Tags:
Kwa kweli katika Bongo Fleva ya sasa sioni wa kuchukua tuzo hizo kubwa. Tatizo ni DJ's wetu kuwabeba watu ambao mimi nawaita "MFANO WA WANAMUZIKI". Na wale ambao ni wanamuziki hawapewi nafasi. Ukitaka kujua kuwa Tanzania ubabaishaji ni mwingi, angalia ile wanaita BONGO STAR SEARCH. wale wambao walishinda na kupewa nafasi ya kutengeneza muziki katika studio fulani fulani, leo hii hawapo katika ramani ya muziki. Ni kichekesho kwa kweli, Jummane Iddi mfano mmoja wapo, yule jamaa nafikiri alipewa ushindi kwa kuangaliwa sura yake inayotia huruma, na wala si vinginevyo. Nasema hivyo kwa sababu uwezo wake kimuziki ni mdogo kuliko maelezo. Haya mwingine huyo kwenye picha ya huu mjadala, sijui kama atafikisha hata miaka miwili akibaki katika ramani ya muziki. Yaani mtu anawika mwezi mmoja, akishapotea ndio moja kwa moja, kuja kumuona tena labda mkutane naye kwenye daladala. Naipenda Tanzania, lakini ku-support wababaishaji siwezi.
PamoJah katika kujenga nchi
© 2021 Created by Tulonge.
Powered by