Tulonge

Kiafya

Tendo la ndoa ni moja kati ya mazoezi ya mwili. Wataalamu wanasema kwamba, unapofanya tendo hilo mara tatu kwa wiki husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini na pia endapo mtu atafanya tendo mara tatu kwa wiki kwa kipindi cha mwaka mzima ni sawa na kukimbia maili 75.Tendo la ndoa huongeza takriban vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 kiwanjani.

Kuongeza mwendo wa damu

Tendo la ndoa husaidia kuongeza kasi ya mtiririko wa damu kwenye ubongo na sehemu nyingine ya viungo vya mwili, hii huchangia kuongeza kasi ya mapigo ya moyo na kuboresha mfumo wa upumuaji. Msukumo thabiti wa damu mpya yenye oxygen na homoni zenye chembe chembe hai zinapopenya kwenye mishipa ya damu husaidia katika uunguzaji wa chakula, pia huondoa kiasi cha uchafu ambao ungesababisha mishipa na kushindwa kufanya kazi na kumfanya mwanadamu apate maumivu ya mwili.

Hupunguza mafuta yenye kileo (Cholesterol)

Tendo la ndoa huweka sawa uwiano wa mafuta yenye kileo (Cholesterol) nzuri na cholesterol mbaya na wakati huo hupunguza kwa ujumla kiasi cha mafuta yenye kileo mwilini.

Kupunguza maumivu.

Wakati wa kufanya mapenzi, homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini ambayo husababisha kuzalishwa kwa homoni iitwayo endorphin ambazo hupunguza maumivu kama vile kuvimba sehemu za viungo (arthritis) maumivu ya shingo (Whiplash) na maumivu ya kichwa.

Ulinzi wa tezi ya kibofu (mwanaume)

Majimaji yanayozalishwa katika tezi ya kibofu (prostate) yakizidi husababisha kuleta matatizo mwilini. Tendo la ndoa la mpangilio huondoa uzalishaji wa majimaji hayo yenye madhara. Mabadiliko ya ghafla ya tendo la ndoa huelekea kuleta matatizo yahusianayo na tezi ya prostate.

Kupunguza mfadhaiko wa moyo.

Kujitosheleza na kupumzisha mwili baada ya tendo la ndoa ni muhimu kwa kutuliza akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini. Watu wenye kushiriki tendo la ndoa wanatajwa kushinda mfadhaiko na kupata usingizi mnono hasa mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi.

Huongeza uzalishaji wa homoni za kiume(testosterone) na za kike (Oestogen). Faida nyingine inayopatika ni kuongeza uzalishaji wa homoni za kiume na za kike likiwemo suala zima la msukumo wa kufanya tendo hilo ambapo mhusika hutosheka zaidi ya yule ambaye hana mazoea ya kufanya mapenzi. Hata hivyo, baadhi ya madaktari wamegundua kwamba ongezeko la homoni za kiume/ kike huweza kuwakinga wanadamu na magonjwa ya moyo.Kuishi muda mrefu huku ukionekana kijanaWakati wa tendo la ndoa homoni iitwayo DHEA huzalishwa mwili mzima. Hii husaidia msisimko wa mapenzi kuongezeka. Kutokana na elimu hiyo DHEA ni kemikali yenye nguvu duniani ambayo husaidia kuweka sawa kinga ya mwili, huongeza ufahamu, kuimarisha mifupa, kutengeneza na kuimarisha afya na kuimarisha mishipa ya moyo (Cardiovascular).

Hupunguza baridi na mafua.

Elimu inaonesha kuwa wanaofanya tendo la ndoa mara moja au mbili kwa wiki huongeza 30% ya uzalishaji wa chembe chembe hai za mwili ziitwazo Immunogloulin A ambazo huwa na kazi ya kuulinda mwili dhidi ya magonjwa. Hizo ni faida chache tu za kufanya tendo la ndoa.

NB : Jambo kubwa la kuzingatia ni kuwa faida hizi hupatikana kwa ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na hofu ya kufumaniwa au kuumbuliwa

Views: 8054

Replies to This Discussion

nitakuja kuzisoma taratibu,

itabidi sasa niweke dozi kama ya panadol, hasubui mchana na jioni, kila siku ili hzo faida nizipate mara mbili zaidi.

Teh teh teh Geoffrey umepinda ww

Thanx for info. Belita

Christer siyo unashukuru tu, inabidi uongeze speed ili uzipate hizo faida

Nilijua tu ukiona nime-comment lazima unijibu dogo, teheeeeeeee!!!!!!!!1

Ndomaana yake, inabidi uanze kupiga kutwa mara tatu dogo.Kama dozi ya Panado

Hahahhahahhaaaaaaaaaaa sasa hata kazi hakuna kufanya jamani, si itakua kasheshe? wengine wanandoa mume yuko Mbeya, mke Dar, inakuwaje hapo?

Christer kwa hao wa hivyo inabidi wapate wasaidizi. Watu kama kina Kunambi na Alfan huwa wanapenda sana kutoa msaada kwa watu ambao hawapo na wenzi wao kwa kipindi kirefy ili kuhakikisha hawakosi faida za tendo hilo.

Alafu ukipata "kimoja" Asubuhi kabla ya kwenda kazini ... siku huwa nzuri sana tofauti na siku unayoenda kazini bila "kimya kimya".. Faida ni nyingi aise... nikuongeza kasi tu!!

Mwenye nyumba akikosekana nyumbani basi nyumba inavamiwa na buibui na kuweka utandu, vile vile mke akikosa mume nae buibui lazima waweke utandu.....lazima jirani asaidie ili nyumba ifanyiwe usafi hahahahaha!

@Dixon unasema kweli, wanaume mara nyingine wakati wa kuamka asubuhi lazima uwe na ile inaitwa morning wood, kwa hiyo ukipata kimoja sio mbaya kabisa!

Ha haa haa haaaa.... kaka Eddie hiyo kali.

Geoffrey, Dixon & Dismas mnaniua na comments zenu. Geoffrey, hiyo dose ya asubuhi, mchana na jioni itabidi baada ya one week utashindwa kutembea. Teh teh teh

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*