Tulonge

Utafiti umeonyesha baadhi ya vitu vilivyosababisha ndoa za babu zetu zidumu ilikuwa babu na bibi kulala pamoja kwenye vitanda, ngozi za wanyama au mikeka yenye ukubwa usiozidi futi 2.5. Umbali wa futi 2.5 uliwawezesha wanandoa kuwa pamoja na kugusana usiku kucha. Hii iliwalazimisha waongee hata kama wamegombana mchana, maana bila kusema sogea huko huwezi kupata nafasi ya kulala. baridi ilivyokuwa inaongezeka kunapokaribia kucha iliwalazimisha wasameheane hata bila ya kuombana samahani, maana kugusana kule kuliwapa joto lililokuwa linafuta lenyewe makosa yote waliyofanyiana mchana na kuanza upya.

Vitanda vyetu vya 6 x 6 vinakwenda anti-clockwise na kazi iliyokuwa inafanywa na vitanda vya akina babu. Vitanda vyetu havina ubavu wa kufuta makosa ya wanandoa waliyofanyiana mchana. Kila mtu anakuwa kwenye kona ya 6x6 na kujisikia aibu kuanza kumgusa mwenzie, nani aanze kupandisha mguu kwenye paja la mwenzie wakati kulikuwa na ugonvi? Ngoma inakuwa droo hadi asubuhi na ugonvi ukiwa palepale na kila mtu akijfanya nunda wa kukataa kujishusha kwa kusema samahani ama kupapasa mwingine.

Rudisheni vitanda vyenu kwa fundi seremali avipunguze viwe 3 x 6 ili viweze kuwasuluhisha wanandoa mnapokoseana sio kwenda kwa mshenga, shoga, wazazi, majirani kutafuta suluhu.

Views: 1210

Replies to This Discussion

Asante sana tulonge UTAFITI wako ni wa kweli kabisa atakae kataa analjambo ake, kwa upande wangu sitepeleka kwa fundi kitanda changu bali nitakihamishia kwa watoto halafu nitampa fundi selema kazi ya kunitengenezea 2.5x6 nadhani visingizio vya kuchoshwa na kazi za mchana kutwa vitaisha.

Kaka Omari upo hapoooo? Jamaa leo kalonga hii ndio mada kali kuliko zote tangu nijiunge na tulonge.

it make some sense@tulonge

Mjata umetisha sana, yani 2.5x6 si mtaweza anguka chini hahhaahaaaa

Naam Kaka Daffa nipo kiukweli hili sina ubishi nalo naunga hoja kani vitanda vile vya zamani hata siku mjukuu umejikuta umesinzia chumbani kwa Babu na Bibi utajikuta umelala juu ya bibi au babu maana hakuna nafasi yako kitanda kidogo hahahah mtafiti wetu nampongeza sana kweli uliuvalia njuga utafiti wako hongera.

Kuna kaukweli. inasemekana hata appointment za bibi/babu, baba/mama zetu zilikua za kweli tupu kama wamekutana leo, wanapanga waonanane tena baada ya wiki saa flani mahala flani na baada ya wiki wanakutana km walivopanga hakukuwa na simu na huwezi kwenda kwao kumtafuta kwaio lazma iwe hivyo na wanakutana bila tatizo. Appointment zetu sasa simu/txt/sijui whatsapp etc na bado appointment zinabuma kwanza hatupangi hata lini kuonana 7bb simu zipo tunawasiliana 24/7 na ikipangwa ni kwa simu/txt etc siku ikifika appointment inavunjika mtu anapiga tu simu excuse pipa zimaaaaaaaaaa au mtu anafika masaa mawili baada ya muda ulopangwa, akipigiwa simu mbona hufiki, niko njiani baby, kuna foleni baby, karibu nafika usiwe na waswas kumbe ndo kwanza yuko home anaoga...................Maendeleo yetu bure kabisa bora Enzi zile.

Hapo umenena, cc huwa tunalaliana juu hata kitanda kiwe kikubwa vp haahaahahaa

Umenena Joan... Mie changu kidogo (4x6) tena winter season ndio penyewe kwa zero distance, baada ya kupigwa na baridi/barafu huko nje kila mtu ataka joto. Hapa 6x6 haina soko
Lol.... Mke mdogo umenifurahisha. Ni kweli appointments za zamani hazikuathiriwa na simu. Kwa upande mwingine nafikiri uongo imekuwa kasumba iliyojijenga kwa wengi hasa jamii yetu bongo. Hapa napoishi, mtu akikupa appointment kuivunja ni nadra sana. Mwingereza akikwambia tukutane pahala fulani muda fulani, utashangaa unafika muda huo na wamkuta mwenzio keshafika kabla ya muda mlopangana tena anakupokea koti na kuvuta kiti kukwambia ukae. Iwapo pahala pa kukutana ni safari ya dakika 40 basi mtu yuko tayari kuondoka masaa 2 kabla ili kufidia traffic, etc. Na hiyo haijalishi ndio first date or forth date. Wapo waingereza wa longolongo lakini wachache na wa longolongo utamjua tokea mwanzo kwani hawa watu inapokuja kwenye mapenzi utasema wamelogwa/wagonjwa. Teh teh teh... Baadhi wako radhi amuache mzazi wake mgonjwa hoi kitandani ili aende kukutana na mpenzi, hasa vidumeChrister said:

Kuna kaukweli. inasemekana hata appointment za bibi/babu, baba/mama zetu zilikua za kweli tupu kama wamekutana leo, wanapanga waonanane tena baada ya wiki saa flani mahala flani na baada ya wiki wanakutana km walivopanga hakukuwa na simu na huwezi kwenda kwao kumtafuta kwaio lazma iwe hivyo na wanakutana bila tatizo. Appointment zetu sasa simu/txt/sijui whatsapp etc na bado appointment zinabuma kwanza hatupangi hata lini kuonana 7bb simu zipo tunawasiliana 24/7 na ikipangwa ni kwa simu/txt etc siku ikifika appointment inavunjika mtu anapiga tu simu excuse pipa zimaaaaaaaaaa au mtu anafika masaa mawili baada ya muda ulopangwa, akipigiwa simu mbona hufiki, niko njiani baby, kuna foleni baby, karibu nafika usiwe na waswas kumbe ndo kwanza yuko home anaoga...................Maendeleo yetu bure kabisa bora Enzi zile.

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*