Tulonge

Mwanaume kuwahi kumaliza anapofanya tendo la kujamiiana…….!Kutoka mbegu za kiume muda mfupi baada ya kumwingilia mwanamke huitwa premature ejaculation. Huu ni udhaifu wa kawaida kwa wanaume walio wengi kwa ujumla wake, ikiwa ni pamoja na vijana. Mtaalamu Ira Sharlip anasema katika utafiti wake kuwa, ni kiasi cha asilimia 20 hadi 30 ya wanaume wa rika zote ambao wana matatizo haya.

Njia za kitabibu za kuweza kumtambua mtu mwenye udhaifu huu inaitwa Intravaginal ejaculatory latency time (IELT). Hata hivyo, mtaalamu Ira Sharlip anaongeza kwa kusema kwamba, utaratibu huu hausaidii sana kumjua mtu mwenye premature ejaculation. Kuna wanaume ambao wanamaliza katika dakika moja tu baada ya kumwingilia mwanamke na wao hudai kwamba, hawana matatizo.

  Na halafu upande mwingine, kuna wanaume ambao wanaweza kuchukua dakika 20 bila kutoa mbegu baada ya kumwingilia mwanamke. Hawa nao ni wagonjwa, kwani muda huo ni mkubwa kuliko wastani. Kwa maana nyingine ni kwamba, maana ya neno premature, zaidi zaidi liko katika mtazamo wa mhusika mwenyewe. Inategemea na mtu mwenyewe anavyotosheka kimapenzi na uwezo wake wa kujidhibiti muda wa kumaliza unapokuwa umewadia.

  Utafiti wa mwaka 2010 katika jarida la Journal of Sexual  Medicine uliona kwamba, kipimo kizuri cha premature ejaculation ni dakika 5.4. Yaani mtu akitoa mbegu baada ya dakika pungufu  ya hizo, tangu amwingilie mwanamke basi ana ugonjwa huu wa premature ejaculation.

Lakini Ian Kerner anasema kipimo ni dakika mbili. Yaani mwanaume akimaliza haja yake kabla ya dakika mbili, basi ana ugonjwa huo. Anaongeza  kwamba, watu wengi anaokabiliana nao ni wale ambao wanatumia muda mfupi chini ya dakika mbili kumaliza haja zao. Wengine hutumia sekunde 30 tu!

  Pia hata sababu za nje zinaweza kuchangia kumfanya mwanaume akawa na tatizo hili. Mtu mwenye mawazo mengi ni rahisi kukumbwa na tatizo hili. Mtu mwenye mawazo mengi anamaliza haraka mara baada ya kumwingilia mwanamke, kwa mujibu wa mtaalamu Kerner.

Lakini kumaliza kwa namna hii pia kuna uzuri wake kwamba, tumejaza dunia kwa kuwa na watu wengi. Kama watu wangekuwa wanachukua saa nzima kumaliza baada ya kumwingilia mwanamke, dunia ingekuwa na uadimu wa watu!

  Washauri nasaha wanaojihusisha na ushauri wa kimapenzi na matibabu wanatoa tiba mbalimbali kwa ajili ya watu wenye wasiwasi; wasiwasi ambao huwafanya wawe wanamaliza haraka sana baada ya kumwingilia mwanamke.

Kuna dawa ambayo mgonjwa akipewa zinamsaidia kurefusha muda wa kuendelea na tendo, baada ya kumwingilia mwanamke. Dawa hizo ni kama zile za kupooza msongo wa mawazo. Pia kuna mazoezi ambayo yanashauriwa kufanywa. Mazoezi haya humsaidia mtu  kujenga upya mkabala wa namna anavyochukulia tendo.

Kwa wale wakazi wa Dar wanaweza kutembelea ofisi zetu za Faji zilizoko Tabata Kimanga ambapo tunatoa tiba ya tatizo hili pamoja na matatizo mengine yanayohitaji ushauri wa kisaikolojia na yale ya tiba yatilifu (Tiba mbadala).

  Lakini pia njia iliyo rahisi zaidi ili kutokuwa mwepesi wa kumaliza haraka ni kujizoeza kuacha kulifikiria tendo hilo la ngono unapokaribia kufikia kileleni (kwa kufanya pole pole zaidi au kufikiria mambo mengine ya nje kama ya mpira, mfano Yanga na Simba au Manchester na Chelsea). Jenga mazoea kufanya namna hiyo. Ukizoea itakuwa ni kama kitu cha kawaida kwa kujikaza kisabuni na kuhakikisha unamsubiri mwenzio ili mwende pamoja kileleni.

  Kila kitu ni kujifunza. Ukijizoeza kujikakamua bila kumaliza hata katika hali ya ham ya juu kwa kumsubiri mpenzi wako, tatizo la premature ejaculation litakuwa limethibitiwa. Hii ni kwa mujibu wa mtaalamu Prosterman.

Chanzo:Jamii Forums (JF)

Views: 7007

Replies to This Discussion

duuh, hiyo noma, nifikilie soka wakati niko bustani ya heden mbona ngumu sana.

ukiwa kwenye mchezo kufikiri kitu kingine kama soka ni ngumu sana.

-Msiwe mnakimbilia kupandana kabla hujamkoleza mkeo. Nikisema kumkoleza namaanisha kumuandaa vya kutosha hadi kufikia hatua ya kutamani kuivuta Flash Disk ili aiingize kwenye USB Port (Nadhani mmenielewa). Hii itamfanya mkeo afike haraka sana.

-Pia inabidi uwe unaanza kwa speed ndogo (taratibu) then unadumu na speed hiyo ndogo kwa muda mrefu ili kumkoleza zaidi. Siyo unaanza kwa fujo utadhani unacheza ndombolo ya solo. Baadae baada ya mkeo kufika unaweza ukaanza kuongeza speed taratibu hadi unafikia speed 190.

-Kuna hiyo ya kujisahaulisha kama upo kwenye hilo tendo. Ila hii inahitaji moyo wa paka. Lile tendo ni balaa ndugu zangu. Kui-force akaili ifikirie mengine ni kazi ngumu. Ila ukiweza inasaidia sana kuchelewa kufika.

-Pia kutumia mpira (condom) huwa inasaidia kuchelewa kufika. Kama haiwaboi (mke/mume) mnaweza itumia.

Kwa kufuata haya, na kama mwanaume huna matatizo mengine lazima utakua wa mwisho kufika. Siyo mwanaume unafika haraka haraka kama kuku.

Kama hujaoa HAKUNA kufanya mapenzi, subiri uoe kwanza kama mimi.

Wewe Tulonge,haya mambo inategemea pia na msichana au mwanamke ana umbile gani,kama hawa wilio jaliwa umbile zuri,hata sec haipiti ushakojoa

Dogo hapo wanaume wamekusoma, heheheheheheeee "Siyo mwanaume unafika haraka haraka kama kuku"   

Hahahahhahaaaa dogo siku hz nimekua mtaalam kiaina

Christer said:

Dogo hapo wanaume wamekusoma, heheheheheheeee "Siyo mwanaume unafika haraka haraka kama kuku"   

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*