Tulonge

Mavazi ni ‘bendera’ muhimu katika uhusiano – Wataalamu

KABLA ya kumshawishi mpenzi wako akupatie burudani, ni muhimu kutazama mtindo wake wa mavazi kwanza ili ufahamu kama yuko tayari  kwa ngoma siku hiyo au la.

 

Wataalamu wa masuala ya mapenzi wanasema mitindo ya mavazi ni muhimu kutambua ikiwa mtu yuko katika hali ya kufanya mapenzi.

 

Wanasema mavazi hutoa maelezo muhimu kuhusu hisia za kimapenzi za mtu na aina ya mapenzi yanayomvutia. Kwa miaka mingi wataalamu wamehusisha mavazi ya watu na hisia zao za kimapenzi lakini sasa wanasema mitindo ya mavazi inaweza kueleza aina ya mapenzi yanayomvutia mtu baada ya wapenzi wa jinsia moja kuongezeka duniani.

 

“Enzi ambazo mavazi yalitumiwa kutambua jinsia ya mtu pekee zimepitwa na wakati. Mitindo ya mavazi anayovalia mtu inaweza kufanya atambuliwe ikiwa ni mraibu wa burudani na pia aina ya burudani anayoshabikia,” asema mwanasaikolojia Rither James wa chuo kikuu cha Mexico kwenye makala yaliyochapishwa mtandaoni.

 

“Kuna mashoga, mabasha na watu wasioshabikia burudani na hao wote unaweza kuwatambua kupitia mavazi yao,” asema mwanasaikolojia huyu.

 

Anasema kama ilivyo vigumu kwa mtu kujitokeza hadharani na kutangaza kuwa ni shoga au mwasherati, ndivyo ilivyo kwa baadhi ya watu hasa wanawake kueleza kwa matamshi kwamba wanawamezea mate jamaa fulani.

 

“Mbinu ambayo watu wengi hutumia kuelezea hisia zao ni kupitia mitindo ya mavazi. Kipusa anaweza kuvalia mavazi  ili kumwelezea mwanaume kwamba anamtamani na kumtembelea au kuhakisha kwamba anayemwinda amemwona. Kwa kawaida, sio rahisi wanawake kuelezea  wanaume kwa maneno kwamba wanawapenda mbali hutumia mavazi kutoa ujumbe huo,” asema Bw James.

 

Mawasiliano

Kulingana na wataalamu, hata wanaofanya kazi maofisini wanaweza kuwasilisha jumbe za mapenzi kupitia mavazi wanayovaa bila kufahamu kwamba wanafanya hivyo.

 

Hata hivyo Bw James anaonya watu dhidi ya kuvaa mavazi yanayoamsha hisia za mapenzi wakiwa kazini japo anakiri kwamba ni vigumu kuepuka hali hii katika ulimwengu wa sasa.

 

“Hata vazi ambalo mtu huvalia ofisini linaweza kumsisimua mwingine kimapenzi bila anayevaa kuwa na habari. Hii ni kwa sababu watu wanaamshwa hisia za kimapenzi na vitu tofauti,” asema mwanasaikolojia huyo.

 

Anaeleza kwamba ni kwa kutambua haya ambapo wataalamu wa mitindo ya mavazi wamelenga kubuni inayoamsha hisia za kimapenzi.

 

“Katika ulimwengu wa sasa, kipusa asiyevalia vazi linaloweza kumpagawisha mwanaume anachukuliwa kwamba amekosa ustaarabu,” asema.

 

Mwanamitindo wa miaka mingi Kate Small, akiri kwamba vimwana wa siku hizi hupenda mavazi ya rangi zinazong’ara ili wavutie wanaume na kupendwa.

 

“ Kuna nyakati ambazo mitindo ya mavazi hutoa maelezo kamili ya hisia za mtu,” asema na kuongeza kuwa baadhi ya watu hueleweka visivyo wanapovaa mavazi fulani.

 

Anasema tofauti na watu wengi wanaoamini mavazi yanayobana mwili ndiyo huchemsha watu kimapenzi, mavazi yasiyobana mwili yaliyonyoka vyema, huchochea hisia za kimahaba zaidi.

 

“ Watu wamepotoshwa kimawazo kwa kuvalia mavazi yanayobana mwili ili watamaniwe kimapenzi au waonekane wako tayari kwa ngoma. Lakini mavazi yasiyobana mwili, yaliyoshonwa kiustadi na yasiyofunika mwili wote ni ishara ya mtu aliye tayari kwa burudani,” asema.

 

Rangi

Anaongeza kwamba watu wengi hasa wanaume huvutiwa na wanawake wanaoonekana kuvalia mavazi nadhifu yenye rangi zinazovutia.

 

“Wanawake ambao wasipokuwa kazini huvalia mavazi nadhifu yanayowabana vizuri huonyesha kwamba sio rahisi kuachilia asali,” aeleza.

 

James na Bi Small wanakubaliana kwamba hatua ya kwanza kuelekea uhusiano wa mapenzi huwa ni mavazi.

 

“ Ni wazi kwamba kitu cha kwanza kinachofanya watu wamezewe mate kimapenzi ni  mavazi wanayovaa” asema Bi Small.

 

Kuhusiana na hili Bw James asema ni watu wasiovutiwa na mitindo ya mavazi wanaowachukulia wanaoiabudu kama wasio na maadili mema.

 

“Lakini ukweli usemwe. Kitu cha kwanza kumvutia mtu kimapenzi ni mavazi ya mwingine,” asema.

 

Hata hivyo anaongeza kuwa ni makosa kulewa na mitindo ya mavazi inayolenga kuchochea mapenzi.

 

“ Lazima uwe na mipaka. Kutembea uchi au kuvaa baadhi ya mitindo maeneo yasiyofaa na wakati usiofaa ni makosa na kukosa maadili,” asema.

 

Bi Small aliyevuma miaka ya tisini, asema hata baadhi ya wanamitindo hukosea kwa kuvaa mitindo fulani maeneo yasiyofaa na hivyo kutoa ishara mbaya kwa mashabiki wao.

 

Bw James anakosoa pia wanaobuni mavazi wakilenga mapenzi akisema hatua yao imefanya taaluma yao ieleweke vibaya na baadhi ya watu.

 

Lakini Bi Small anasisitiza kwamba kwa sababu yana sehemu yake katika mapenzi, inategemea mtu anavutiwa na mitindo gani ya mavazi.

 

“Mavazi yanaweza kuzua mvuto wa kimapenzi na hili haliwezi kupukika na simaanishi kuvaa mavazi ya aibu. Ninachomaanisha ni kuvaa mavazi yaliyoshonwa kitaalamu, wakati unaofaa na mahali panapofaa,” asisitiza.

 

“ Mpenzi wako akiwa mtanashati unajisikia vyema ukimtambulisha kwa watu,” asema.

 

Lakini anasema kuna viongozi wa kidini wanaoshikilia kuwa baadhi ya  mitindo ya mavazi inaeneza uasherati na hata kuipinga marufuku katika makanisa yao.

 

“Kuna baadhi ya dini na madhehebu yasiyoruhusu wanawake kuvaa mavazi yanayoacha sehemu za mwili zikiwa wazi. Watu wanapasa kuheshimu imani na kanuni za dini zao,” asema.

 

Hata hivyo anasema hakuna mtu anayefaa kunyimwa uhuru wa kuvaa mitindo ya mavazi anayotaka kama inavyotendeka katika baadhi ya mataifa ulimwenguni.

 

“Watu waheshimu dini zao. Hakuna makosa kufanya hivi sawa na vile sio makosa kuamua kuvaa tofautina dini ili kujenga maisha yako ya mapenzi,” asema.

Views: 1117

Replies to This Discussion

Noted with thanks Lilian!

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*