangu akajua fika huyo kijana atakua ni mimi tu.

Niliendelea kumshangaa sana huyu dada jinsi alivyoweza kuyatambua mahitaji yangu, hata kabla sijafika na kuagiza. Wakati nikiwa bado nimesimama pale na yule muhudumu nisijue nini cha kufanya, ghafla niligonganisha macho na yule dada alikua akinitazama huku akitabasamu, ilinibidi na mimi nitabasamu tu kuonyesha ya kwamba sikua na hofu yeyote. Nilitoka mahali nilipokuwa na kumfuata pale alipokua ameketi, mara tu baada ya kufika nilimshukuru kwa msaada wake huku nikivuta kiti kilichokua pembeni kwa ajili ya kuketi, “Usijali Erick, mimi nipo kwa ajili ya kukusaidia”, alinijibu huku akiingiza mkono kwenye pochi yake, alitoa shilingi elfu kumi kisha akanipatia. Nilisita kidogo kuipokea ile fedha lakini alinilazimisha hadi nikaipokea, nilimshukuru sana naye akanijibu kama ilivyokua awali, “Usijali Erick, mimi nipo kwa ajili ya kukusaidia”. Wakati yote haya yakiendelea ghafla tulisikia mlio wa honi kuashiria ya kuwa muda wa kuondoka ulikuwa tayari umekwisha fika.

Tulinyanyuka kutoka pale tulipokua na kuelekea ndani ya basi,wakati huo nilikua nimeshikilia mfuko wangu wa chipsi nilizobakiza, lakini ile soda nilikua nimekwisha imaliza hivyo chupa niliiacha palepale mezani. Tulienda moja kwa moja hadi kwenye ile siti yetu kisha tukaketi tayari kwa safari ya kuelekea dar sasa.

Mara tu baada ya abiria wote kuingia haikuchukua mda mrefu basi letu lilianza safari ya kuelekea Dar. Nilizifungua zile chipsi nilizokua nazo ndani ya mfuko kisha nikamkaribisha yule dada, lakini alinijibu ya kuwa ameshiba hivyo niendelee tu. Haikua tabu sana kwangu hivyo nilianza kula taratibu huku nikiwa na maswali mengi sana kichwani mwangu kuhusiana na yule dada, wakati nikiwa katika hali hiyo kuna wazo lilinijia kichwani..

Itaendelea jumatatu ijayo..

Views: 1292

Replies to This Discussion

Wazo gana kaka?

Hadithi nzuri, sasa na mimi najua kinachoendelea!! Tuombe uzima tuone kitakachojiri j3 ijayo!!

Kwenda zao Dixon, hujui lolote

Dixon Kaishozi said:

Hadithi nzuri, sasa na mimi najua kinachoendelea!! Tuombe uzima tuone kitakachojiri j3 ijayo!!

Yani na wewe kwa kukurupuka hujambo. hahaha. Mimi nilikua sijaisoma hadithi hii. Leo nimepata nafasi kusoma mwanzo mpaka sehemu hii ya tatu ndiyo maana nikasema na mimi NIMEJUA kinachoendelea na si KITAKACHOENDELEA... hehee

story nzuriiiiiiiiii

teh teh teh sasa nimekuelewa

Dixon Kaishozi said:

Yani na wewe kwa kukurupuka hujambo. hahaha. Mimi nilikua sijaisoma hadithi hii. Leo nimepata nafasi kusoma mwanzo mpaka sehemu hii ya tatu ndiyo maana nikasema na mimi NIMEJUA kinachoendelea na si KITAKACHOENDELEA... hehee
hahahaa.. asante kwa kunielewa ... sasa jumatatu itakua balaaa....

Teh teh ndomaana yake, huyo Erick atajuta kukutana na huyo dada. Najua vijana wengi hupenda kukaa siti ya karibu na binti ila huyu aliye na Erick ni balaa. Erick asije akatokea dirishani j3 ijayo

Dixon Kaishozi said:

hahahaa.. asante kwa kunielewa ... sasa jumatatu itakua balaaa....
Yani hii hadithi naiona kama movie flan hivi.. hahaa.. kama Namuona Erick.. nae anamoyo sana maana mpaka hapo kama ni mimi nishazimia... dah.. hadi j3 naiona mbali..

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*