Tulonge

JAPOKUWA wanawake bado hawajapita wanaume katika suala la kutoka nje ya ndoa, idadi ya wanawake wanaotoka nje ya ndoa na kutafuta mabwana wengine ili kuwatimizia haja yao ya tendo la ndo imeongezeka, kwa hapa nyumbani inasemekana kati ya asilimia 14-16 ya wanawake walio kwenye ndoa wameshalala na wanaume wengine takribani mara moja katika maisha yao ya ndoa.

Wanaume wapo juu kidogo, kati ya asilimia 20-30, wameshatoka na wanawake wengine, wengi wao wakiwa ni wanawake ambao wanafanya nao kazi au marafiki wa karibu. Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayosababisha wanawake watike nje ya ndoa.

1. Uhaba wa tendo la ndoa.
Unakumbuka wakati mnaanza kutongozana na kuchumbiana, meseji na simu haziishi bebi nakupenda bebi sijui nini. Ghafla watoto anapata mimba, watoto wanazaliwa, majukumu yanaongezeka, kazi zinazidi. Ukirudi nyumbani wewe ni kula kuoga na kulala, unasahau kwamba wanawake siku zote wanataka wajione wanatakwa, kama unajifanya humtaki na humuonyeshi kama yeye ni mzuri, ataenda kutafuta mtu ambaye anamuonyesha kwamba anamtaka. Achana na mambo ya kujifanya mtu mzima, mbusu mke wako hadharani, mshike mkoni, mtumie meseji za uchokozi. Ukifanya hivyo utajikuta damu bado inachemka na bado mnatakana hata kama mna miaka 70.

2. Kuonyesha utundu.
Asikudanganye mtu kila msichana ana utundu wake ambao ameuficha mahali anasubiri uuvumbue.
Kama anajifanya mwanamke wa heshima, mnazima taa ndio mnaendelea na mambo yenu, anajifanya anaona aibu na wewe unamuamini hivyo hivyo. Ni kazi yako wewe mwanaume kuutafuta utundu wa mkeo uko wapi, mfanye awe huru kufanya jambo analotaka kufanya na wewe na wala usimjaji kwamba amejifunzia wapi. Usipofanya hivyo ataenda kumtafuta jamaa ambaye atamfanya awe huru kuonyesha utaalamu wake (inner sex kitten)

3. Kujithamini (Self-esteem)
Tendo la ndo linamfanya mwanamke ajithamini zaidi, ajione mrembo na kwamaba anapendwa. Kama mke au demu wako anaonyesha kutojithamini na kwambwa wewe utakuwa unatamani au unapenda kulala na wasichana wazuri kuliko yeye, ni kazi yako kumfanya ajisikie mzuri, ajithamini nakujipenda zaidi. Usipofanya hivyo kuna jamaa huko nje ataropoka, duh! leo umependeza na mambo yanaweza kuishia pengine.

4. Kulipiza kisasi
Hapana, sio kulipiza kisasi kwasababu amekukamata kwamba umelala na mwanamke mwingine, wanawake wanaweza kuona kuwa namna ya kukuumiza ni kwenda kulala na mwanaume mwingine kwa kulipiza kisasi kwa kosa ulilofanya, iwe ni kwamba ulikamatwa ukidanganya, umemuumiza moyo wake, na anapunguza uaminifu kwako na kutojali kukuumiza wewe. Ili kurudisha uaminifu, haitoshi kumwambia tu kwama samahani, na matendo yako yanatakiwa yabadilike.

Jaribu kuzingatia mambo haya na utaondoa vishawishi vya kusababisha mke wako aende kutimiza haja yake ya tendo la ndoa na mwanaume mwingine.

Chanzo: thehabari.com

Views: 1456

Replies to This Discussion

Asante sana

Asante kwa ushauri!

Wanawake siku zote wanataka wajione wanatakwa, mbusu mke wako hadharani, mshike mkono, mtumie meseji za uchokozi"  Hapa sina neno ni ukweli mtupu!

Wanawake wanapenda kusifiwa kuwa wazuri au wamependeza na zawadi ndogondogo hata kama hazina thamani wanafrahi kweli pia hawapendi kudanganywa.

Kiukweli wanawake wanapenda sana kusifiwa kudekezwa kujaliwa muonyeshe unampenda hasa mbele za watu yaani kichwa kitavimba kwa misifa na atajiona yeye ndio kila kitu hakuna zaid yake ukijifanya uko busy sana na mambo yako humjali hata muuza mboga pale gengeni atamchukuwa maana kila akienda sokoni jamaa muuza mchicha anamsifia basi kiulaiiini anajichukulia hahahah kidume ukipita jamaa anajisifu bwege yulee nimeshamgongea hahahah.

 

Kudekezwa! @ Omary, hilo nalo neno haswaaaaaaaaaa!

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*